Ndoa

Ndoa ni muungano kati ya watu wawili au zaidi unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii.

Tukio la kuanzisha ndoa linaitwa harusi, na kabla ya ndoa kuni kipindi cha uchumba ambapo watu hao wawili walio kubaliana wanachunguzana tabia na kujifunza au kujuana zaidi baina yao. Kama watu wanaohusika wakikomesha ndoa yao kisheria, hali hii inaitwa talaka.

Ndoa
Pete, alama ya ndoa.

Katika utamaduni wa nchi nyingi uhusiano huo ni kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja tu na unalenga ustawi wao na uzazi wa watoto katika familia.

Katika nchi nyingine, hasa za Kiislamu na za Afrika, inakubalika ndoa kati ya watu wawili ambao mmojawapo ana au anaweza kuwa na mwenzi au wenzi wengine pia (mitara au upali), hususan ndoa ya mwanamume mmoja na wanawake zaidi ya mmoja. Kumbe kwingine, hasa Ulaya, hilo ni kosa la jinai.

Mara nyingi harusi inafanyika kwa ibada maalumu kadiri ya dini ya wahusika.

Baadhi ya madhehebu ya Kikristo yanatazama ndoa kati ya wabatizwa wawili kuwa sakramenti: rejea Ndoa (sakramenti). Hasa Kanisa Katoliki linaamini ndoa haiwezi kuvunjwa kwa talaka kutokana na kauli ya Yesu: "Mungu alichokiunganisha, binadamu asikitenganishe" (Mk 10:9).

Suala la ndoa ya jinsia moja

Tangu mwaka 2000 idadi inayozidi kuongezeka ya nchi zimeanza kuruhusu ndoa kati ya watu wawili wa jinsia moja. Kumbe nchi nyingine zinapinga vikali jaribio hilo kama kinyume cha dini na desturi au hata maumbile yenyewe. Tabia za kingono kati ya wanyama wa jinsia moja zimeonekana katika spishi 500 hivi duniani kote, lakini wanaosema kuwa ushoga ni kinyume cha maumbile wanamaanisha maumbile ya binadamu yanayotakiwa kuongozwa na akili na utashi, si silika tu kama ilivyo kwa viumbehai wengine wote. Kwa mfano, wanyama wanazaliana hata wakiwa na undugu, kwa mfano mama na mtoto, lakini kwa binadamu haifai. Vilevile ubakaji unafanywa na wanyama mbalimbali, lakini kwa binadamu haufai kabisa kwa sababu unasababisha mwathiriwa asiyekubali apitie uchungu na mateso. Hiyo ndiyo sababu jamii iliyostaarabika haiwezi kuuvumilia ubakaji; waathiriwa na wote ambao wangeweza kuwa waathiriwa wanapaswa kulindwa wasibakwe. Ulinganisho huo wa ndoa ya jinsia moja na ubakaji si kamili kwa kuwa hauhusishi mwathiriwa asiyekubali, anayelazimika kuvumilia uchungu na mateso, na pengine, badala yake wapenzi wa jinsia moja ambao wanazuiwa kuoana wanajisikia uchungu. Hata hivyo, inabidi kulinda maadili ya jamii ili iweze kustawi dhidi ya tamaa zisizoijenga.

Takwimu zinaonyesha kwamba katika ndoa za jinsia moja uaminifu wa moyoni na wa mwilini ni mdogo kuliko katika ndoa za jinsia mbili.

Uchunguzi mwingi umeonyesha kwamba wanaume waliofunga ndoa za jinsia moja wana kiwango cha talaka cha chini kidogo kikilinganishwa na kile cha watu waliofunga ndoa za jinsia mbili. Ndoa za wanaume wawili zinasedeka kushinda zile za jinsia mbili na zile za wanawake wawili.

Kiwango cha juu cha talaka kati ya wanawake kinapatana na takwimu zinazoonyesha kwamba kwa ujumla wanawake ndio wanaoanzisha talaka zilizo nyingi.

Vilevile utafiti fulani umehusianisha kuhalalishwa kwa ndoa za jinsia moja na upungufu mkubwa wa kiwango cha kujaribu kujiua kwa watoto.

Hata hivyo, nchi nyingi, hasa za Afrika, hazikubali ndoa za jinsia moja. Sheria za nchi nyingine zinawapa watu wawili wa jinsia moja wanaoishi pamoja haki karibu zilezile za watu wa ndoa, lakini zinakwepa kuita miungano hiyo "ndoa".

Tanbihi

Ndoa  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndoa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

HarusiJamiiTalakaWatu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Orodha ya Marais wa TanzaniaDhahabuBaraza la mawaziri Tanganyika 1961KichecheSalaTenziAbedi Amani KarumeStephane Aziz KiUtamaduniOrodha ya Watakatifu WakristoManchester United F.C.Mkoa wa KilimanjaroMajiMawasilianoLionel MessiSaudiaUfupishoMoshi (mji)Afrika ya MasharikiUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiLongitudoNdoaNyasa (ziwa)SarufiMatumizi ya LughaKatibaMishipa ya damuMeliTaasisi ya Taaluma za KiswahiliTarakilishiNomino za dhahaniaMadhehebuMeta PlatformsNishatiNyati wa AfrikaMapambano ya uhuru TanganyikaChuraInshaUainishaji wa kisayansiZana za kilimoBurundiKunguniNembo ya TanzaniaMamba (mnyama)Vielezi vya mahaliRejistaYoung Africans S.C.BundiHekaya za AbunuwasiMkoa wa MaraNenoBarack ObamaKipepeoShinaUchumiUti wa mgongoTupac ShakurTanganyika (ziwa)TeknolojiaUtendi wa Fumo LiyongoIntanetiMaji kujaa na kupwaMatiniAgano JipyaKiingerezaSheriaKibwagizoMilaHistoria ya WokovuVitendawiliMbuVivumishi vya kumilikiOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaRoho MtakatifuLingua franka🡆 More