Pumu

Pumu (kwa Kiingereza asthma) ni ugonjwa wa kudumu wa uvimbe wa makoromeo ulio na sifa za dalili zinazobadilika na kujirudia, hewa kuzibwa na bronkospasimu.

Pumu
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyPulmonology, immunology Edit this on Wikidata
ICD-10J45.
ICD-9493
OMIM600807
DiseasesDB1006
MedlinePlus000141
eMedicinearticle/806890
MeSHD001249

Dalili ni pamoja na kukoroma, kukohoa, kujikaza kwa kifua, na kukosa pumzi.

Inashukiwa kusababishwa na jenetikia pamoja na hali ya mazingira. Kwa kawaida huzingatia mtindo wa dalili, matokeo baada ya matibabu ya muda, na spirometri. Imeainishwa kulingana na idadi ya dalili, wingi wa kupumua kwa nguvu (FEV1), na idadi ya juu ya kupumua. Inaweza pia kuainishwa kama atopiki (ya nje) au isiyo ya atopiki (ya ndani) ambapo atopi inarejelea maelekezo ya kuanzia type 1 hypersensitivity.

Dalili kali hutibiwa na Beta2-adrenergic agonist ya kuvuta (kama vile salbutamol) na kotikosteroidi za mdomo. Katika visa vikali kotikosteroidi za mishipa, salfeti ya magnesia na ulazwaji hospitalini unaweza kuhitajika.

Dalili zinaweza kuzuiwa kwa kujiepusha na visababishi, kama vile alajeni na vitu vinavyowasha, na kwa kutumia kotikosteroidi za kuvuta. Beta-adrenoceptor agonist zinazofanya kazi kwa muda mrefu (LABA) au leukotriene antagonist inaweza kutumika kando ya kotikosteroidi iwapo dalili za ugonjwa hazitadhibitiwa.

Uenezi umeongezeka tangu mwaka 1970. Kufikia 2011, watu milioni 235–300 walikuwa wameathiriwa ulimwenguni, ikijumuisha takribani vifo 250,000.

Ishara na dalili

Ugonjwa huu huwa na visa vya kujirudia vya kukoroma, upungufu wa pumzi, kujikaza kwa kifua, na kukohoa. Makohozi yanaweza kutoka mapafuni, lakini kwa kawaida huwa vigumu kuyatoa. Ukiendelea kupata nafuu yanaweza kutokea uchafu kama usaha kwa sababu ya kiwango cha juu cha seli nyeupe za damu ziitwazo esinofili. Dalili huwa mbaya zaidi usiku na mapema asubuhi au kwa athari ya mazoezi au baridi. Baadhi ya watu wenye ugonjwa huu ni nadra kwa kawaida kuhisi dalili, kwa athari za visababishi, ilhali wengine wanaweza kuwa na dalili zinazotambulika na zinazoendelea.

Hali zinazohusiana

Hali kadhaa za afya hutokea mara nyingi kwa walio na pumu ikiwa ni pamoja na: ugonjwa wa ucheuaji wa astro-esophajeli (GERD), rhinosinusitisi, na apnea inayosumbua wakati wa kulala. Matatizo ya kisaikolojia huwa ya kawaida na wasiwasi unaotokea kati ya asilimia 16–52 na tatizo la sununu katika asilimia 14–41. Hata hivyo, haijulikani iwapo ugonjwa huu husababisha matatizo ya kisaikolojia au iwapo matatizo ya kisaikolojia husababisha pumu.

Visababishi

Ugonjwa huu husababishwa na mchanganyiko wa mwingiliano mgumu na usioeleweka kikamilifu wa kimazingira na kijenetiki. Masuala haya huathiri ukali wake na matokeo yake baada ya matibabu. Inaaminika kuwa ongezeko la hivi karibuni la ugonjwa huu unasababishwa na kubadilika kwa masuala ya kiepijenetiki (kuridhika kando na yanayohusiana na Mfuatano wa DNA) na kubadilika kwa mazingira ya kuishi.

