Mkoa wa Iringa ni mojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 51000.
Upo katikati ya nchi, kidogo upande wa kusini. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Njombe, Mbeya, Singida na Dodoma.
Makao makuu yako katika manisipaa ya Iringa.
Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania na kupakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania upande wa kaskazini.
Hadi mwaka 2012 Mkoa wa Iringa ulikuwa na eneo lenye ukubwa wa jumla ya km² 58,936. Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km² 43,935.
Tangu mwaka 2012 wilaya tatu za kusini zimetengwa na Iringa na kuwa mkoa mpya (Mkoa wa Njombe) kwa hiyo eneo la Iringa limepungua kilomita za mraba 21,347. Eneo linalobakia la km² 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama milima na misitu.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 1,192,738 katika wilaya 5 zifuatazo: Iringa Vijijini (wakazi 315,354), Mufindi (wakazi 288,996), Kilolo (wakazi 263,559), Iringa Mjini (wakazi 202,490), na Mafinga Mjini (wakazi 122,329).
Wenyeji wa mkoa ni hasa Wahehe; wengine wanatokea makabila ya jirani kama Wabena, Wakinga, Wapangwa, Wasangu, Wawanji, Wagogo n.k.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mkoa wa Iringa, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.