Familia

Familia (kutoka Kilatini familia) ni kikundi cha watu wanaokaa pamoja kama baba, mama na watoto.

Kikundi hicho mara yingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la ukoo unaounganisha watu wenye asili katika uzazi wa pamoja.

Familia
Familia pana ya baba, mama, watoto na ndugu wengine, Basankusu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Familia
Familia pana ya machotara huko Cape Town, Afrika Kusini.
Familia
Sanamu ya Familia: wazazi na mtoto.
Familia
Mama na watoto, Berlin, Ujerumani, 1962.
Familia
Baba na watoto, Kopperston, Marekani, 1946.

Aina za familia

Aina za familia zinatofautiana duniani kutokana na utamaduni na hali ya jamii.

Katika nchi nyingi za Afrika familia ndogo ya baba, mama na watoto kwa kawaida ni sehemu tu ya familia kubwa zaidi pamoja na ndugu wa baba na mama, akina babu na bibi na kadhalika. Lakini hata Afrika kuna taratibu tofautitofauti kama ni ndugu wa baba au ndugu wa mama wanaotazamiwa kuwa karibu zaidi kwa watoto wa familia ndogo.

Vilevile kuna tofauti kama muundo wa kawaida ni mume mmoja na wake wengi na kila mmoja akiwa na watoto wake tena.

Katika jamii za nchi zilizopita kwenye mapinduzi ya viwandani kama Ulaya na Marekani familia inamaanisha hasa familia ndogo inayokaa pamoja katika nyumba. Ukoo haujapotea lakini umuhimu wake umepungua sana na mara nyingi ni chaguo la watu ndani ya ukoo kama wanapenda kujumuiana na ndugu zao au la.

Katika mazingira ya miji mikubwa au pale ambako koo za kale zimeporomoka na kuachana kuna jumuiya ndogo sana kama mama na watoto ambao ni familia bila baba au wanaume. Aina hii ya familia yenye mzazi mmoja tu imepatikana pia kama familia ya baba na watoto kama utamaduni unamruhusu baba peke yake kulea watoto.

Katika mazingira ya umaskini, vita au mabadiliko ya haraka sana kuna pia watoto wengi wanaoishi kwa bibi au babu na hata hali hii ni aina ya familia.

Viungo vya nje

Familia 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Familia  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Familia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BabaKilatiniKundiMamaUkooUzaziWatotoWatu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoNdiziMatiniMkoa wa TaboraWahaBinadamuChe GuevaraMsamiatiRitifaaWikipediaWilliam RutoMuundo wa inshaNdovuYouTubeSkeliUchawiManispaaShangaziVitenzi vishiriki vipungufuBungeMtaalaOrodha ya Watakatifu WakristoKiini cha atomuHoma ya manjanoTarafaUjerumaniMaadiliChawaKigoma-UjijiUongoziHistoria ya BurundiUharibifu wa mazingiraTambikoViwakilishiIdhaa ya Kiswahili ya Radio TehranOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaKiraiAthari za muda mrefu za pombeMajigamboLingua frankaIstanbulShairiDhahabuUsafi wa mazingiraMkoa wa MbeyaShuleBenjamin MkapaLugha za KibantuMkataba wa Helgoland-ZanzibarAsili ya KiswahiliBikira MariaClatous ChamaMbadili jinsiaMobutu Sese SekoMadhehebuMiundombinu ya kijani katika nchi ya Kenya, mji wa NairobiKilwa KisiwaniNomino za wingiMazungumzoNgano (hadithi)MachweoFasihiDodoma MakuluBenki ya DuniaUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020WachaggaTenziJuxUkatili wa kijinsiaUnyevuangaApril Jackson🡆 More