Idi Amin: Rais wa Uganda kuanzia 1971 hadi 1979

Idi Amin Dada (/ˈiːdi ɑːˈmiːn/;  1923–1928 – 16 Agosti 2003) alikuwa mwanasiasa na afisa wa jeshi ambaye alipata kuwa Rais wa Uganda kuanzia mwaka 1971 hadi 1979.

Alitawala kidikteta ilhali uchumi wa nchi uliporomoka na makosa mengi ya jinai dhidi ya haki za kibinadamu yalitendwa.

Idi Amin: Maisha, Mtawala wa Uganda, Marejeo
Idi Amin
Idi Amin: Maisha, Mtawala wa Uganda, Marejeo
Idi Amin pamoja na Askofu Luwum aliyeuawa baadaye kwa amri yake.
Idi Amin: Maisha, Mtawala wa Uganda, Marejeo
Idi Amin akibebwa kifalme na wafanyabiashara Waingereza huko Kampala.

Idadi ya watu waliouawa Uganda chini ya utawala wake imekadiriwa kuwa kati ya 100,000 na 500,000.

Katika miaka yake ya kushika serikali Amin alibadilika kutoka uhusiano wa kirafiki na nchi za magharibi, na hasa Israeli, kuhamia upande wa Muammar Gaddafi wa Libya, Mobutu Sese Seko wa Zaire, Umoja wa Kisovyeti na Ujerumani ya Mashariki. Hata hivyo Amin alipata usaidizi wa ofisi ya upelelezi ya Marekani CIA iliyotuma silaha na vifaa vingine kwa jeshi lake.

Mwaka 1977 Amin alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufalme wa Maungano (Uingereza) akajitangaza kuwa alishinda na kujiongezea sifa ya CBE ("Conqueror of the British Empire"). Kuanzia wakati ule cheo chake rasmi kilikuwa "His Excellency President for Life, Field Marshal Alhaji Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE".

Jaribio la Amin la kutwaa sehemu za Mkoa wa Kagera wa Tanzania kwenye mwaka 1978 lilisababisha Vita ya Kagera baina ya Tanzania na Uganda na mwisho wa utawala wake. Amin alikimbia kukaa ugenini Libya na baadaye Saudia alipoishi hadi kifo chake mwaka 2003.

Maisha

Alikotoka

Hakuna uhakika juu ya mwaka na mahali alikozaliwa. Amin mwenyewe hakuandika kumbukumbu ya maisha yake wala hakuagiza taarifa rasmi juu ya maisha yake. Vyanzo mbalimbali vinasema ya kwamba alizaliwa mnamo 1925 Koboko au Kampala. Mtafiti Fred Guweddeko amedai Amin alizaliwa 17 Mei 1928, lakini hii imepingwa. Mwanawe Amin Hussein alisema babake alizaliwa Kampala mwaka 1928.

Kufuatana na Fred Guweddeko wa Chuo Kikuu cha Makerere Idi Amin alikuwa mwana wa Andreas Nyabire (1889–1976) wa kabila la Wakakwa, ambaye alikuwa Mkatoliki aliyehamia Uislamu mnamo 1910 akibadilisha jina lake kuwa Amin Dada na kumpa mwana wa kwanza jina hilo pia.

Iddi Amin alilelewa na mama yake bila baba kijijini katika Uganda ya Kaskazini-magharibi. Kufuatana na Gudewekko mamake Amin Assa Aatte (1904–1970) alikuwa Mlugbara aliyetibu watu kwa mitishamba. Amin alisoma miaka kadhaa kwenye shule ya Kiislamu huko Bombo kuanzia mwaka 1941.

Amin mwanajeshi

Baada ya miaka michache ya shule na kazi ndogondogo aliajiriwa mwaka 1946 na afisa Mwingereza wa jeshi la kikoloni King's African Rifles (KAR).

Aliingia jeshini huko Jinja akifanya kazi ya msaidizi jikoni akiendelea kupokea mafunzo ya kijeshi. Baadaye Amin alidai ya kwamba alilazimishwa kuhudumia huko Burma katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mwaka 1947 alihamishiwa Gilgil, Kenya. Mwaka 1949 alitumwa kaskazini kwa kupigania waasi Wasomalia huko. Tangu mwaka 1952 kikosi chake kilihudhuria katika juhudi za kupambana na wanamgambo wa Maumau karibu na Mlima Kenya.

Aliendelea kupanda vyeo vilivyopatikana kwa Waafrika katika jeshi la KAR na muda mfupi baada ya uhuru alipewa cheo cha luteni yaani afisa kamili kama mmoja wa Wauganda wawili. Baada ya uhuru wa Uganda mwaka 1962 alikuwa kapteni halafu mwaka 1963 meja. Mwaka 1964 alikuwa makamu wa mkuu na mwaka 1965 mkuu wa jeshi, mwaka 1970 mkuu wa mikono yote ya kijeshi. In 1970, he was promoted to commander of all the armed forces.