Mazingira

Masuala mengi ya kimazingira yamehusishwa na kutokea kwa pumu na maumivu ikiwa ni pamoja na: alejeni, kuchafuka kwa hewa na kemikali zingine za kimazingira. Kuvuta sigara wakati wa ujauzito na baada ya kuzaa huhusishwa na hatari kuu za dalili zinazofanana na za pumu. aina ya hewa, kutoka kwa magari barabarani au ngazi za juu za ozoni , zimehusishwa na kutokea kwa pumu na ongezeko la ukali wake. Hatari ya mchanganyiko wa ogani fukivu inaweza kuchochea kutokea kwa pumu; uhatarisho wa fomadeidi, kwa mfano, huwa na ushirikiano halisi. Pia, fithaleti katika PVC huhusishwa na ugonjwa huu kwa watoto na watu wazima kama ilivyo kwa viwango vya juu vya hatari ya endotoksini.

Pumu huhusishwa na uhatarisho wa alejeni za ndani ya nyumba. Alejeni za kawaida za ndani ni pamoja na: wadudu wa vumbi, mende, magamba ya wanyama, na kuvu. Juhudi za kupunguza wadudu wa vumbi zimepatikana kutofaa. Maambukizi fulani yanayohusiana na upumuaji yanaweza kuongeza hatari ya kupata pumu yanapopatikana utotoni kama vile:virusi vya sinksia vya upumuaji na virusi vya rhino. Hata hivyo maambukizi mengine yanaweza kupunguza hatari.

Nadharia ya usafi

Nadharia ya usafi hujaribu kuelezea viwango vya kuongezeka kwa pumu kote ulimwenguni kama matokeo ya moja kwa moja na yasiyokusudiwa ya kupungua kwa hatari wakati wa utotoni, hadi kwa bakteria na virusi visivyo na maambukizi. Imependekezwa kuwa kupungua kwa hatari ya bakteria na virusi sehemu yake ni kwa sababu ya kuongezeka kwa usafi na kupungua kwa ukubwa wa familia katika jamii za kisasa. Ushahidi unaodhibitisha nadharia ya usafi ni pamoja na viwango vya chini vya pumu kwa mashamba na maboma yaliyo na wanyama vipenzi.

Matumizi ya antibiotiki mapema maishani yamehusishwa na kutokea kwa pumu. Pia, kuzaa kwa njia ya operesheni ya Siza huhusishwa na ongezeko la hatari (lililokadiriwa kwa asilimia 20–80) ya pumu—ongezeko hili la hatari linahusishwa na ukosefu wa kudhibiti bora wa bakteria ambao mtoto mchanga angepata kutoka kwa njia inayopitia kwenye njia ya uzazi. Kuna uhusiano kati ya pumu na kiwango cha utajiri.

Jenetikia

CD14-endotoxin interaction based on CD14 SNP C-159T
Endotoxin levels CC genotype TT genotype
High exposure Low risk High risk
Low exposure High risk Low risk

Historia ya familia ni suala la hatari huku jeni nyingi tofauti zikihusishwa. Iwapo mmoja wa mapacha ataathiriwa, uwezekano wa mwingine kuwa na ugonjwa ni takriban asilimia 25. Kufikia mwisho wa 2005, jeni zilikuwa zimehusishwa na pumu katika idadi sita au zaidi za watu zilizotengana ikiwa ni pamoja na:GSTM1, IL10,CTLA-4, SPINK5,LTC4S, IL4R na ADAM33 kati ya zingine. Nyingi za jeni hizi zinahusiana na mfumo wa kingamwili au urekebishaji wa inflamesheni. Hata kati ya orodha ya jeni zilizodhibitishwa na uchunguzi uliorudiwa, matokeo hayajawa sawa kati ya idadi zote za watu zilizotathminiwa. Mwaka wa 2006 zaidi ya jeni 100 zilihusishwa na pumu katika uchunguzi wa muungano wa jeni moja pekee; mengi yanaendelea kutambuliwa.

