Mbosso: Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania

Mbwana Yusuph Kilungi (anajulikana kwa jina lake la kisanii kama Mbosso; amezaliwa 3 Oktoba 1991) ni mwimbaji, mtunzi na mwanamuziki kutoka nchini Tanzania.

Umaarufu ulianza akiwa na kundi zima la Yamoto Band ambalo ndani yake kuliwa na Aslay, Beka Flavour, Enock Bella na Mbosso. Kwa pamoja walikuwa wanaunda Yamoto Band chini ya Mkubwa Fella na Wanawe. Jina la Mkubwa na Wanawe lilikuwa na hadi sasa bado lipo hivyo hivyo kama Mkubwa na Wanawe. Ndani ya mkubwa na Wanawe kuna vipaji mbalimbali.

Baada ya Yamoto Band kufa, Mbosso aliamua kurudi nyumbani kwao kijijini huko Kibiti. Ambapo alijihusisha na vitendo mbalimbali vya kihalifu hasa kwa kukata tamaa na kuona wenzi wake wakiwa wanapata mafanikio yeye akiwa amebaki tu nyumbani. Jambo hili, lilikuwa tofauti kidogo na kina Aslay na Beka Flavour. Hawa waliendelea kutamba katika muziki hadi hapo Diamond Platnumz alipoona muda huu unafaa sasa kumrudisha Mbosso katika tasnia ya muziki kama alivyomuahidi mnamo mwakwa 2014 ya kwamba atamsaidia na kumuweka kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava. Wimbo wa kwanza wa Mbosso ulitoka mnamo tarehe 28 Januari 2018 na ulikwenda kwa jina la Watakubali.

29 Januari alitambulishwa mbele ya hadhira ya kwamba yeye ni msanii kamili aliyesaini mkataba na WCB.

Hadi sasa Mbosso ametoa wimbo kama vile Watakubali, Nimekuzoea, Alele, Shida, Picha Yake, Hodari, Nipepe, Hodari, Tamu. Wimbo mwingine aliotoa na kundi la Wasafi jina lake lilikuwa Zilipendwa na wimbo mwingine aliotoa na Diamond Platnumz na lavalava wimbo ambao jina lake ni Jibebe.

Marejeo

Mbosso: Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbosso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

19913 OktobaJina la kisaniiMtunziMwanamuzikiMwimbajiTanzania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Vasco da GamaFani (fasihi)Namba tasaKiarabuAmri KumiIniRwandaVielezi vya mahaliLenziHedhiUkomeshaji wa Biashara ya WatumwaMbuga za Taifa la TanzaniaNdiziPunyetoAndalio la somoMusaKassim MajaliwaLugha rasmiDini nchini KenyaShuleViunganishiZabibuHakiHistoria ya WokovuUkristoUzazi wa mpango kwa njia asiliaUtawalaVivumishiMfuko wa Taifa wa Hifadhi ya JamiiAfrika KusiniUhuru wa TanganyikaOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaKongoshoTundu Antiphas Mughwai LissuKiimboDNAMikoa ya TanzaniaJakaya KikweteFisiWanyakyusaZama za ChumaMiundombinuSanaaFigoKishazi tegemeziSensaWallah bin WallahTeknolojiaTabiaUmoja wa Muungano wa AfrikaWangoniHassan MwakinyoKiambishi awaliAgano la KaleMuungano wa Madola ya AfrikaAmfibiaUkuaji wa binadamuShengFutiUshairiNandyOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaSintaksiHenokoMkoa wa SongweHuduma ya kwanzaNomino za wingiUtamaduniUaKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniMkoa wa RukwaMsituPijiniBongo FlavaPonsyo Pilato🡆 More