Bara (au kontinenti) ni pande kubwa la nchi kavu la Dunia linalozungukwa na bahari.
Kwa kawaida tunatofautisha mabara 7 ya Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antaktiki, Asia, Australia, na Ulaya.
Ramani ya dunia inayoonyesha mabara saba yanayohesabiwa kwa kawaida. |
Neno "bara" lamaanisha pande kubwa la nchi kavu , tofauti na bahari au visiwa vidogo karibu na pwani ya nchi kavu kubwa zaidi. Neno "kontinenti" latokana na Kilatini "terra continens" yaani "nchi (kavu) mfululizo".
Kwa hiyo elezo la neno bara / kontinenti katika sayansi ya jiografia ni "masi kubwa na mfululizo za nchi kavu zinazotengwa kwa maeneo makubwa ya maji" Lakini hali halisi sehemu kubwa ya mabara saba yanayokubaliwa kwa kawaida hayatengwi kabisa kati yake kwa maji. Kwa mfano Ulaya na Asia hayatengwi kabisa na tofauti yake ni kihistoria na kiutamaduni, si kijiografia. Pia neno "masi kubwa" halieleweki waziwazi kabisa. Kwa nini Greenland yenye eneo la kilomita za mraba 2,166,086 inaitwa "kisiwa" lakini Australia yenye eneo la 7,617,930 huitwa bara?
Mabara yote ya Dunia yetu huwa na pwani kwenye bahari kuu ambayo ni moja tu ikigawiwa kwa sehemu mbalimbali na mabara vigezo vingine.
Kwa lugha ya kawaida “bara” ni eneo mfululizo wa nchi kavu. Kwa maana hii “Tanzania bara” ni eneo lote la Tanzania isipokuwa visiwa ambavyo ni sehemu ya nchi ya Tanzania bila visiwa vya Unguja, Pemba, Mafia na kadhalika.
Vivyo hivyo “Ulaya bara” ni eneo la Ulaya bila visiwa kama Britania, Eire, Malta na kadhalika.
Kwa macho ya jiolojia “bara” ni pana kuliko nchi kavu tu. Tunaangalia eneo lote la miamba inayounda bara. Siku hizi tunajua kwamba kila bara linalingana na kipande cha ganda la dunia tunachoita bamba la bara (continental plate). Kipande hiki kinaendelea pia chini ya uso wa bahari katika tako la bara (continental shelf) katika maji yasiyo na kina kikubwa pamoja na visiwa vya sehemu hizi. Kwa mtazamo huu visiwa vya Britania na Eire ni sehemu za Ulaya na vivyo hivyo Autralia na Guinea Mpya ni bara moja.
Kwa maana ya utamaduni wazo la bara linaweza kujumlisha pia visiwa vya mbali kama vile Iceland huhesabiwa sehemu ya Ulaya au hata mikoa ya Ufaransa katika Bahari Hindi kuhesabiwa kisiasa katika Ulaya.
Kwenye ramani zinazotumia lugha ya Kiingereza kawaida huhesabiwa mabara saba duniani, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo.
Mara nyingi visiwa vya Pasifiki hujumlishwa pamoja na Australia kama
na kuhesabiwa kama bara.
[[File:Continental models-Australia.gif|thumb|450px|Ramani inayoonyesha njia mbalimbali za kugawa dunia kwa mabara. Kutegemeana na mawazo ya wataalamu mabara huweza kuhesabiwa kwa namna tofauti. Kwa mfano Eurasia kwa kawaida huhesabiwa kuwa mabara 2 Ulaya na Asia (nyekundu). Wengine hujumlisha pia Eurasia pamoja na Afrika kuwa bara 1. Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini wakati mwingine hutazamiwa kuwa bara moja ya Amerika.
Kutokana na elezo kuu kuwa bara ni masi ya nchi kavu iliyotengwa na bara nyingine kwa maji kuna mawazo tofauti kuhusu idadi ya mabara.
wakibaki na Amerika, Afro-Eurasia, Australia na Antaktiki.
Mabara jinsi yalivyo leo hayakuwepo tangu mwanzo wala hayakai vile. Ilhali kila bara linalingana na bamba 1 au mabamba ya gandunia ina pia mwendo pamoja na bamba lake. Wanajiolojia huamini ya kwamba miaka mamilioni iliyopita mabara yote yaliwahi kukaa pamoja kama bara 1 kubwa sana lililoendelea kupasuliwa baadaye. Vipande huelea juu ya koti ya dunia ambayo ni kiowevo na moto. Mwendo wa mabamba umepimiwa kuwa sentimita kadhaa kila mwake. Uhindi zamani haikuwepo sehemu ya Asia, na sasa hivi Afrika inaelekea kupasuliwa kwenye mstari wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.
Bara | Eneo (km²) | Asilimia ya nchi kavu yote | Wakazi 2008 | Asilimia ya Wakazi wa dunia | Msongamano wa watu kwa km² |
---|---|---|---|---|---|
Asia | 43,820,000 | 29.5% | 369,000,000 | 36% | 86.70 |
Afrika | 30,370,000 | 20.4% | 222,011,000 | 22% | 29.30 |
Amerika Kaskazini | 24,490,000 | 16.5% | 168,720,000 | 16% | 21.0 |
Amerika Kusini | 17,840,000 | 12.0% | 152,000,000 | 15% | 20.8 |
Antaktika | 13,720,000 | 9.2% | 1,000 | 0.00002% | 0.00007 |
Ulaya | 10,180,000 | 6.8% | 203,000,000 | 20% | 69.7 |
Australia | 9,008,500 | 5.9% | 32,000,000 | 0.3% | 3.6 |
Eneo la dunia yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu.
Mabara jinsi yanavyoonekana hukaa juu ya mabamba ya gandunia ambayo ni vipande vikubwa vya mwamba vinavyounda uso wa dunia. Mabara tunavyoyajua yanalingana kila moja na bamba lake na kila bamba ina mwendo wake wa polepole. Hii ni sababu ya kwamba baada ya miaka mingi uso wa dunia utaonekana tofauti kuliko leo.
Kijiolojia bara haliishi kwenye pwani pale bahari inapoanza. Bara linaendelea chini ya uso wa bahari kama tako la bara.
Mabara na mabamba yao ni kama ifuatayo: Afrika (Bamba la Afrika), Antaktika (Bamba la Antaktika), Australia (Bamba la Australia), Ulaya na sehemu kubwa ya Asia (Bamba la Ulaya-Asia), Amerika Kaskazini pamoja na Siberia (Bamba la Amerika ya Kaskazini) na Amerika Kusini (Bamba la Amerika ya Kusini). Mabamba madogo yamejitenga ingawa nchi juu yao inaonekana kuwa sehemu ya bara lingine. Mfano wake ni Bara Hindi iliyokuwa kama bara ndogo au kisiwa kikubwa zamani lakini tangu miaka milioni 10 imejisukuma chini ya bamba la Asia-Ulaya na kuikunja hadi kutokea kwa milima ya Himalaya.
Kwa jumla miamba ya sehemu za mabara ni mipesi kushinda miamba ya chini na hii ni sababu ziko juu ya miamba mingine.
Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 192 katika mabara yote ya ulimwengu, mara huzidi kukitokea na mgawanyiko wa nchi au hupungua kukitokea umoja au muungano wa nchi.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Bara, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.