Jinsia ni hali ya viumbe hai wengi kuwa wa kiume au wa kike, jambo muhimu katika mpango wa kuendeleza uhai kupitia uzazi.
Hata hivyo, si viumbe vyote vinaendeleza uhai kwa njia ya uzaliano kijinsia:
Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu mapendo |
Moyo katika mapokeo ya Ulaya ni mchoro unaowakilisha mapendo. |
Vipengele Msingi |
---|
Mapendo kadiri ya sayansi |
Mapendo kadiri ya utamaduni |
Upendo (fadhila) |
Upendo safi |
Kihistoria |
Mapendo ya kiuchumba |
Mapendo ya kidini |
Aina za hisia |
Mapendo ya kiashiki |
Mapendo ya kitaamuli |
Mapendo ya kifamilia |
Mapendo ya kimahaba |
Tazama pia |
Mafungamano ya binadamu |
Jinsia |
Tendo la ndoa |
Maradhi ya zinaa |
Siku ya wapendanao |
Kuna pia njia ya kujizalisha ambayo ni namna ya pekee ya uzalioni kijinsia. Mimea kama karanga na pia wanyama kadhaa mfano vyawa na samaki kadhaa wanaweza kuanzisha wadogo bila manii ya kiume. Wanyama kama mategu ni huntha wanaobeba manii pamoja na vijiyai mwilini na wanazaa ndani yao.
Kati ya wanadamu hali ya kuwa mwanamume au mwanamke inategemea nukta ya utungaji mimba na kudumu moja kwa moja.
Inatokana na milioni za mbegu zilizomo kwa kawaida katika shahawa ya mwanamume, ambazo baadhi yake ni za kiume (zenye chembeuzi Y) na baadhi za kike chembeuzi X.
Kijiyai cha mwanamke hakichangii uainishaji wa jinsia ya mtoto, kwa kuwa kina pea ya chembeuzi X tu.
Ikiwa mbegu inayowahi kujipenyeza katika kijiyai cha mwanamke ni ya kiume, mimba itakuwa ya kiume (XY), kumbe ikiwahi moja ya kike, mimba itakuwa ya kike (XX).
Kulingana na tofauti hiyo, binadamu huyo mpya atazidi kukua na kutokeza viungo maalumu vya uzazi kama:
Viungo hivyo vitakomaa wakati wa ubalehe.
Ni pia muhimu kazi ya chachu za jinsia (homoni za jinsia) zilizo tofauti kwa mwanamume na mwanamke.
Sehemu fulani ya tofauti kati ya jinsia mbili hutegemea pia utamaduni.
Katika kila jamii, hasa zilizoendelea, kuna idadi fulani ya watu ambao utambuzi wa jinsia si wa kawaida kutokana na hali ya pekee ya chembeuzi (hasa XYY na XXY) au uwepo wa homoni za jinsia nyingine ndani yao au uwepo wa viungo vya uzazi mchanganyiko au visivyo kamili au visivyoeleweka. Hata hivyo chembeuzi Y inathibitisha kuwa mhusika ni wa kiume.
Watu wengine wana tatizo la utasa, ambalo linazidi kuongezeka hasa katika nchi zilizoendelea hata kuvuka asilimia 10 ya wakazi.
Wengine, kwa sababu zisizoelezeka vya kutosha na biolojia wala saikolojia, hawajisikii ipasavyo na jinsia yao (hasa ubaridi wa kijinsia na elekeo la ushoga na usagaji).
Siku hizi watu huongea mara nyingi juu ya usawa wa jinsia mbili. Hakika kuna usawa wa hadhi kati ya mwanamke na mwanamume. Kwa mfano, Biblia inatangaza usawa huo wa binadamu wote tangu sura yake ya kwanza (Mwa 1:26-30). Humo tunajifunza kwamba: wote wameumbwa na Mungu, tena kwa sura na mfano wake, wote wametiwa roho, wote wana akili na utashi, wote wamepata baraka yake ili kuongezeka na wote wamepewa uwezo wa kutawala dunia pamoja na vyote vilivyomo. Hata hivyo, kila mmoja ni sura na mfano wa Mungu kwa namna fulani tu, hivi kwamba mwanamke anafanana zaidi na Mungu katika baadhi ya sifa zake na mwanamume vilevile katika sifa nyingine.
