Kuwait

Kuwait (kwa Kiarabu: الكويت ‎) ni nchi ndogo ya Uarabuni kwenye Ghuba ya Uajemi.

Kuwait
Kuwait
Ramani ya Kuwait
Kuwait
Kuwait inavyoonekana kutoka angani (2001)
Kuwait
Jiji la Kuwait

Imepakana na Irak na Saudia.

Jiografia

Karibu nchi yote ni jangwa, lakini kuna pwani na visiwa vidogo.

Historia

Historia ya Kuwait ilianza kama utemi mdogo chini ya familia ya Al-Sabah iliyokuwa chini ya Sultani wa Uturuki aliyetawala nchi jirani ya Irak hadi vita kuu ya kwanza ya dunia.

Tangu kuingia kwa Waingereza katika nchi za ghuba, mwaka 1899 watawala wa Kuwait walijiweka chini ya ulinzi wa Uingereza kwa sababu waliuona afadhali kuliko ukuu wa Uturuki.

Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi ya Waosmani na baadaye dhidi ya Saudia.

Baada ya kuporomoka wa dola la Uturuki Kuwait iliendelea kama nchi lindwa chini ya Uingereza hadi kupata uhuru wake tarehe 19 Juni 1961.

Katika miaka iliyofuata Kuwait iliona madai ya Irak ya kuwa tangu zamani Kuwait ni mkoa wake uliotengwa na ukoloni.

Tarehe 2 Agosti 1990 dikteta wa Irak Saddam Hussein alivamia Kuwait na kuiteka. Katika vita ya pili ya ghuba Marekani pamoja na nchi nyingine ilishambulia jeshi la Irak katika Kuwait na kurudisha serikali ya Emir al Sabah.

Watu

Kati ya wakazi 4,044,500 asilimia 30 pekee ni wananchi au Wakuwait wenyewe. Wengine wote ni watu waliokuja kufanya kazi na kuishi hapo. Pamoja na wahamiaji kutoka nchi jirani, 60% ya wakazi ni Waarabu. Zaidi ya 30% tena wana asili ya India au nchi nyingine za Asia. Waafrika ni 76,698.

Lugha rasmi ni Kiarabu; wananchi wanakiongea kwa lahaja maalumu. Kiingereza pia kinatumika hasa, hasa katika biashara.

Upande wa dini, wananchi karibu wote ni Waislamu, hasa Wasuni (70%), lakini pia Washia (30%). Ndiyo dini rasmi. Wakristo ni zaidi ya 10%, lakini karibu wote ni wahamiaji. Wahindu kutoka India ni wengi zaidi kidogo (karibu 15%). Wabuddha ni 2%.

Uchumi

Nchi ni tajiri kutokana na wingi wa mafuta ya petroli yaliyopo chini ya ardhi yake. Akiba zake ni kama 10% za akiba za dunia yote. Kabla ya kupatikana kwa mafuta mwaka 1938 nchi ilikuwa maskini lakini sasa ni kati ya nchi tajiri zaidi duniani.

Kabla ya kugunduliwa kwa mafuta palikuwa na kilimo kidogo sana, halafu ufugaji na hasa uvuvi baharini.

Tazama pia

Marejeo

  • Abu-Hakima, Ahmad Mustafa, mhariri (1983). [[[:Kigezo:Google books]] The Modern History of Kuwait: 1750-1965]. London: Luzac & Company. ISBN 9780718902599. 
  • Abu-Hakima, Ahmad Mustafa, mhariri (1965). [[[:Kigezo:Google books]] History of Eastern Arabia, 1750-1800: The rise and development of Bahrain and Kuwait]. Bahrain: Khayats. 
  • Tétreault, Mary Ann, mhariri (2000). [[[:Kigezo:Google books]] Stories of Democracy: Politics and Society in Contemporary Kuwait]. New York: Columbia University Press. ISBN 0231114885. 

Viungo vya nje

Kuwait 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Kuwait  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kuwait kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kuwait JiografiaKuwait HistoriaKuwait WatuKuwait UchumiKuwait Tazama piaKuwait MarejeoKuwait Viungo vya njeKuwaitGhuba ya UajemiKiarabuUarabuni

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Millard AyoKiambishi awaliMaajabu ya duniaLa LigaTenziKinjikitile NgwaleKupatwa kwa JuaMfumo wa homoniMatendo ya MitumeHuzuniTamathali za semiFonimuShangaziHekaya za AbunuwasiHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoOrodha ya nchi kufuatana na wakaziWikipediaMkoa wa RuvumaIdi AminUandishi wa ripotiAzimio la ArushaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniKunguniUti wa mgongoMoyoManispaaGhanaNabii IsayaNomino za jumlaMapenziSayariTendo la ndoaMsamiatiHoma ya manjanoMuunganoKifua kikuuKifaaSoga (hadithi)KengeSimu za mikononiKiswahiliHuduma ya ujumbe mfupiZama za MaweTungo kishaziJoyce Lazaro NdalichakoFonolojiaNg'ombeDhanaSemiOrodha ya Watakatifu WakristoAla ya muzikiMmomonyokoMkanda wa jeshiKishazi huruWaluoMkondo wa umemeMartha MwaipajaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaNadhariaViwakilishi vya kumilikiMuziki wa hip hopLingua frankaMaigizoKhadija KopaIsraeli ya KaleZuchuAina za manenoSintaksiAgano JipyaKilatiniWapogoloRaiaMkoa wa NjombeNguvaSensa🡆 More