Biashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki

Biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki ni jina la kutaja aina ya biashara iliyokuwa ikifanyika kutoka katika pwani hadi ndanindani ya Afrika Mashariki.

Awali ilianza katika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki na kisha kuenea katika vijieneo vya ndani kabisa vya Afrika Mashariki.

Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Historia

Kipindi

Biashara hii inasemekana ilianzia karne ya 18 na 19, ikachukua zaidi ya miaka 30-50 hadi ilipokuja kuingiliwa na wakoloni mwishoni kabisa mwa karne ya 19.

Washiriki

Wafanyabiashara wakuu waliohusishwa na biashara hiyo walikuwa Waarabu na Waswahili kutoka Pwani na Wayao kutoka kusini mwa Tanganyika, Wakamba kutoka kusini mwa Kenya na vilevile Wanyamwezi kutoka Tabora. Makabila mengi yalishiriki katika biashara hiyo, lakini vingunge wenyewe ni Wayao, Wakamba na Wanyamwezi.

Muundo wa biashara

Biashara ilikuwa katika muundo wa misafara mitatu ambayo ilianzia pwani ikaenda hadi ndanindani kabisa mwa ukanda wa Afrika Mashariki. Misafara hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:

Msafara wa Kaskazini

Safari ilianzia Mombasa na baadhi ya maeneo ya Pangani hadi maeneo ya Kilimanjaro kuelekea pembezoni mwa ziwa Victoria, kupitia Wakikuyu, Wataita, Wamaasai, na Wanyika. Msafara huo ulikuwa unaongozwa na Wakamba kutoka Kenya.

Msafara wa Kati

Msafara huu ulianzia Bagamoyo kupitia maeneo ya kati ya Tanganyika - Tabora (Unyanyembe). Kuanzia huko msafara ulienda hadi Ujiji, halafu Buganda kupitia Buhaya, magharibi mwa fukwe ya Ziwa Victoria. Msafara ulikuwa chini ya Wanyamwezi ambao katika karne ya 19 walikuwa chini ya Mtemi Mirambo na Mtemi Nyungu ya Mawe na Mtemi Fundikira mnamo 1839. Msafara huu ulikuwa una shughuli nyingi na muhimu sana kupita misafara yote mitatu.

Msafara kusini

Msafara huu ulianzia katika bandari ya Mikindani na Kilwa kuelekea kanda ya Ziwa Tanganyika kupitia kusini mwa Ziwa Nyasa. Msafara ulifika Monomutapa kwa ajili ya dhahabu. Ulikuwa chini ya Wayao ambao walikuwa chini ya Mataka I kwenye karne ya 19. Wayao walifanya biashara kaskazini mwa Kilwa na Zambezi ya chini kuelekea Kusini. Baadaye walipata silaha wakawa viongozi mara moja katika maeneo ya Ziwa Nyasa na pwani. Wayao walishikiri msafara wa Kusini ambao uliishia Afrika ya Kati wakati Wakamba walikuwa Kaskazini na Wanyamwezi walishikiria msafara wa Kati ulioanzia Bagamoyo hadi Ujiji.

Bidhaa zilizokuwa zinapatikana katika biashara

Wafanyabiashara wa Waswahili na Waarabu kutoka pwani waliuza bunduki, shanga, unga wa bunduki, nguo na bidhaa nyingine za kiwandani. Watu kutoka ndanindani kabisa mwa Afrika Mashariki walitoa bidhaa kama vile pembe za ndovu, nta ya nyuki, dhahabu, ngozi za wanyama na vitu vingine vya thamani.

Sababu za kuibuka kwa Biashara ya Masafa Marefu ya Afrika Mashariki

Kuibuka na kuendelea kwa biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki kulichangiwa na mambo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na:

(A) Upatikanaji wa bidhaa za kutosha katika Afrika Mashariki

Hili lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji hasa katika sekta ya kilimo.

(B) Kuibuka kwa wafanyabiashara wakubwa

Kuibuka kwa jamii kubwa ya wafanyabiashara katika Afrika Mashariki kama vile Wanyamwezi, Wayao na Wakamba nako kulichangia kukua kwa biashara.

(C) Uwepo wa miji mikubwa ya pwani

Uwepo wa miji mikubwa ya pwani kama vile Bagamoyo, Mikindani na Pangani kuliongezea ukuaji wa biashara kwa kufuatia wa kwamba miji hiyo ilikuwa kianzio cha safari za masafa marefu wakati wa uendeshaji wa biashara.

