Mapenzi Ya Jinsia Moja

Mapenzi wa jinsia moja (kwa Kiingereza: homosexuality) ni mwelekeo wa kimapenzi kati ya watu wa jinsia ileile.

Mwelekeo ukifuatwa unageuka tabia.

Mapenzi Ya Jinsia Moja
Bendera ya fahari, bendera inayowakilisha watu wa LGBT, wakiwemo wapenzi wa jinsia moja.
Mapenzi Ya Jinsia Moja
Utafiti wa mwaka 2019 (Pew Global Research Poll): Asilimia ya wakazi wanaokubali mapenzi wa jinsia moja yawe halali katika jamii:      0-10%      11-20%      21-30%      31-40%      41-50%      51-60%      61-70%      71-80%      81-90%      91-100%      Hakuna taarifa

Mwelekeo wa kimapenzi humaanisha mihemko ya kimahaba au mivuto ya kimapenzi kwa jinsia fulani. Mwelekeo huo kwa kawaida humfanya mtu kupenda jinsia tofauti na ya kwake (kuwa na mvuto kwa watu wa jinsia nyingine), jambo ambalo linawezesha uzazi kadiri ya maumbile.

Hata hivyo kuna wanawake wanaovutiwa na wanawake wenzao na wanamume wanaovutiwa na wanaume wenzao, mbali ya watu wanaovutiwa na jinsia zote mbili (kwa Kiingereza: “bisexual”), mbali na wale wasio na mwelekeo wowote wala kusikia mvuto wowote wa namna hiyo (kwa Kiingereza: “asexuals”).

Watu wana mang'amuzi tofauti juu ya mwelekeo wao wa kimapenzi. Baadhi wanajitambua kwa muda mrefu kabla hawajaanza uhusiano na wengine. Baadhi hujihusisha na vitendo vya kimapenzi kabla ya kujitambua na kuchukua msimamo juu ya mwelekeo wao. Vivutio vya msingi ambavyo huunda mwelekeo wa kimapenzi wa watu wazima kwa kawaida huibuka katika ubalehe. Wakati huo wengine wanayumba kwa muda fulani katika kujitambua, lakini baadaye wengi wao wanakomaa katika mwelekeo wa kawaida . Wapo wanaotaka hao watoto wapewe mapema dawa za kuzuia ubalehe ili baadaye iwe rahisi kuwafanyia upasuaji wa kubadili vyungo vya uzazi kadiri ya mwelekeo wao kama kwamba mwili ulivyo hauna maana. Serikali za nchi mbalimbali, kama Uswidi, Ujerumani na Uingereza, zimeshatakaza tiba za namna hiyo kwa kuona madhara yake kubwa.

Binadamu, akiwa na akili na utashi, halazimiki wala hapaswi kufuata mielekeo yake yote, bali anatakiwa kuidhibiti, la sivyo ataharibika upande wa afya ya mwili na ya nafsi vilevile, mbali ya kuharibu maisha ya jamii. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na mwelekeo wa kuwazini watoto wadogo, mwingine wa kula kupita kiasi, n.k. Wakifuata mielekeo hiyo ataleta madhara tu. Maadili yanafundisha kufikiri kabla ya kufuata mwelekeo wowote.

Istilahi

Aina kuu za wapenzi wa jinsia moja ni wasagaji, mashoga, wasenge na mabasha. Maneno hayo yanaweza kutumika kwa dhihaka au kwa lengo la kudhalilisha watu wa namna hiyo. Matumizi hayo yanaweza kuathiri vibaya hisia na heshima ya watu hao.

Wasagaji ni wanawake wanaojamiiana na wanawake wengine. Neno hilo linatokana na kitenzi "kusaga".

"Wasenge" na "mashoga" ni takribani visawe: yote mawili huhusu mwanamume anayeingiliwa katika ngono ya jinsia moja na mara nyingi huhusishwa kwa upungufu wa uume, au mwanamume ambaye angetaka awe mwanamke. Kwa upande mwingine, basha ni mwanamume anayemwingilia shoga.

Mara nyingi, mashoga huitana "kaka poa", na hivyohivyo wasagaji huitana "dada poa". Kwa Kiingereza, shoga anaitwa gay. Hapo awali, gay ilimaanisha "furaha", lakini imekuwa na maana ya mwanamume anayeelekea watu wa jinsia yake, huku wanawake wa namna hiyo wakitajwa kuwa lesbians.

Historia

Tafiti tofauti kote ulimwenguni zimegundua kuwa mtu 1 hadi 10 kati ya 100 wanavutiwa na watu wa jinsia yao wenyewe.

Ushoga umekuwepo katika jamii na tamaduni nyingi, na pia unasemekana kutokea katika spishi 500 hivi za wanyama.

Moja ya dhihirisho la mapema zaidi ulimwenguni la ushoga kati ya watu ni michoro ya miambani ya Wasan wa Zimbabwe ambayo inaonyesha mahusiano ya jinsia moja. Michoro hiyo ya maelfu ya miaka iliyopita na vilevile ushahidi mwingine wa kihistoria unaonyesha kuwa ushoga umekuwepo katika bara la Afrika tangu kale.

