Tajikistan ni nchi ndogo ya Asia ya Kati ambayo haina pwani kwenye bahari yoyote.
Tajikistan |
---|
Imepakana na Uchina, Afghanistan, Uzbekistan na Kyrgyzstan.
Eneo lake ni km² 143,100.
Sehemu kubwa ya nchi ni milima ya Pamir yenye kimo kati ya mita 3600 na 4400.
Kihistoria maeneo ya Tajikistan yalitawaliwa na madola mbalimbali, hasa na Uajemi.
Uislamu ulifika huko mnamo mwaka 800 BK.
Mwaka 1868 Tajikistan ilivamiwa na Urusi na kuwa sehemu ya Dola la Urusi, halafu sehemu ya Umoja wa Kisovyet baada ya mapinduzi ya 1917. Tangu mwaka 1929 iliitwa Jamhuri ya Kisovyet ya Kisoshalisti ya Tajikistan.
Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisoviet, Tajikistan ilipata uhuru wake mwaka 1991.
Kati ya mwaka 1992 hadi 1997 kulikuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilisababisha Warusi wengi kuondoka na ilikwisha kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Baada ya mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 Septemba 2001 jeshi la Marekani lilipata nafasi ya kutumia vituo vya kijeshi kwa ajili ya vita katika Afghanistan.
Wakazi wengi ni Watajiki na kuongea Kitajiki (84.2%), lugha ambayo inahusiana na Kiajemi. Ndiyo lugha rasmi na ya kawaida. Kabila linalofuata kwa ukubwa ni Wauzbeki (13.9%). Angalia pia orodha ya lugha za Tajikistan.
Wananchi wengi ni Waislamu (96.7%), hasa Wasuni, na ndiyo dini rasmi tangu mwaka 2009; Washia ni 3%. Wakristo ni 1.6%, hasa Waorthodoksi na Waprotestanti.
Angalia mengine kuhusu Tajikistan kwenye miradi mingine ya Wiki: | |
Fafanuzi za Kiingereza kutoka Wiktionary | |
picha na media kutoka Commons | |
misaada ya kujisomea kwa Kiingereza kutoka Wikiversity | |
nukuu kutoka Wikiquote | |
matini za ushuhuda na vyanzo kutoka Wikisource | |
vitabu kutoka Wikibooks |
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tajikistan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Tajikistan, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.