Kutambua tofauti za maumbile ya mwanamke na mwanamume ni msaada mkubwa kwa ajili ya kuelewana na kushirikiana vizuri. Ujuzi huo unamwezesha mtu kufahamu kwa nini mwingine anawaza, anasema na kutenda tofauti naye. Mradi ujuzi wa udhaifu wa kila upande usimfanye yeyote ajikuze na kumdharau mwenzake, wala ajisikie mnyonge, bali uamshe ndani yake juhudi za kukamilika kwa kushinda udhaifu alionao. Hata hivyo mwenzake aelewe kwamba juhudi hizo haziwezi kufaulu mia kwa mia kutokana na umbile lilivyo.
Tofauti za maumbile na tabia kati ya wanawake na wanaume zinajitokeza tayari katika mbegu za kike na za kiume, ambazo zote zinatengenezwa na mwili wa mwanamume, lakini za kwanza ni fupi zaidi, zinakwenda polepole zaidi ila zinadumu kirefu kuliko za pili baada ya kutoka mwilini mwa baba. Ni hizo mbegu ambazo zinamiminwa kwa mamilioni ndani ya mwili wa mama na kushindana ili ziwahi kufikia kijiyai kilichoiva, ambacho kwa kawaida ni kimoja tu na kinasubiri mgeni wake.
Mbegu yoyote ya mwanamume, iwe ya kike au ya kiume, inapopenya kijiyai cha mwanamke, mara inapatikana mimba ya seli moja ambayo tayari ina jinsia yake isiyoweza kubadilika tena kwa namna yoyote ile, hata baada ya mtoto kuzaliwa, kukua na hatimaye kufa. Seli zake zote zitakuwa daima za jinsia ile. Utambulisho huo wa msingi unasababishwa na baba tu.
Kadiri seli ya kwanza inavyozidi kujigawa, viungo vya mwili vinazidi kupatikana na tofauti zifuatavyo zinazidi kutokea upande wa jinsia kulingana na mbegu ilivyokuwa:
Kutokana na tofauti hizo na nyinginezo, wanawake wanafaa zaidi kwa kazi kadhaa na wanaume kwa kazi nyingine. Mwanamke hawi bora anapofaulu kufanana na mwanamume, bali anapokuwa mwenyewe kama alivyo, yaani alivyoumbwa na Mungu kwa ajili ya umoja wa wawili tofauti. Si suala la ubaguzi, bali ni maumbile, hivyo ni hekima ya Mungu.
Jinsia mbili zinaposhirikiana kwa upendo na heshima bila kushindana, familia na jamii zinakwenda vizuri kwa michango maalumu ya jinsia zinazokamilishana. Kinyume chake, pale ambapo wanawake wanataka kushindana na wanaume ili washike nafasi yoyote, sisi sote tunakosa ule mchango maalumu wa jinsia ya kike hata kuliko wanapobaguliwa na kuzuiwa wasiutoe.
Kwa msingi huo unaweza ukaeleweka uamuzi wa Yesu wa kuteua wanaume tu kuwa mitume ingawa aliwaheshimu sana wanawake, kuanzia Mama yake, Bikira Maria. Huyo, aliye kielelezo cha wanawake wote, kwa upendo wake kamili alichangia na anazidi kuchangia ustawi wa Kanisa na wa ulimwengu kuliko mtume yeyote yule. Kwa kuwa Yesu ametuonyesha kuwa jambo bora si kutawala, bali kupenda na kutumikia kama mwenyewe alivyofanya akiongozwa na Roho Mtakatifu, ambaye ndani ya Mungu ni Upendo-Nafsi, ni Zawadi-Nafsi anayekamilisha umoja wa Baba na Mwana. Ndiyo sababu anatusukuma kupenda na kujitoa badala ya kutaka kutawala. Katika hilo wanawake wanaelekea zaidi.
Kimsingi zaidi, inafaa tujitahidi kuelewa fumbo la Mwana wa Mungu kujifanya mwanamume awe bwanaarusi wa Kanisa linalokusudiwa kumzalia watu wote kabisa. Ingawa Mungu hana mwili, na kwa sababu hiyo hana jinsia, Yesu Mwanae ni mwanamume na ametushirikisha uhusiano wake na Mzazi wa milele aliyemuita Baba. Hilo si bure: ndiye aliyetangulia kutupenda na ndiye anayetuwezesha kufanya lolote. Kazi yetu ni hasa kuwa tayari kupokea upendo wake na utendaji wake wowote ili uzima ustawi ndani mwetu na kandokando yetu.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jinsia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.