Ushairi: Muundo

Ushairi ni utungo wa kisanaa ulio na madhumuni ya kutumbuiza au kuelimisha.

Tena, ushairi ni tawi mojawapo la fasihi andishi. Kinyume chake ni nathari.

Ushairi: Muundo
Kibao cha Gilgamesh.
Ushairi: Muundo
Shairi la Beowulf.

Inawezekana kutunga mashairi yenyewe au kutumia lugha ya kishairi katika aina nyingine za sanaa, kwa mfano tamthiliya au nyimbo.

Ushairi una historia ndefu. Kwa mfano, mwanafalsafa Aristotle katika kitabu chake Ushairi ("Poetics" kwa Kiingereza) anachunguza matumizi yake katika hotuba, tamthiliya, nyimbo na futuhi.

Ushairi una vipera vifuatavyo:

1. nyimbo

2. ngonjera

3. mashairi mepesi

4. maghani

5. tendi

6. rara

7. rara nafsi

Maana na tafsiri ya ushairi kulingana na washairi wakubwa

Katika kujenga hoja mbalimbali za ushairi ni nini. Wakongwe na magwiji wa ushairi wa awali walieleza maana mbalimbali za ushairi kulingana na utunzi. Wakongwe hao waliamini kuwa mtunzi ana uhuru wa kutunga aina za mashairi wazipendazo bora tu wapashe ujumbe kwa hadhira. Washairi hao walitunga mashairi bila kujali arudhi za ushairi.

Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya vina, una ufasaha wa maneno machache au muhtasari. Mwauliza wimbo, shairi na tenzi ni nini? Wimbo ni shairi ndogo, ushairi ni wimbo mkubwa na utenzi ni upeo wa ushairi. Mwauliza tena kina na ufasaha huweza kuwa nini? Kina ni mlingano wa sauti za herufi. Kwa maneno mengine huitwa mizani ya sauti na ufasaha ni uzuri wa lugha. Mawazo na maoni na fikra za ndani zinapoelezwa kwa muhtasari wa shairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu.

Ushairi ni lafudhi ya asili inayoeleweka zaidi na moyo wa kila mtu anayeishi katika jamii inayohusika.

“Ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale. Ndicho kitu kilicho bora sana katika maongozi ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalumu kwa shairi.

Utungo ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya chenziye; wenye vipande vilivyo na ulinganifu wa mizani zisizo pungufu wala zilizo zaidi; na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato maalum na yenye lugha nyofu, tamu na laini, lugha ambayo ni tetelezi kwa ulimi kwa kuitamka, lugha ambayo ina uzito wa fikra, tamu kwa mdomo wa kuisema, tumbuizi kwa masikio ya kuisikia na yenye kuathiri moyo uliokusudiwa na kama ulivyokusudiwa.

Abdilatif Abdallah

Uandishi wa mashairi ya Kiswahili ulianzia Lamu na Pate kabla ya kuenea katika Mkoa wa Tanga, Zanzibar, na maeneo mengine ya jirani. Utamaduni huo bado unatekelezwa hadi leo

Marejeo

Ushairi: Muundo  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ushairi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Fasihi andishiNathariSanaaTawi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

VokaliVitendawiliUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaJKT TanzaniaKiarabuMajiJumuiya ya Afrika MasharikiTasifidaMkoa wa SongweMgawanyo wa AfrikaIdi AminMpira wa miguuMbuniBenki ya DuniaMziziVivumishi vya pekeeMfumo wa upumuajiLigi ya Mabingwa UlayaSamia Suluhu HassanWizara za Serikali ya TanzaniaShikamooKichecheVieleziSarufiPasifikiHekimaBahashaJinaPichaVita ya Maji MajiNafsiRamaniTamathali za semiMadiniMauaji ya kimbari ya RwandaStafeliMaji kujaa na kupwaVoliboliItifakiMkoa wa KigomaHistoriaKigoma-Ujiji23 ApriliOrodha ya mito nchini TanzaniaBiashara ya watumwaHomoniTendo la ndoaKalenda ya KiislamuZuchuIlemelaUzazi wa mpango kwa njia asiliaKajala MasanjaDayolojiaUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius NyerereNdoa katika UislamuWimboLatitudoNdiziLahaja za KiswahiliDemokrasiaImaniViganoSexMange KimambiWagogoPumuNetiboliMbeya (mji)MrijaKilimanjaro (volkeno)Kidole cha kati cha kandoVivumishiVyombo vya habariSamliMtotoOrodha ya Marais wa MarekaniMadawa ya kulevya🡆 More