Miongo mingi ya utafiti na uzoefu ya kitabibu imepelekea mashirika ya afya na ya afya ya akili kutamka kuwa mielekeo hiyo si ugonjwa. Shirika la Afya Duniani (WHO) liliondoa ushoga katika orodha yake ya magonjwa ya akili mnamo 1990.

Vyanzo vyake

Hakuna makubaliano kati ya wanasayansi juu ya sababu hasa ambazo humfanya mtu kuwa na mwelekeo wa kupenda jinsia ileile ya kwake au kupenda jinsia zote mbili badala ya jinsia tofauti. Hata hivyo, wanasayansi wanakubaliana kwamba chanzo cha mwelekeo wa kimapenzi wa mtu ni muungano changamani wa vipengele vya kibiolojia na kimazingira.

Wanasayansi wengi wanafikiri mwelekeo wa kimapenzi hauwezi kubadilika kwa hiari, utashi, nguvu, au malezi tofauti.. Hadi leo, hakuna utafiti wa kutosha wa kisayansi kuonyesha kwamba tiba inayolenga kubadili mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja ni salama au inafaa. Kwa kuongezea, uhamasishaji wa matibabu ya mabadiliko unaonekana kuchangia mazingira mabaya kwa wapenzi wa jinsia moja.

Hata hivyo, tafiti mbalimbali zimeonyesha watu hao wana matatizo makubwa ya kiakili au walau wana urahisi mkubwa zaidi wa kupatwa nayo .

Misimamo ya sheria

Mapenzi Ya Jinsia Moja 
Mashoga wa Marekani.
Mapenzi Ya Jinsia Moja 
Wasagaji wa Marekani.
Mapenzi Ya Jinsia Moja 
Sheria za nchi kuhusu ushoga
     Ndoa za jinsia moja      Mahusiano mengine      Laws against expression      Faini au kifungo (haitekelezwi)      Faini au kifungo      Adhabu ya kifo (haitekelezwi)      Adhabu ya kifo

Pengine mashoga, wasagaji na wapenda jinsia zote mbili hukumbana na unyanyapaa, na hata ukatili kwa sababu ya mwelekeo wao wa kimapenzi tofauti na kawaida. Wengine hubaguliwa kwenye shule, vyuo na sehemu zao za kazi, hata wananyimwa huduma za afya na haki, na hupata msaada mdogo kutoka kwa wanafamilia na marafiki. Hali hiyo hufanya iwe vigumu kujitangaza kuwa shoga, msagaji, au mpenda jinsia mbili.

Tatizo hilo la kimataifa ni kubwa zaidi katika nchi nyingi za Afrika. Kituo cha Utafiti cha Pew mnamo 2020 kiligundua kuwa 14% tu ya Wakenya wanaona mapenzi ya jinsia moja yanapaswa kukubalika. Hivyo katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), isipokuwa Rwanda, ngono ya jinsia moja huchukuliwa ni uhalifu na pengine adhabu iliyopangwa ni kifungo cha muda mrefu, ingawa kwa kawaida haitekelezwi. Matokeo yake, wachache tu wako wazi kuhusu mwelekeo wao wa kimapenzi, wakati wengi wanalazimika kuishi kwa usiri na uwongo, ili waendane na maadili yaliyokubalika katika jamii yao.

Chuki dhidi ya mashoga (kwa Kiingereza: “homophobia”) ina madhara makubwa kwa afya ya akili na ustawi wa wasagaji, mashoga na wapenda jinsia mbili, hasa wakijaribu kuficha mwelekeo wao wa kimapenzi. Unyanyapaa na ukatili vinazidisha mafadhaiko waliyonayo tayari kutokana na kutambua tofauti iliyopo kati ya mwili wao na mwelekeo wao. Mara nyingi wanashindwa kukabili hali hiyo na kujikubali walivyo. Hivyo wako katika hatari ya kuingia ulevi wa aina mbalimbali na kujiua kuliko wenzao wanaovutiwa na jinsia tofauti. Watu wanaotamani kuwasaidia wanaweza kufanya kazi na mashirika husika kuwapatia ushauri nasaha pamoja na kupambana na unyanyapaa.

Mashoga, wasagaji na wapenda jinsia mbili wanaotaka kupunguza unyanyapaa wanaweza kuwa wazi kuhusu mwelekeo wao wa kimapenzi, huku wakichukua tahadhari muhimu ili kuwa salama kadiri iwezekanavyo. Kuwaambia watu wengine kuwa wewe ni mpenzi wa jinsia moja au tofauti huitwa “kujitokeza”. Mara nyingi hiyo ni hatua muhimu ya kisaikolojia kwa sababu wanaohisi lazima wafiche mielekeo yao ya kimapenzi huripoti wasiwasi wa mara kwa mara kuliko mashoga na wasagaji ambao wako wazi.