Amin jinsi alivyopanda vyeo jeshini
Idi Amin: Maisha, Mtawala wa Uganda, Marejeo  King's African Rifles
1946 aliingia King's African Rifles
1947 Askari wa kawaida
1952 Koplo
1953 Sajenti
1958 Sajenti mtumishi
1959 Effendi (afisa mteule)
1961 Luteni (mmoja kati ya Wauganda wawili waliofikia cheo hiki katika KAR)
Idi Amin: Maisha, Mtawala wa Uganda, Marejeo  Jeshi la Uganda
1962 Kapteni
1963 Meja
1964 Makamu wa Mkuu wa Jeshi la Uganda
1965 Kanali, Mkuuwa Jeshi
1968 Meja Jenerali
1971 Mkuu wa dola
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi wa Dola
Amiri Jeshi Mkuu wa Uganda
1975 Field Marshal

Mkuu wa Jeshi na mapinduzi

Amin alipandishwa cheo na waziri mkuu Milton Obote baada ya uasi wa wanajeshi katika Afrika ya Mashariki wa 1964 uliokomeshwa na askari Waingereza katika Tanganyika, Kenya na Uganda akawa makamu wa mkuu wa Jeshi aliyekuwa bado Mwingereza. Kutoka hapa alishirikiana na Obote katika hatua za kuimarisha utawala wa waziri mkuu. Wakati bunge la Uganda lilitaka utafiti kuhusu mashtaka ya Obote kushiriki katika biashara ya siri ya pembe za ndovu kutoka Kongo Obote iliamua kubadilisha katiba na jeshi la Amini lilimfukuza Mkuu wa Dola Kabaka Mutesa kwa nguvu, halafu Obote alijitangaza kuwa rais. Sasa Amin alikuwa kanali na Mkuu wa Jeshi.

Amin alianza kuajiri hasa askari kutoka kaskazini ya Uganda mpakani mwa Sudani.

Idi Amin: Maisha, Mtawala wa Uganda, Marejeo 
Milton Obote, Rais wa pili wa Uganda, ambaye alipinduliwa na Idi Amin mwaka 1971.

Mwaka 1970 Obote aliendelea kumpa Amin cheo cha mkuu wa mikono yote ya jeshi na ulinzi. Lakini Amin alisikia pia ya kwamba kulikuwa na mashtaka dhidi yake kutokana na matumizi ya makisio ya jeshi na mipango ya Obote kumfanyia utafiti. Hapo Amin alitumia nafasi ya safari ya Obote kwenda nje kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, akatwaa mamlaka ya serikali tarehe 25 Januari 1971.

Mtawala wa Uganda

Mwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka.

Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake.

Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Kanada hasa.

Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979.

Amin alitorokea Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulikia siasa tena.

Alikufa mjini Jeddah tarehe 16 Agosti 2003.

Marejeo

Idi Amin: Maisha, Mtawala wa Uganda, Marejeo  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Idi Amin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Idi Amin MaishaIdi Amin Mtawala wa UgandaIdi Amin MarejeoIdi Amin16 Agosti19231928197119792003AfisaDiktetaHaki za kibinadamuJeshiJinaiMwakaMwanasiasaRaisUchumiUganda

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Israeli ya KaleMazingiraNikki wa PiliMajiNomino za kawaidaVivumishi vya pekeeRamadan (mwezi)VieleziUholanziRoho MtakatifuShairiKitenziUhaiTungo kishaziAdhuhuriUhifadhi wa fasihi simuliziVivumishi vya -a unganifuAgano JipyaUkatiliUtumbo mwembambaMtemi MiramboSheriaBiolojiaNomino za pekeeMilki ya OsmaniMkoa wa PwaniHistoria ya KanisaWanyamweziWaraka kwa WaebraniaSumakuSarujiKamusi ya manaa na matumiziBabeliMimba kuharibikaJokate MwegeloPauline Philipo GekulUharibifu wa mazingiraJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaSeli za damuRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniKiambishiAina za udongoYG7Viwakilishi vya kuoneshaMafuta ya petroliRisalaUsafi wa mazingiraUkimwiMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaMaliasiliPaa (maana)UfupishoIdi AminHistoriaLafudhiAndalio la somoOrodha ya vitabu vya BibliaHifadhi ya mazingiraOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaAina za manenoNgonjeraMapenziKhadija KopaKamusi ya Kiswahili - KiingerezaEdward SokoineWachaggaMichezo ya jukwaaniKilwa KisiwaniKiimboKinjikitile NgwaleKuraniNyekunduNdoa katika Uislamu16🡆 More