Raymond Shaban Mwakyusa (anafahamika zaidi kwa jina lake kama Rayvanny; amezaliwa 22 Agosti 1993) ni mwimbaji na mtunzi wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania (kwa asili ni mtu wa mkoani Mbeya).
Rayvanny | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Raymond Shaban Mwakyusa |
Pia anajulikana kama | Rayvanny |
Amezaliwa | 22 Agosti 1993 |
Asili yake | Mbeya,Tanzania |
Aina ya muziki | Bongo Flava,Afro Pop |
Kazi yake | Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi |
Ala | Piano, sauti |
Miaka ya kazi | 2011–mpaka sasa |
Studio | Wasafi Records,Next Level Music |
Ame/Wameshirikiana na | Harmonize, Diamond Platnumz |
Tovuti | Rayvanny |
"Rayvanny" alianza kujulikana kupitia wimbo wake "Kwetu" si siku nyingi sana tangu Harmonize atoe wimbo wake wa Bado.
Baadaye Natafuta Kiki, Sugu ambayo imetolewa kama wimbo wa ziada tu hasa ukizingatia umechukua biti ya Bow Wow (What's My Name). Halafu Mbeleko, Shikwambi, Zezeta na Kijuso aliyoimba na Queen Darleen, Pochi Nene aliyoimba na s2kizzy na baadaye Mwanza wimbo ambao aliimba na msanii mwenzie Diamond Platnumz. Wimbo huo ulifungiwa na Baraza la Sanaa nchini Tanzania BASATA kutokana na kutokuwa na maadili mema hivyo kufanya wimbo huo kufungiwa kupigwa kwenye vyombo vya habari nchini Tanzania.
Baada ya wimbo huo kufungiwa yeye na Diamond walitoa wimbo uitwao Tetema, wimbo ambao ulipendwa na watu wengi kuufanya kuwa na watazamaji wengi kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mfupi sana.
Nambari | Mada ya wimbo | Mwaka | Tan |
---|---|---|---|
1. | "Kwetu" | 2016 | |
2. | "Natafuta Kiki" | 2016 | |
3. | "Sugu" | 2017 | |
4. | "Mbeleko" | 2017 | |
5. | "Shikwambi" | 2017 | |
5. | "Zezeta" | 2017 | |
6. | "Chuma Ulete" | 2017 | |
7. | "Unaibiwa" | 2017 |
Nambari | Mada ya Wimbo | Mwaka | Mwanamuziki mkuu | Tan |
---|---|---|---|---|
1. | "Salome" | 2016 | Diamond Platnumz | |
2. | " Kijuso" | 2017 | Queen Darleen | |
3. | "Zilipendwa" | 2017 | Rich Mavoko, Diamond Platnumz, Mbosso, Harmonize, Lavalava, Queen Darleen | |
1. | "Cuppy jollof on the jet" | 2020 | Rema |
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rayvanny kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Rayvanny, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.