Harmonize: Msanii wa Tanzania na mjasiriamali wa muziki

Harmonize (kwa jina lake halisi Rajab Abdul Kahali; mara kadhaa hujiita Konde Boy; amezaliwa Chitoholi, mkoa wa Mtwara ni mwimbaji na mtunzi wa muziki kutoka Tanzania.

Harmonize
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Rajab Abdul Kahali
Pia anajulikana kama Harmonize
Asili yake Mtwara,Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava,Afro Pop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi
Ala Piano, sauti
Miaka ya kazi 2011–mpaka sasa
Studio KONDE MUSIC WORLDWIDE
Ame/Wameshirikiana na Rayvanny, Diamond Platnumz
Tovuti Tovuti Halisi

Alianza kuvuma kwa kibao chake cha kwanza "Aiyola" (2015), Bado (2016), Matatizo (2016) na baadaye akatoa nyimbo na msanii mwenzie kutoka lebo moja ya WCB (Wasafi Classic Baby) ambaye ni Diamond Platnumz.

Aliamua kuhama WCB na kuanzisha lebo yake Konde Music Worldwide [1].

Kwa ngwaru ni wimbo ambao ulibamba karibia maeneo yote ya Afrika ya Mashariki akatoa kibao kingine kiitwacho inama nyimbo ambayo aliimba na msanii kutoka nje ya Tanzania ambaye anaitwa burna na diamond Platnumz alikuwepo kwenye huo wimbo. Sasa hivi anatamba na kibao kiitwacho Never Give Up, wimbo ambao unaelezea historia ya maisha yake kuanzia alivyo kuwa na maisha magumu sana. Harmonize anasimamiwa na Joel Joseph au kwa jina lingine Mr Puaz. Kwa sasa msanii huyu yuko peke yake baada ya kujitoa WCB pia amekuwa akitoa ngoma kama vile uno ambayo imepata umaarufu mkubwa na kuwa gumzo yani number one on trending. Pia kwa sasa ameachia kazi yake ya pili iitayo kushoto kulia ambayo amesikika akimtaja Diamond ambapo ni kwa mara ya pili.

Maisha ya Awali

Harmonize ana asili ya Mtwara. Alisoma katika shule ya sekondari Mkundi iliyopo mjini Mtwara. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, Harmonize alielekea Dar es Salaam ambako alijipatia riziki yake ya kila siku.

Harmonize mwanzoni alibeba maji ili kupata tonge la chakula, pia alikuwa akiuza kahawa kwa wafanyabiashara wengine na wakazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kabla ya sauti yake kutambulika mitaani. Kisha kuchukuliwa na lebo ya Diamond Platnumz ijulikanayo kama WCB. Kwa sasa ameamua kujiondoa katika lebo hiyo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Alianza kujihusisha na muziki mnamo mwaka 2011 ambapo alitoa nyimbo mbalimbali lakini hazikuweza kupata umaarufu mkubwa mpaka pale ambapo alikutana na Diamond Platinumz mnamo mwaka 2015 na kuanza kufanya muziki pamoja naye.

Harmonize ndiye mwanamuziki aliyetoa albamu yenye nyimbo 18 akiwa amewashirikisha Yemi Alade wa Nigeria na albamu hiyo inaitwa Afro East.

Diskografia

Nambari Mada ya wimbo Mwaka
1. Aiyola 2015
2. Bado ft Diamond Platnumz 2016
3. Matatizo 2017
4. Happy Birthday 2017
5. Shula 2017
6. Sina 2017
7. Niambie 2017
8. Dont go 2017
9. Nishachoka 2017
10. Nakupenda 2017
11. Kwa ngwaru ft. Diamond platnumz 2018
12. Dm chick 2018
13. Atarudi 2018
14. Paranawe ft. Rayvanny 2018
15. Niteke 2019
16. Show me what you gat ft. Yemi Alade 2019
17. Kainama ft. Diamond Platnumz na Burna boy 2019
18. Ndoenda 2019
19. Never give up 2019

|20. |Mdomo |2021

Tuzo na teuzi

Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo
2016 Bado Ft Diamond Platnumz WatsUp TV Tuzo la Video Bora zaidi ya Mwimbaji Chipukizi Ameshinda
Yeye Mwenyewe African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kwa Mwimbaji Chipukizi Ameshinda
African Entertainment Awards (AEAUSA) kwa Msanii Chipukizi Bora zaidi Ameshinda

2022 kilimanjaro Tanzania music arward= best male artist

Tanbihi

Harmonize: Maisha ya Awali, Diskografia, Tuzo na teuzi  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Harmonize kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Harmonize Maisha ya AwaliHarmonize DiskografiaHarmonize Tuzo na teuziHarmonize TanbihiHarmonizeJinaMkoa wa MtwaraMtunziMuzikiMwimbajiTanzania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Reli ya TanganyikaKanisa KatolikiHifadhi ya SerengetiYouTubeVichekeshoMkondo wa umemeTarakilishiZiwa ViktoriaCristiano RonaldoBendera ya KenyaSikioMkoa wa RuvumaKilimoWachaggaJapaniMkoa wa SimiyuKitufeSheriaMkoa wa ShinyangaAnthropolojiaKishazi tegemeziKarafuuOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaMaudhuiFasihiHafidh AmeirTajikistanMsalaba wa YesuUaMkoa wa KataviLady Jay DeeUnyanyasaji wa kijinsiaWayahudiNabii IsayaMkoa wa MtwaraBarabaraTwigaSitiariAsiaVita Kuu ya Pili ya DuniaSadakaOrodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMkoa wa Dar es SalaamLahajaTabainiWhatsAppHoma ya matumboVitenzi vishirikishi vikamilifuHarmonizeBiblia ya KikristoTiba asilia ya homoniUandishi wa inshaKenyaKomaPijini na krioliKisononoWashambaaJumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta dunianiMachweoFasihi andishiHifadhi ya NgorongoroWiki FoundationAslay Isihaka NassoroInjili ya LukaVivumishi vya pekeeKilimanjaro (Volkeno)Jacob StephenAfrika Mashariki 1800-1845BungeMtandao wa kompyutaBiasharaMichezo ya jukwaaniKiambishiKatekisimu ya Kanisa KatolikiWaluguruOrodha ya nchi za Afrika🡆 More