Kimalay ni lugha ya Kiaustronesia nchini Malaysia, Brunei, Singapuri na Indonesia inayozungumzwa na Wamalay.
Ni lugha ya mawasiliano kwa wengi, hata nchini Ufilipino, Timor Mashariki na Uthai, tofauti na Kimalay Sanifu ambayo ni lugha rasmi nchini Malaysia.
Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kimalay kama lugha mama ilihesabiwa kuwa watu milioni 77, lakini wasemaji wote wanaweza kufikia milioni 200-290.
Kufuatana na uainishaji wa lugha wa ndani zaidi, Kimalay iko katika kundi la Kimalayiki.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kimalay kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kimalay, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.