Mongolia

Mongolia (kwa Kimongolia: Монгол Улс, mongol uls) ni nchi ya bara la Asia.

Mongolia

Imepakana na nchi za Urusi na Uchina.

Ni nchi kubwa ya 19 duniani lakini kuna wakazi wachache tuː jumla milioni 2.6 hivyo msongamano wa watu ni mdogo sana.

Sehemu za kusini mwa Mongolia ya kihistoria ziko ndani ya Jamhuri ya Watu wa China.

Jiografia

Mongolia 
Ramani ya Mongolia

Mongolia ni nchi ya mbuga yabisi, majangwa na milima inayofikia kimo cha mita 4,374 juu ya UB (Nayramadlin Orgil).

Kaskazini mwa nchi kuna ardhi yenye hali ya sakitu ya kudumu yaani yenye halijoto chini ya 0 C° ndani yake isiyopoa hata wakati wa majira ya joto. Kusini kuna jangwa kubwa la Gobi.

Asilimia 10 pekee za nchi ina misitu hasa mlimani na ardhi inayolimika ni 1 % tu.

Hali ya hewa

Hali ya hewa ni ya kibara na ina tofauti kubwa. Majira hubadilishana kuwa na joto pia baridi kali. Wastani wa siku ni kati ya −25 °C na +20 °C. Hali halisi wakati wa joto mchana kuna joto kali lakini usiku huwa baridi.

Usimbishaji una tofauti kubwa kati ya kaskazini na kusini mwa nchi. Kusini ni yabisi zaidi hadi kushuka kwa mm 100 za mvua pekee kwa mwaka katika jangwa la Gobi.

Miji

Miji mikubwa ni mji mkuu Ulaanbaatar (Улаанбаатар) (takriban wakazi milioni moja - zaidi ya theluthi ya watu wote wa taifa), halafu Erdenet (wakazi 79,649), Darchan (72,386) na Choibalsan (44,367).

Historia

Miaka 800 iliyopita nchi hii ilikuwa chanzo cha moja kati ya milki kubwa kabisa katika historia wakati ambako Chingis Khan alipounda Milki ya Wamongolia iliyoenea kuanzia China hadi Mashariki ya Kati na Ulaya.

Hadi mwaka 1992 nchi iliitwa Jamhuri ya Watu wa Mongolia na kufuata sera za ukomunisti.

Watu

Wakazi ni hasa Wakhalkhas (82%), Wakazaki (4%) na wengineo.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kimongolia.

Upande wa dini, Wabuddha ni 53%, Waislamu ni 3%, wafuasi wa dini za jadi ni 2.9%, Wakristo ni 2.2%, lakini 38.6% hawana dini yoyote.

Uchumi

Uchumi wa Mongolia hutegemea hasa migodi na ufugaji. Kihistoria Wamongolia walikuwa wafugaji waliohamahama na wanyama wao na kuishi katika hema. Tangu mapinduzi ya mwaka 1921 sekta ya migodi na viwanda ilijengwa.

Sekta ya kisasa ya biashara iko hasa kwenye mji mkuu.

Hadi leo karibu nusu ya wakazi huishi nje ya miji wakifuatana na wanyama wao ambao ni hasa kondoo, mbuzi, ng'ombe, farasi na ngamia.

Kilimo kipo mahali pachache kufuatana na tabia yabisi ya nchi. Wakati wa baridi sehemu kubwa ya wafugaji hukaa vijijini walipojenga nyumba.

Migodi ni hasa makaa mawe, shaba, bai na dhahabu.

Tazama pia

Viungo vya nje

Mongolia 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Serikali
    General information
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Mongolia  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mongolia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Mongolia JiografiaMongolia HistoriaMongolia WatuMongolia UchumiMongolia Tazama piaMongolia Viungo vya njeMongoliaAsiaBara

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UtafitiKumamoto, KumamotoZama za ChumaMuhammadMkoa wa MbeyaViwakilishi vya -a unganifuCAFDiwaniWimbiKombe la Mataifa ya AfrikaVivumishi vya kumilikiTupac ShakurKiwakilishi nafsiPichaNahauSimba S.C.UfupishoWayahudiMsituHerufiGoogle ChromeBarua pepeAla ya muzikiVita ya Maji MajiSinagogiLugha fasahaUgonjwa wa kuambukizaNgonjeraUsawa (hisabati)Mkoa wa IringaUtoaji mimbaNyotaHistoria ya AfrikaKanisa KatolikiZeruzeruMfumo wa mzunguko wa damuDar es SalaamUmoja wa MataifaMusaMoyoJoyce Lazaro NdalichakoVielezi vya wakatiUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaChelsea F.C.NyegereOrodha ya Marais wa KenyaUpendoMkoa wa TaboraMfumo wa upumuajiUmoja wa Muungano wa AfrikaBarabaraKipindupinduSamakiHadithi za Mtume MuhammadMkoa wa KataviSayariBahariMadhara ya kuvuta sigaraMkoa wa Dar es SalaamBendera ya TanzaniaOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaAmfibiaAkiliMkoa wa MaraKata za Mkoa wa Dar es SalaamUislamuWahayaRisalaWhatsAppMatumizi ya LughaSensaIsraeli ya KaleKiambishiAina za manenoKitomeo🡆 More