Milango Ya Fahamu

Milango ya fahamu ni ogani za mwili zinazoturuhusu kujua mazingira yetu.

Mifano yake ni macho na masikio. Ni njia asili ya kutambua mtazamo au hisia.

Milango Ya Fahamu
Macho, pua na nywele ndefu za "ndevu" ni milango muhimu kwa huyu paka.

Kibiolojia inaelezwa kuwa ogani yenye uwezo wa kupokea habari za nje ya mwili, kama vile nuru, sauti, halijoto, mwendo, harufu au ladha, na kuzibadilisha katika mishtuko ya umeme inayofikishwa kwa njia ya mfumo wa neva hadi ubongo.

Kama milango ya fahamu imeharibika, tunasema mtu ni kipofu, bubu au kiziwi, ana matatizo kuelewa mazingira yake sawa na jinsi wanavyoweza watu wengine.

Milango ya fahamu ni muhimu sana kwa Viumbe hai kutokana na kwamba inasadia kiumbe hai katika shughuli zake za kila siku, hasa katika kufatuta mahitaji muhimu (kwa Kiingereza yanaitwa Basic needs).

Fahamu zetu

Milango Ya Fahamu 
"Fahamu tano za binadamu" kadiri ya mchoraji Mwaustria Hans Makart (1840-1884).

Mara nyingi watu hutaja fahamu tano( ) ambazo ni:

  1. Kusikia ni fahamu ya sauti kupitia masikio
  2. Kuona ni fahamu ya nuru kupitia macho
  3. Kuonja ni fahamu ya ladha kupitia ulimi
  4. Kunusa ni fahamu ya harufu kupitia pua
  5. Mguso ni fahamu ya nyuso za vitu kupitia ngozi, hasa ya mkono

Hali halisi kuna fahamu zaidi:

  1. Fahamu ya joto - baridi
  2. Fahamu ya maumivu
  3. Fahamu ya uwiano (inayotuwezesha kusimama, kutofautisha juu na chini)
  4. Fahamu ya mwili wetu (inayotuwezesha kugusa pua wakati macho yamefungwa)

Mfumo wa kibiolojia ya fahamu zetu

Ogani mbalimbali za mwili ziko tayari kupokea vichocheo kutoka mazingira yetu.

Neva katika ogani husika zina uwezo wa kupokea vichocheo vya nje vinavyotafsiriwa katika ubongo kwa fahamu mbalimbali

  1. vichocheo vya kikemia vinavyotuwezesha kuonja na kunusa
  2. vichocheo vya nuru vinavyotuwezesha kuona
  3. vichocheo vya halijoto vinavyotuwezesha kutofautisha joto na baridi
  4. vichocheo vya shinikizo na mwendo
  5. vichocheo vya athari hatari vinavyotafsiriwa na ubongo kwa maumivu au kichefuchefu

Wanyama pia wana ogani zinazowawezesha kutambua:

  1. vichocheo vya kusumaku (kwa mfano ndege wanaohamahama mbali kila mwaka kwa kufuata uga wa sumaku wa dunia)
  2. vichocheo vya umeme
  3. vichocheo vya mnururisho sumakuumeme nje ya nuru ya kawaida, kwa mfano nyuki hutambua mawimbi ya urujuanimno yasiyoonekana na binadamu

Picha za milango ya fahamu

Marejeo

Milango Ya Fahamu  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Milango ya fahamu kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Milango Ya Fahamu Fahamu zetuMilango Ya Fahamu Mfumo wa kibiolojia ya fahamu zetuMilango Ya Fahamu Picha za milango ya fahamuMilango Ya Fahamu MarejeoMilango Ya FahamuHisiaMachoMasikioMazingiraMwiliOgani

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Shomari KapombeMkataba wa Helgoland-ZanzibarOrodha ya vyama vya kisiasa nchini KenyaKupatwa kwa MweziMuundo wa inshaMaji kujaa na kupwaMbeguLongitudoMauaji ya kimbari ya RwandaOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaRiwayaMkanda wa jeshiTungo kiraiKutoka (Biblia)SayansiVitenzi vishiriki vipungufuKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaMbiu ya PasakaKisononoUnju bin UnuqBasilika la Mt. PauloAli Hassan MwinyiUNICEFBustani ya EdeniThe MizHadithi za Mtume MuhammadTashihisiNamba ya mnyamaMbaraka MwinsheheJomo KenyattaDhahabuChombo cha usafiriKahawiaWahaTungo sentensiSanaaKamusi elezoKondomu ya kikeOrodha ya milima ya TanzaniaVivumishi vya pekeeHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMafarisayoAngkor WatTaswira katika fasihiTamthiliaFonolojiaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniUenezi wa KiswahiliUrusiFasihi ya KiswahiliHaitiKifua kikuuKunguniJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaVita Kuu ya Kwanza ya DuniaOrodha ya nchi kufuatana na wakaziUkristo barani AfrikaMajina ya Yesu katika Agano JipyaOrodha ya shule nchini TanzaniaKalenda ya mweziUajemiMisimu (lugha)NimoniaKiambishiMofimuNgamiaUkomboziStadi za lughaZabibuUtamaduniAbedi Amani KarumeBunge la Afrika MasharikiMapafuUshoga🡆 More