Nembo Ya Tanzania

Nembo ya Tanzania ni ngao ya askari inayoshikwa na watu wawili.

Nembo Ya Tanzania
Nembo ya Tanzania

Ngao ina sehemu nne: juu sehemu ya dhahabu, chini yake bendera ya taifa, halafu sehemu nyekundu na chini kabisa sehemu ya buluu-nyeupe;

a) robo ya juu inaonyesha mwenge wa uhuru juu ya rangi ya dhahabu inayokumbusha juu ya utajiri wa madini ya nchi

b) robo ya pili ni bendera ya Tanzania

c) rangi nyekundu inamaanisha ardhi nyekundu ya Afrika na kilimo kama msingi wa maisha ya watu.

d) milia ya buluu na nyeupe katika robo ya nne inamaanisha mawimbi ya bahari na maziwa kwenye mipaka ya nchi pamoja na bahari inayozunguka Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano.

Juu ya sehemu hizo kuna mkuki na majembe mawili yanayokumbusha juu ya utetezi wa uhuru na umuhimu wa kazi katika ujenzi wa taifa.

Ngao yote imeviringishwa na mapembe ya ndovu yanayomaanisha utajiri wa wanyamapori na hifadhi za taifa.

Ngao inalala juu ya mlima Kilimanjaro ambayo ni mlima mkubwa wa Tanzania.

Watu wawili wanaoshika ngao ni mwanamume na mwanamke kama dalili ya ushirikiano wa jinsia zote mbili taifani. Wanasimama juu ya mpamba na mkarafuu ambayo yote inatoa mazao muhimu ya kibiashara ya Tanzania Bara kwa pamba na Zanzibar kwa karafuu.

Kanda njano ya maandishi chini ya ngao huonyesha kaulimbiu ya taifa "Uhuru na Umoja".

Viungo vya nje

Tags:

AskariNgao

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mungu ibariki AfrikaMaudhui katika kazi ya kifasihiWilaya ya RufijiDemokrasiaUgonjwa wa uti wa mgongoNuruMahakamaUpendoOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaRashidi KawawaStafeliNabii EliyaJumuia ndogondogo za KikristoUbadilishaji msimboAzimio la ArushaJuaCherehaniBaraza la Maaskofu Katoliki TanzaniaNg'ombePalestinaWanu Hafidh AmeirWangoniUNICEFMkoa wa MtwaraViunganishi vihusishiOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaKibena (Tanzania)Wilaya ya UkereweLuis MiquissoneAfrika ya Mashariki ya KijerumaniMizimuKen WaliboraKunguruVitenzi vishirikishi vikamilifuNelson MandelaKalenda ya KiislamuKhadija KopaMohamed HusseinSintaksiHistoria ya WapareJipuAwilo LongombaWilaya ya TunduruMvuaKinyongaKidole cha katiUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaUandishiMtume PetroViungo vinavyosafisha mwiliLigi ya Mabingwa UlayaHistoria ya TanzaniaMkanda wa jeshiMfumo wa upumuajiNamba ya mnyamaNomino za pekeeMweziAlfu Lela U LelaHortense Aka-AnghuiVihisishiWanyamboHelaBaha'iNevaFasihi andishiVivumishi vya idadiMsambaKisaweVivumishi vya -a unganifuMitume na Manabii katika UislamuHoma ya manjanoHisia🡆 More