Brunei

Brunei (jina rasmi niː برني دار السلام , Negara Brunei Darussalaam, yaaniː Taifa la Brunei, Nyumba ya Amani) ni usultani mdogo na nchi huru kaskazini mwa kisiwa cha Borneo huko Asia ya Kusini-Mashariki.

Brunei

Imepakana na majimbo ya Sarawak na Sabah ya Malaysia tu, ingawa sehemu kubwa ya kisiwa hicho inatawaliwa na Indonesia.

Mji mkuu ni Bandar Seri Begawan.

Mtawala wa nchi ni sultani Hassan al-Bolkiah. Anasemekana kuwa kati ya watu tajiri zaidi duniani kutokana na mapato ya mafuta ya petroli.

Historia

Dola la Brunei lilistawi kuanzia mwaka 1368 hadi karne ya 17 likienea katika sehemu kubwa ya Borneo na hata visiwa vingine. Lilipokea Uislamu katika karne ya 15.

Baada ya kunyang'anywa maeneo mengi na Wazungu (Wahispania, Waholanzi na Waingereza), mwaka 1888 sultani aliomba ulinzi wa Uingereza ambao uliendelea hadi uhuru wa mwaka 1984.

Watu

Wakazi wengi (66%) ni wa jamii ya Wamalay, 10% ni Wachina, 3.4% ni Waborneo asili, 2.3% ni Wahindi, 16.8% wana asili tofauti.

Lugha rasmi ni Kimalay, lakini Kiingereza pia kinatambuliwa na katiba ya nchi.

Dini rasmi ni Uislamu wa madhehebu ya Sunni ambayo inafuatwa na thuluthi mbili za wakazi, lakini wakazi wengine wanafuata dini za Ubuddha (13%), Ukristo (10%) na dini za jadi (2%). Asilimia 7 hawana dini maalumu.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Brunei 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:


    Serikali
    Taarifa za jumla
    Biashara
    Utalii
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Brunei  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Brunei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Brunei HistoriaBrunei WatuBrunei Tazama piaBrunei MarejeoBrunei Viungo vya njeBruneiAsiaBorneoJina rasmiKaskaziniKisiwaKusiniMasharikiNchi huruUsultani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Vipimo asilia vya KiswahiliVieleziNg'ombeMusaHektariUshairiTendo la ndoaSalim Ahmed SalimLugha ya isharaTanganyikaJumuiya ya MadolaLenziSayariMmeaMwanaumeOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaMichezo ya watotoUtoaji mimbaInshaMaliasiliPesaKitenzi kikuuViwakilishi vya sifaMisriKupakua (tarakilishi)Virusi vya CoronaBiashara ya watumwaChristina ShushoUzazi wa mpangoOrodha ya kampuni za TanzaniaBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiNgonjeraDubai (mji)UtafitiTungo sentensiBagamoyo (mji)MaktabaKitunda (Ilala)AfrikaKishazi huruMJHistoria ya BurundiMwanamkeSintaksiEe Mungu Nguvu YetuMbooMartin LutherMvuaMaeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaMarie AntoinetteMohamed Gharib BilalDemokrasiaNandyAnwaniUaLugha ya maandishiWilaya ya KigamboniTamthiliaJumuiya ya Afrika MasharikiKamusi ya Kiswahili - KiingerezaMbadili jinsiaWajitaIndonesiaLigi ya Mabingwa AfrikaMlongeKihusishiMatiniOrodha ya Magavana wa TanganyikaMburahatiAfrika Mashariki 1800-1845Mkoa wa Ruvuma🡆 More