Dini (kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka: ad-din) inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji.
Ibada ni nguzo mojawapo iliyo dhahiri miongoni mwa dini kadhaa katika kuunganisha dhamira za mwenye kushika dini na mhimili wa imani, lakini dini inahusu pia mafundisho kuhusu maadili, mema na mabaya, imani na jinsi ya kushiriki katika jumuiya za waumini.
Kwa maana nyingine "dini" inataja jina kielelezo juu ya aina mbalimbali za imani jinsi inavyopatikana duniani, yaani jumuiya za kidini.
Dini kwa maana hiyo yenye wafuasi wengi duniani ni:
Pamoja na hizi kuna dini mbalimbali zinazojulikana tangu karne nyingi duniani hata kama idadi ya wafuasi si kubwa sana kwa mfano:
Pia kuna imani ambazo zinafanana kwa namna fulani, hivyo mara huhesabiwa kama imani mbalimbali za pekee, mara huhesabiwa kama kundi la dini zenye misingi ya pamoja au kama matawi ya imani moja. Zikitazamiwa pamoja idadi ya wafuasi ni kubwa kiasi lakini zikihesabiwa moja-moja idadi ya wafuasi si kubwa sana, kama vile:
Hasa Asia ya Mashariki zimetokea mafundisho ambayo mara huhesabiwa kati ya dini mara kati ya falsafa. Mifano yake ni:
Wafuasi wao mara nyingine hufuata pia kwa wakati mmoja dini zingine kama vile Ubuddha au Ukristo.
Historia inajua pia dini zilizotokea mara kwa mara katika nchi mbalimbali. Mfano wa dini iliyoanzishwa katika karne ya 19 na kusambaa kote duniani ni Baha'i. Kuna mifano mingi mingine. Si rahisi kuzitaja zote.
Zaidi ya hayo kuna miendo yenye tabia za kidini, ambayo hakuna makubaliano ya wataalamu kama ni dini au la, kwa mfano New Age na Yoga.
Dini kwa kipindi kirefu cha maisha ya mwanadamu imekuwa kitovu cha ustaarabu wa jamii husika. Hivyo kadiri jamii inavyobadilika ndivyo mambo mengi huongezwa ama kutolewa katika mapokeo yake ili hali kuakisi mazingira ya nyakati.
Katika wakati wa sasa, kumekuwepo kwa jitihada mbalimbali zinazopokea na kuchunguza misingi ya dini na maisha katika sura ya kisomi na hata kiudadisi.
Kuna masomo mbalimbali ambayo huangalia na kuchunguza dini kwa kutumia mbinu za kitaaluma. Kati ya hizo kuna:
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Dini, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.