Ua

Maua ni majani ya pekee kwenye sehemu za uzazi wa mimea.

Maua
Maua mbalimbali
Maua mbalimbali
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: mmea
Ngeli: Maua

Mara nyingi kwa nje huwa na rangi za kuvutia na kwa sababu hii maua yanapendwa pia na wanadamu kama mapambo. Katika lugha ya kila siku neno "ua/maua" linataja pia mmea wote wenye maua.

Ua
Mchoro wa ABC unaoonyesha kukua kwa ua

Petali

Majani ya nje au petali yanayoonekana vizuri pamoja na rangi yake huitwa petali. Huwa na rangi mbalimbali ili kuvuta wadudu wanaochavusha ua na hivyo kuusaidia mmea kuzaa. Yanaviringisha na kukinga viungo vya uzazi ndani yake.

Ua 
Sehemu za ua
1 kombe, 2 Sepali, 3 Petali, 4 Stameni zenye chavulio na filamenti, 5 Pistili yenye stigma, staili na ovari

Viungo vya uzazi

Viungo hivi kimsingi ni vya aina mbili:

Ua 
Mchoro wa sehemu za ua

Stameni

Stameni huwa na pande mbili:

    • Filamenti ni kama shina ya stameni. Juu yake kuna
    • Chavulio chenye mbelewele ambazo ni seli za kuzaa za kiume.

Pistili

Pistili au sehemu ya kike huwa na sehemu tatu:

    • Stigma ni uso wa kunata juu wa pistili; kazi yake ni kushika mbelewele
    • Staili inashika stigma na kupitisha mbelewele ndani yake
    • Ovari ina chembekike ndani yake. Chembekike ni kama yai la mnyama; ikitunganishwa na mbelewele, mbegu hujitokeza.
Ua 
Aina mbalimbali za maua ya Israeli.

Pistili zimeundwa kwa kapeli moja au kadhaa ambazo ni aina za majani maalumu yanayobeba ovari.

Ovari na mbegu

Baada ya utungishaji ua hukauka na mbegu inakua ndani ya ovari. Kwa mimea kadhaa ovari inaendelea kuwa tunda linalotunza mbegu ndani yake; kusudi la tunda ni kuvuta wanyama wanaokula tunda na kusambaza mbegu kwa njia hii.

Jinsia

Mimea mingi huunganisha sehemu za kike na za kiume ndani ya ua moja; mfano ni ua la waridi. Kuna pia mimea yenye maua ambayo ni ama ya kike au ya kiume, kwa mfano maua ya mtango au mboga.

Viungo vya nje

Ua 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Ua  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Ua PetaliUa Viungo vya uzaziUa JinsiaUa Viungo vya njeUaJaniLughaMimeaNenoPamboRangiUzaziWanadamu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MaudhuiHuduma ya ujumbe mfupiUkwapi na utaoCleopa David MsuyaMaigizoBikiraMethaliUfahamuMagonjwa ya machoMajeshi ya Ulinzi ya KenyaMsokoto wa watoto wachangaMgonjwaDar es SalaamJinaMsumbijiMuundo wa inshaViwakilishi vya urejeshiPemba (kisiwa)UaItifakiKupatwa kwa JuaUandishi wa barua ya simuMalebaAntibiotikiMapenziUenezi wa KiswahiliTanganyikaHistoria ya TanzaniaJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaWahangazaMaktabaSalim KikekeBabeliVisakaleHadithi za Mtume MuhammadWhatsAppBarua pepeIsimuDodoma MakuluSimuMkoa wa ArushaNdege (mnyama)ViganoUgonjwa wa uti wa mgongoStadi za lughaPijiniNikki wa PiliSoga (hadithi)Mwenge wa UhuruMkoa wa KilimanjaroShairiCristiano RonaldoTendo la ndoaVitenzi vishirikishi vikamilifuMafua ya kawaidaIdhaa ya Kiswahili ya Radio TehranTashbihaNyanda za Juu za Kusini TanzaniaSentensiVielezi vya idadiChristina ShushoNomino za kawaidaFasihiDhima ya fasihi katika maishaMgawanyo wa AfrikaKiambishiUkimwiBongo FlavaNg'ombeKalenda ya Kiislamu🡆 More