Jamhuri Ya China: Nchi za Asia Mashariki

Jamhuri ya China (pia: Taiwan) ni nchi ya visiwani katika Asia ya Mashariki upande wa kusini-mashariki wa China bara.

Makala hii yaeleza habari za Taiwan. Kwa habari za Jamhuri ya Watu wa China au China bara tazama hapa
Jamhuri ya China

Eneo

Sehemu kubwa ya eneo lililo chini ya serikali ya Jamhuri ya China ni kisiwa cha Taiwan, lakini pia lina visiwa vidogo mbele ya mwambao wa China bara.

Mbali ya visiwa mbalimbali katika Bahari ya China visivyo na wakazi, upande wa magharibi kuna mafunguvisiwa matatu:

  • Visiwa vya Wavuvi ama Pescadores - (Penghu, 澎湖列島)
  • Quemoy (Kinmen, 金門)
  • Matsu (馬祖列島)

Historia

Jamhuri ya China iliundwa mwaka 1912 mjini Nanking baada ya mapinduzi ya China ya 1911 iliyomaliza utawala wa kifalme wa nasaba ya Qing. Sun Yat-sen akawa rais wa kwanza.

Serikali ya jamhuri ilidai mamlaka juu ya China yote ingawa hali halisi viongozi wa kijeshi na wapinzani mbalimbali walishika utawala katika maeneo kadhaa.

Nchi jinsi ilivyo sasa ni tokeo la vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China iliyokwisha mwaka 1949 na ushindi wa Wakomunisti chini ya Mao Zedong na kuundwa kwa Jamhuri ya Watu wa China huko Beijing.

Wakomunisti walifukuza serikali ya chama cha Kuomintang iliyoongoza Jamhuri ya China.

Mwaka 1949 serikali ya Kuomintang chini ya jenerali Chiang Kai-shek na mabaki ya jeshi lake pamoja na wafuasi wengi ilihamia Taiwan walipoendelea kutawala. Wakomunisti walikosa nguvu ya kuwafuata hadi kwenye visiwa kutokana na vitisho vya Marekani.

Hivyo serikali katika Taiwan iliendelea kujiita "serikali ya China" na kutangaza shabaha yake kuwa ukombozi wa China yote.

Hali halisi utawala wa Wakomunisti barani uliimarika na mipango yote kinyume chake ilionekana kama ndoto. Lakini kwa miaka minghi serikali ya Taipeh ilichukua nafasi ya China yote kimataifa.

Jamhuri ya China ilikuwa kati ya nchi zilizoanzisha Umoja wa Mataifa mwaka 1945 na serikali ya Kuomintang iliendelea kushika kiti cha China hadi mwaka 1971.

Tarehe 25 Oktoba 1971 Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua ya kuwa Jamhuri ya Watu wa China iwe mwakilishi wa China bara kwenye UM, hivyo Jamhuri ya China alijiondoa.

Siku hizi uhusiano kati ya China zote mbili ni mgumu. Wananchi wengi wa Jamhuri ya China wameanza kujitazama kama Wataiwani, si Wachina tena. Lakini China inadai nchi hii ni sehemu yake.

Nchi imefaulu sana kiuchumi, ikishika nafasi ya 15 duniani.

Watu

Wakazi ni 23,780,452 (2018), hivyo msongamano ni mkubwa sana.

Wengi wao (zaidi ya 95%) ni Wachina waliotokana na wale waliohamia kisiwani hasa kuanzia karne ya 17. Wenyeji ni 2% tu.

Kichina ndiyo lugha rasmi na ya taifa, pia lugha ya kawaida katika lahaja zake mbalimbali. Lugha za wenyeji, ambazo ni kati ya lugha za Austronesia, zinazidi kufa.

Nchi inaheshimu uhuru wa dini na wakazi wengi (81.3%) wanayo moja ya kwao. Serikali inazitambua 26.

Yenye wafuasi wengi ni Ubuddha (35.1%), Utao (33%), Ukristo (3.9%, wakiwemo Waprotestanti 2.6% na Wakatoliki 1.3%) na Yiguandao (3.5). Wenyeji wengi ni Wakristo (64%).

Tazama pia

Viungo vya nje

Jamhuri Ya China: Eneo, Historia, Watu 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Taarifa za jumla

Serikali

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Jamhuri Ya China: Eneo, Historia, Watu  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya China kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Jamhuri Ya China EneoJamhuri Ya China HistoriaJamhuri Ya China WatuJamhuri Ya China Tazama piaJamhuri Ya China Viungo vya njeJamhuri Ya ChinaAsia ya MasharikiBaraChinaKusiniMasharikiNchi ya visiwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

ArudhiVieleziUfahamuVisakaleMapambano ya uhuru TanganyikaMtiUti wa mgongoAgano la KaleOrodha ya visiwa vya TanzaniaFananiAlomofuSoko la watumwaNguzo tano za UislamuNomino za kawaidaMkoa wa ManyaraKipindupinduMunguMkoa wa MwanzaYoung Africans S.C.Ugonjwa wa kuharaUbadilishaji msimboMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaUlemavuMatumizi ya lugha ya KiswahiliMshororoNgono zembeSumbawanga (mji)Zama za MaweNomino za pekeeMalariaUzazi wa mpango kwa njia asiliaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaMkoa wa DodomaKalenda ya KiislamuWarakaMfumo katika sokaVenance Salvatory MabeyoWizara za Serikali ya TanzaniaMbossoKutoa taka za mwiliMnyoo-matumbo MkubwaMtakatifu MarkoSaidi NtibazonkizaToharaChupaFamiliaKizunguzunguAli Hassan MwinyiMnazi (mti)Mazoezi ya mwiliNdege (mnyama)Vivumishi vya pekeeJogooHali ya hewaKiunzi cha mifupaShuleOrodha ya nchi za AfrikaVielezi vya wakatiHistoria ya KiswahiliNguruwe-kayaWamasaiOrodha ya viwanja vya ndege nchini TanzaniaBungeChuo Kikuu cha MuhimbiliKing'amuziBawasiriMofimuNuktambiliTungoWabena (Tanzania)Uvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiAina za manenoUchorajiMamba (mnyama)Kenge🡆 More