Riwaya (kutoka neno la Kiarabu رواية riwaya ) ni kazi andishi ya fasihi ambayo kwa kawaida ni ndefu kuliko hadithi fupi.
Urefu wa riwaya, maana yake ni kwamba msuko simulizi umejengeka vizuri, kuna wahusika wengi, unaenea muda mrefu, na mada zake ni nzito na pana kiasi.
Mifano mizuri ya riwaya kwa lugha ya Kiswahili ni Nagona au Mzingile, zilizoandikwa na mwandishi Euphrase Kezilahabi.
Kamusi ya Fasihi iliyotolewa na K. W. Wamitila inataja aina nyingi tofauti za riwaya, k.m. riwaya sahili, riwaya changamano, riwaya kiambo, riwaya ya kibarua na nyingine nyingi.
Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Riwaya kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Riwaya, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.