Mnururisho (ing.
Mnururisho huwa na chanzo, mwelekeo usionyoka na kasi.
Mifano ya mnururisho inayoonekana au kusikika kirahisi ni nuru na joto. Binadamu ana milango ya fahamu kwa ajili mnurirsho huo kama vile macho kwa nuru na neva kenye ngozi kwa joto. Mifano ya mnururisho isiyoonekana ni mnururisho wa sumakuumeme katika redio na TV, eksirei au kinyuklia. Kuna viumbe vyenye milango ya fahamu kwa minururisho mingine, kwa mfano samaki au ndege zinazotambua uga za umeme au sumaku. Nyuki huona infraredi isiyoonekana kwa macho ya kibinadamu.
Mnururisho uko kati ya sehemu za fizikia zilizochunguliwa zaidi na sayansi na kupata matumizi mengi katika teknolojia ya kibinadamu.
Hata hivyo wataalamu hawana uhakika mnururisho mwenyewe ni nini hali halisi. Kadiri na mbinu za upimaji huonekana mara kama mwendo wa chembe yaani vipande vidogo sana vya mada (kama vile elektroni au nyutroni) na mara kama wimbi yaani mwendo wa nishati isiyo na umbo wa kimada.
Mnururisho unaweza kuathiri vitu vinavyoguswa nao. kama nishati yake ni kubwa ya kutosha inaweza kusababisha halijoto kupanda, mabadiliko ya kikemia au pia madhara kwa vitu na viumbe hai.
Kuna aina nyingi za mnururisho au njia za uenezaji wa nishati.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mnururisho, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.