Hadithi au Sunnah ni maneno na vitendo ambavyo Mtume Muhammad alikuwa akisema au akifanya katika kipindi chake cha utume.
Hadithi hizi ni mmoja kati ya miongozo ya imani kwa Waislamu.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Uislamu na dini nyingine |
Hadithi hizi zinajumuisha pia mambo aliyoyaona au kuyasikia katika muda wa utume wake akalinyamazia kimya au akawa hakulipinga na akalikubali.
Muhammad aliishi miaka kama arobaini bila kuwa na imani ya Mungu pekee.
Kisha Mwenyezi Mungu akamletea mjumbe kutoka kwake aitwaye malaika Jibrili anayeaminiwa na Waislamu kuwa ndiye aliyempa aya zilizoko katika msahafu wa Waislamu, Kurani.
Inaelezwa kuwa Jibrili alimpa Muhammad aya hizo kwa muda wa miaka ishirini na mitatu mpaka alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.
Hadithi za Mtume Muhammad zimekusanywa katika vitabu vingi sana na wanazuoni mbalimbali wa Hadithi, lakini vitabu vya hadithi ambavyo ni muhimu na vinategemewa na wengi katika Uislamu ni hivi vifuatavyo:
Mtume Muhammad alikuwa hapendelei Hadithi zake ziandikwe wakati mmoja na Kurani, yasije yakachanganyika maneno yake na yale ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Hadithi zilichelewa kuandikwa mpaka baada ya kufariki kwake dunia kwa muda mkubwa kidogo, na kwa sababu hiyo Hadithi zikatawanyika sehemu mbalimbali kulingana na usahihi wake au udhaifu wake au uwongo wake.
Hivyo kuna Hadithi aina nne kulingana na fahamu na kutegemewa kwa msimulizi wa hiyo Hadithi: Hadithi Sahihi, Hadithi Hasan (Nzuri), Hadithi Dhaifu na Hadithi Maudhu'u (Hadithi ya Uwongo).
Vile vile, kuna aina nyingine za Hadithi zilizogawanyika kwa mujibu wa mambo mengine kama vile: kwa mujibu wa wapokezi, au mfululizo wa wasimulizi, au idadi ya wasimulizi katika kila sehemu ya mfululizo, au kwa mujibu wa simulizi lenyewe na msimulizi wake.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Hadithi za Mtume Muhammad, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.