Misimamo ya dini

Uyahudi, Ukristo, na Uislamu kimapokeo huchukulia tabia za mapenzi ya jinsia moja kuwa ni dhambi. Mafundisho ya Uhindu, Ubudha, Ujain, na Kalasinga hayako wazi kabisa juu ya mwelekeo wa mapenzi ya jinsia moja, na viongozi wa dini hizo wanatoa maoni tofauti. Leo, watu kutoka dini zote wanazidi kukubali mapenzi ya jinsia moja, na hata ndoa ya jinsia moja. Idadi inayokua ya madhehebu ya Uprotestanti hufanya baraka za ndoa za jinsia moja. Asilimia kadhaa za wapenzi wa jinsia moja wanaripoti kwamba hawaoni mgongano kati ya mwelekeo wao wa kimapenzi na imani yao.

Katika Biblia

Kadiri ya Biblia, Mungu baada ya kumuumba Adamu alisema, “Si vema mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwa 2:18). Maana yake, umbile la mwanamume linaelekea kukamilishana na lile la mwanamke kiroho na kimwili. Kwa kuwa roho haionekani, ni rahisi zaidi kuona jinsi miili yao inavyofaa kuungana iwe mwili mmoja. Hata hivyo mkamilishano huo unafanyika katika nafsi pia, ambazo zina vipawa tofauti vinavyowezesha kwa pamoja kukabili vizuri maisha ya nyumbani, ya uchumi, ya siasa, ya dini n.k. Kufikiria uumbaji wa mtu katika jinsia mbili ndiyo njia ya kuelewa Muumba alitaka nini, kwamba jinsia hizo zinalenga kukamilishana katika ndoa kwa kupendana na kuzaliana (Mwa 1:26-28): "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi".

Kadiri ya Mtume Paulo, kushindwa kutambua kwamba jinsia hizo mbili zinalenga kukamilishana katika ndoa kwa kupendana na kuzaliana ni sawa na kupotewa na hekima.

Katika Kanisa Katoliki

Papa Fransisko, mkuu wa Kanisa Katoliki, ameongea mara kwa mara juu ya hitaji la kukaribisha na kupenda watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kimapenzi, kwa kuwa wote ni sura na mfano wa Mungu. Hata hivyo mafundisho ya Kikatoliki The teachings of the Catholic Church on same-sex attraction are summarized in the Catechism of the Catholic Church:

2357 Homosexuality refers to relations between men or between women who experience an exclusive or predominant sexual attraction toward persons of the same sex. It has taken a great variety of forms through the centuries and in different cultures. Its psychological genesis remains largely unexplained. Basing itself on Sacred Scripture, which presents homosexual acts as acts of grave depravity, tradition has always declared that 'homosexual acts are intrinsically disordered.' They are contrary to the natural law. They close the sexual act to the gift of life. They do not proceed from a genuine affective and sexual complementarity. Under no circumstances can they be approved.

2358 The number of men and women who have deep-seated homosexual tendencies is not negligible. This inclination, which is objectively disordered, constitutes for most of them a trial. They must be accepted with respect, compassion, and sensitivity. Every sign of unjust discrimination in their regard should be avoided. These persons are called to fulfill God's will in their lives and, if they are Christians, to unite to the sacrifice of the Lord's Cross the difficulties they may encounter from their condition.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Mapenzi Ya Jinsia Moja  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapenzi ya jinsia moja kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Mapenzi Ya Jinsia Moja IstilahiMapenzi Ya Jinsia Moja HistoriaMapenzi Ya Jinsia Moja Vyanzo vyakeMapenzi Ya Jinsia Moja Misimamo ya sheriaMapenzi Ya Jinsia Moja Misimamo ya diniMapenzi Ya Jinsia Moja Tazama piaMapenzi Ya Jinsia Moja MarejeoMapenzi Ya Jinsia Moja Viungo vya njeMapenzi Ya Jinsia MojaJinsiaKiingerezaMapenziTabia

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMwakaNguruwe-kayaBiasharaUfugajiMohamed HusseinBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiNomino za pekeeMagonjwa ya kukuMbeziMaji kujaa na kupwaYesuMadhara ya kuvuta sigaraMtakatifu PauloMajiUtamaduniHistoria ya KenyaMkanda wa jeshiMbossoVasco da GamaWilaya ya IlalaNuktambiliFamiliaAdolf HitlerWanyama wa nyumbaniHisiaNgeliMkoa wa IringaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiUandishi wa barua ya simuKassim MajaliwaArsenal FCNembo ya TanzaniaAgano JipyaKitenzi kikuu kisaidiziMishipa ya damuRayvannyPunyetoWilaya ya KinondoniTasifidaMajira ya baridiKinembe (anatomia)Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya TanzaniaKihusishiTashihisiKengeMauaji ya kimbari ya RwandaPumuMkoa wa Unguja Mjini MagharibiMapenzi ya jinsia mojaAfrika Mashariki 1800-1845Baraza la mawaziri TanzaniaTambikoUjimaNamba tasaOrodha ya kampuni za TanzaniaMaambukizi ya njia za mkojoJoziNamba ya mnyamaAina za ufahamuSakramentiMjombaTarbiaMahindiLigi ya Mabingwa UlayaUtumwaMkonoKataKiambishi awaliKisaweMkoa wa RuvumaImani🡆 More