Matokeo/madhara ya biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki

Biashara ya masafa marefu ilikuwa na matokeo kadha wa kadha katika maeneo ya pwani hadi ndanindani kabisa mwa Afrika Mashariki. Matokeo hayo ni pamoja na:

(A) Ukuaji wa miji

Biashara ilipelekea kukua kwa miji na vijiji hasa ndanindani huko mwa Afrika Mashariki kwa mfano Ujiji, Mpwapwa, Tabora na kwingineko.

(B) Ukuaji wa dola za kitemi

Biashara hii ilichangia kiasi kikubwa kukua kwa dola mbalimbali za kitemi kama vile Wanyamwezi, Ukimbu, na Wahehe katika maeneo ya Tanganyika. Vilevile dola la Buganda lilikuja kukua mno katika karne ya 19 kwa kufuatia biashara hii.

(C) Utambulisho wa tamaduni mpya

Tamaduni mpya, kwa mfano dini ya Kiislamu na mtindo wa uvaaji wa kanzu na baraghashia ulienea ndani kabisa ya Afrika Mashariki.

(D) Maendeleo/ukuaji wa lugha ya Kiswahili

Lugha ya Kiswahili ilienea kwa kiasi kikubwa sana kutoka katika pwani ya Afrika Mashariki hadi maeneo ya ndani kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wanatumia Kiswahili kama chombo cha mawasiliano wakati wa kubadilishana bidhaa.

(E) Ukuaji wa biashara ya utumwa

Biashara ya masafa marefu ilienda sambamba na ukuaji wa biashara ya utumwa - hasa katika maeneo ya ndani ya Afrika Mashariki.

(F) Kuibuka kwa wafanyabiashara na viongozi wakubwa

Kuna baadhi ya watu walioibuka kama wafanyabiashara na viongozi wakubwa nje ya biashara kwa kufuatia utajiri uliokithiri kutoka katika biashara. Hili lilijumlisha Mirambo, Machemba, [Nyungu ya Mawe]] na Mkwawa.

(G) Ndoa za mseto

Watu kutoka maeneo ya pwani walioana au kuzaliana na watu kutoka ndani kabisa mwa Afrika Mashariki.

Tazama pia

Viungo vya nje

Tags:

Biashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki HistoriaBiashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki Muundo wa biasharaBiashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki Bidhaa zilizokuwa zinapatikana katika biasharaBiashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki Sababu za kuibuka kwa Biashara ya Masafa Marefu ya Afrika MasharikiBiashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki Matokeomadhara ya biashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiBiashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki Tazama piaBiashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika Mashariki Viungo vya njeBiashara Ya Masafa Marefu Ya Afrika MasharikiAfrika MasharikiBiasharaPwani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KiraiNafsiOrodha ya kampuni za TanzaniaUzazi wa mpangoNyukiHurafaUturukiHeshimaWayahudiAlomofuBikira MariaMkoa wa IringaJumuiya ya Afrika MasharikiOrodha ya Marais wa KenyaMbooDuniaFutiTupac ShakurMkoa wa ShinyangaNandyBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiNazi (tunda)Mwanza (mji)Hadithi za Mtume MuhammadTundu Antiphas Mughwai LissuAzimio la ArushaWilaya za Tanzania 4Wimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiAdhuhuriUsawa (hisabati)Mkoa wa Unguja Mjini MagharibiXabi AlonsoVipaji vya Roho MtakatifuUundaji wa manenoNelson MandelaMendeAsiaItifakiLugha fasahaTeknolojiaAthari za muda mrefu za pombeOrodha ya makabila ya KenyaRayvannyAdolf HitlerBonde la UfaVichekeshoLafudhiDodoma (mji)SayariUaWahayaNdiziTiktokUongoziHistoria ya IranBungeTreniKylian MbappéMohamed Omary MchengerwaTabianchi ya TanzaniaMagonjwa ya machoAfrika ya MasharikiMtotoSoko la watumwaMafua ya kawaidaUtamaduniMkoa wa KigomaSheriaRaiaRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMkoa wa MaraRwandaRidhiwani Jakaya KikweteUfahamuPasaka ya KikristoNgw'anamalundiMaji🡆 More