Manabii wa Uislamu ni binadamu wanaume ambao huhesabiwa na Waislamu kuwa manabii waliochaguliwa na Mungu.
Kwa imani ya Kiislamu manabii hao wote walihubiri ujumbe uleule wa kumwabudu Allah.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Uislamu na dini nyingine |
Kuna majina ya watu 25 kwenye Qur'an wanaotajwa kuwa manabii. Wengi kati yao hutajwa pia katika Biblia na majina yao jinsi yalivyo kawaida katika Uyahudi na Ukristo yanatajwa katika mabano.
Sehemu za habari za manabii wa Qurani na watu wa Biblia hulingana, lakini mara nyingi ziko tofauti pia. Kwa mfano Ibrahim wa Qurani aliambiwa na Mungu kumtoa mwanawe kama sadaka lakini jina lake halitajwi, kumbe katika Biblia habari hii inasimuliwa juu ya Isaka. Dawud hutajwa na Qurani kama nabii, wakati Daudi wa Biblia ni mfalme mwenye manabii wake (hasa Gad na Nathan), ingawa anaweza kuhesabiwa kama nabii kwa sababu ya kuchangia kitabu cha Zaburi (ambacho kina utabiri mbalimbali kuhusu Yesu.
Manabii hao wa Qurani ni pamoja na
(jina la Qurani, kwa maandishi ya Kiarabu,, sura ya Qurani anapotajwa, jina la Kibiblia linaloweza kumaanishwa)
Kufuatana na mafundisho ya Uislamu katika dini zote za mbinguni ambazo Mwenyezi Mungu amewaletea wanadamu kwa njia ya Mitume na Manabii, kama dini ya Kiyahudi, dini ya Kinasara (Ukristo) na dini ya Kiislamu, hao Mitume na Manabii wametajwa katika vitabu walivyokuja navyo, na hii ni ishara moja kubwa kuwa dini hizo zina asili moja na Mwenyezi Mungu mmoja.
Katika kitabu cha Wayahudi cha Talmud, Mitume wao wametajwa kama ifuatayo:
Abrahamu, Isaka, Yakobo, Mose, Haruni, Yoshua, Samueli, Solomoni, Obadia, Jehu bin Hanani, Azaria bin Odedi, Jahazieli Mlawi, Eliezeri bin Dodavahu, Hosea, Amos, Mika, Amoz (baba wa nabii Isaya), Eliya, Elisha, Yona, Isaya, Yoeli, Nahumu, Habakuki, Sefania, Uria, Yeremia, Ezekieli, Shemaia, Baruku, Neria (baba wa Baruku, Meseia (baba wa Neria), Hagai, Zekaria, Malaki yaani Ezra, Hasofer, Mordekai Bilshan, Oded (baba wa Azaria), na Hanani (baba wa Jehu)
Mitume wengine walitajwa katika Agano la Kale, kati yao ni: Adamu, Noah (Nuh), Yuda (Yahuda), Daudi.
Wengine tena wanatajwa katika Agano Jipya, hasa Yohane Mbatizaji (Yahya) na Yesu bin Mariamu ('Îsa).
Mwenyezi Mungu ametaja Mitume na Manabii 25 katika Qurani, na katika Hadithi za Mtume Muhammad imetajwa kuwa idadi yao kwa jumla ni 124,000, katika hao 315 ni Mitume na waliobaki ni Manabii.
Kati ya hao waliotajwa ndani ya Qurani ni:
Adam, Idris, Nuh, Hud, Salih, Lut, Ibrahim, Ismail, Is-haq, Yaqub, Yusuf, Shu'aib, Ayyub, Dhulkifl, Musa, Harun, Daud, Sulaiman, Ilyas, Ilyas'a, Yunus, Zakaria, Yahya, Isa, na Muhammad.
Miongoni mwao, watano ni Mitume wakubwa ambao walipewa mitihani mingi wakawa na subira kustahimili matatizo ya umma zao. Hawa ni Nuhu, Ibrahimu, Musa, Isa na Muhammad.
Mitume ni wale ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa kauma na umma mbalimbali ili kuwaelekeza njia yake na kuwaepusha na njia za upotofu za Ibilisi na Shetani.
Kumbe Manabii ni wale walioletewa ufunuo na wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili wawafahamishe watu wao kuhusu ujumbe wake.
Lakini si wote wanakubali kuwatofautisha hivyo.
Kadiri ya Uislamu Mitume na Manabii wote, tangu alipoletwa Adam mpaka Mtume wa mwisho kuletwa duniani, wote wamekuja na ujumbe mmoja wa kuwa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote na viumbe vyote ni Mmoja na hana mshirika, na kuwa yeyote atakayemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, basi huyo huwa amepotea na ametoka njia iliyonyoka, na malipo yake ni kutiwa motoni milele.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mitume na Manabii katika Uislamu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.