Mkoa wa Pwani ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 61000.
Mkoa umepakana upande wa Kaskazini na Tanga, upande wa mashariki na Dar-es-Salaam na Bahari Hindi, upande wa kusini na mkoa wa Lindi na upande wa magharibi na mkoa wa Morogoro.
Makao makuu ya mkoa yako Kibaha.
Mkoa huu unalo eneo la km² 32,407, ukiwa na idadi ya wakazi wapatao 2,024,947 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 kutoka 1,098,668 (2012).
Mkoa huu wenyeji wake ni watu wa makabila ya Wakwere, Wazaramo, Wandengereko na Wanyagatwa.
Wilaya ya Rufiji imegawanyika sehemu mbili, visiwani na bara: wenyeji wa visiwani ni wa kabila la Wanyagatwa na walio bara ndio Wandengereko. Wenyeji wa visiwani wanajishughulisha sana na uvuvi, kilimo cha mnazi na kupika chumvi, Wandengereko wanajishughulisha sana na mazao ya vyakula kama vile mpunga, mahindi n.k.
Mkoa wa Pwani una wilaya nane (katika mabano idadi ya wakazi wakati wa sensa ya mwaka 2022 ):
Mkoa huu una jumla ya majimbo ya uchaguzi yanayofikia (9) ambayo yanajumuisha Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kibaha Vijijini, Kibiti, Kisarawe, Mafia, Mkuranga na Rufiji
Mkoa huu ni maarufu sana kwa shughuli za kiutalii hususani katika mji wa Bagamoyo.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mkoa wa Pwani, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.