Maajabu Ya Dunia

Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa Kale.

Wagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).

Maajabu Ya Dunia
Maajabu saba ya dunia ya kale
Orodha ya makala yafuatana na picha hizi saba

Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon

Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika ustaarabu huo. Kwa hiyo hakuna mifano kutoka Uhindi, China, Asia ya Mashariki, Amerika, Afrika kusini ya Sahara wala Ulaya ya Kaskazini.

Majengo ya orodha ya Antipater hayakudumu hadi leo, isipokuwa Piramidi za Giza. Mengine yaliharibika kutokana na matetemeko ya ardhi au kubomolewa, tena hadi leo hapajulikani mahali pa "Mabustani ya Semiramis". Sanamu na picha za kuchongwa kutoka Kaburi la Mausolo na Hekalu la Artemis zilikusanwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Britania mjini London, Uingereza.

Maajabu saba ya Kale

  1. Piramidi za Giza (Misri ya Kale)
  2. Mabustani ya Semiramis (Babeli, leo Irak)
  3. Hekalu ya Artemis mjini Efeso ((Ugiriki ya Kale, leo Uturuki, Asia Ndogo)
  4. Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)
  5. Kaburi la Mausolo mjini Halikarnassos (Ugiriki ya Kale, leo Uturuki)
  6. Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)
  7. Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)

Kati yake piramidi pekee zimebaki hadi leo.

Maajabu ya dunia ya sasa

Katika ulimwengu kila siku maajabu yanaongezeka na kufanya maajabu mapya ya dunia kukubalika mara kwa mara. Kwa mfano, mwaka 2016 kuna maajabu yake. Orodha ya maajabu hayo hutolewa na watu mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti: wengine wanaishia upande wa majengo, wengine wanahesabu hata mazuri ya uasilia n.k.

Vitu hivi hadi kufikia kuitwa maajabu ya dunia ina maana ni vya pekee duniani kote, na hakuna kitu kingine kama hicho au cha kufanana nacho.

Tanzania kuna kitu kimoja ambacho kinasemekana ni kati ya maajabu ya dunia ambacho ni kasoko ya Ngorongoro, iliyoko mkoa wa Manyara.

Picha za "Maajabu ya Kisasa"

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • D'Epiro, Peter, and Mary Desmond Pinkowish, "What Are the Seven Wonders of the World? and 100 Other Great Cultural Lists". Anchor. 1 December 1998. ISBN 0-385-49062-3
  • "The Seven Wonders of the World, a History of Modern Imagination" written by John & Elizabeth Romer in 1995
  • "The Seven Wonders of the Ancient World" edited by Peter Clayton and Martin Price in 1988
  • Johann Conrad Orelli (ed.) Philonis Byzantini Libellus de septem orbis spectaculis. 1816. The original travel guide by Pseudo-Philo
  • Lendering, Jona (2007–2010). "Seven Wonders of the Ancient World". Livius.Org. Iliwekwa mnamo 28 July 2012.  Check date values in: |accessdate= (help)

Viungo vya nje

Maajabu Ya Dunia 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Maajabu Ya Dunia  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maajabu ya dunia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Maajabu Ya Dunia Maajabu saba ya KaleMaajabu Ya Dunia Maajabu ya dunia ya sasaMaajabu Ya Dunia Picha za Maajabu ya KisasaMaajabu Ya Dunia Tazama piaMaajabu Ya Dunia TanbihiMaajabu Ya Dunia MarejeoMaajabu Ya Dunia Viungo vya njeMaajabu Ya DuniaJengoWagirikiWagiriki wa Kale

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

TarafaIntanetiOrodha ya nchi kufuatana na wakaziHaki za binadamuSakramentiLahaja za KiswahiliIsraeli ya KaleYerusalemuUaMichael JacksonTAZARAHekaya za AbunuwasiMfumo wa vyama vingiBaraza la mawaziri Tanganyika 1961RisalaKichecheViwakilishi vya idadiUtamaduni wa KitanzaniaHarusiBundiDhanaJokate MwegeloMkoa wa ArushaKombe la Dunia la FIFAJuxKiswahiliMahindiWazigulaWahaAslay Isihaka NassoroLugha ya kwanzaTamathali za semiKaaSteve MweusiWilaya za TanzaniaVidonda vya tumboVivumishi vya -a unganifuUkoloniMwanamkeNomino za kawaidaRayvannyNyangumiMofolojiaOlduvai GorgeAdhuhuriOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoWapareTungo sentensiSilabiAlama ya barabaraniTiktokOrodha ya viongoziMaskiniBenjamin MkapaMajigamboTungo kiraiHisiaMbuMichoro ya KondoaKilimoInsha ya wasifuAlmasiVidonge vya majiraMkoa wa RuvumaYoung Killer MsodokiOrodha ya Marais wa TanzaniaMkoa wa SongweAgano la KaleKifua kikuuIniTashihisiTabianchi ya TanzaniaViwakilishi vya sifa🡆 More