Baadhi ya tofauti ya jenetikia unaweza kusababisha ugonjwa unapounganishwa na hatari ya kimazingira. Kwa mfano upolimofi moja ya nunukliotaidi katika eneo la CD14 na hatari ya endotoksini (zao la bakteria). Hatari ya endotoksini unaweza kupatikana kutoka kwa vyanzo kadhaa vya kimazingira ikiwa ni pamoja na moshi wa tobako, mbwa na mashamba. Hatari ya pumu, kisha husababishwa na jenetiki ya mtu na kiwango cha hatari ya endotoksini.

Hali ya tiba

Seti ya kizema ya atopi, aleji ya mafua na pumu huitwa atopi. Suala la hatari kuu zaidi la kupata ugonjwa ni historia ya ugonjwa wa atopi; huku pumu ikitokea kwa kiwango cha juu kwa walio na kizema au mafua ya mzio. Ugonjwa huu umehusishwa na Churg–Strauss syndrome, ugonjwa wa kipekee wa kingamwili na vaskulitisi. Watu binafsi walio na aina fulani za utikaria pia wanaweza kuhisi dalili za pumu.

Kuna uhusiano kati ya unene na hatari ya ugonjwa huku zikiwa zimeongezeka miaka iliyopita hivi karibuni. Masuala kadhaa yanaweza kusababisha ikiwa ni pamoja na kupungua kwa utendakazi wa upumuo kwa sababu ya ongezeko la mafuta na hasa kwa kuwa tishu ya adiposi husababisha hali ya pro-inflamesheni.

Dawa za Beta blocker kama vile propranolol zinaweza kusababisha ugonjwa kwa walio na uwepesi wa kuipata. Cardioselective beta-blockers, hata hivyo, huonekana kuwa salama kwa walio na ugonjwa mdogo au wa kiasi. Dawa zingine zinazoweza kusababisha matatizo ni ASA, NSAID, na vizuizi vya enzaimu anjiotensini-badilishi.

Ongezeko

Baadhi ya watu huwa na pumu tulivu kwa majuma au miezi kisha kuwa kali kwa ghafla. Watu tofauti huathirika kwa njia tofauti na masuala mbalimbali. Watu wengi binafsi wanaweza kupata ongezeko kali kutokana na baadhi ya maajenti sababishi.

Visababishi vya kinyumbani vya ugonjwa huu ni pamoja na vumbi, magamba ya mnyama (hasa manyoya ya paka na mbwa), mende alejeni na kuvu. marashi ni kisababishi cha kawaida cha mashambulizi kali kwa kina mama na watoto. Ambukizo la virusi na bakteria la trakti ya juu ya kupumua unaweza kuongeza ugonjwa. Mfadhaiko wa kisaikolojia mfadhaiko unaweza kuzidisha dalili—inakisiwa kuwa mfadhaiko hubadilisha mfumo wa kingamwili na hivyo huongeza athari ya inflamesheni ya njia ya hewa kutokana na alejeni na vitu ambavyo huwasha.

Pathofisiolojia

Pumu 
Kizuizi cha mwanya wa bronkioli kutoka mucoid exudate, goblet cell metaplasia, na epitheliumu utando msingi unaovimba kwa mtu aliye na pumu.

Pumu husababishwa na uvimbe kwa njia za hewa ikifuatiwa na mikazo katika eneo hilo msuli mdogo. Hii pamoja na visababishi vingine husababisha maumivu yanayotokana na njia ya hewa iliyonyembamba na dalili za hali ya juu za kukoroma. Uwembamba unaweza kurudi hali yake ya kawaida bila matibabu Mara kwa mara njia za hewa hujibadilisha. Mabadiliko ya njia za hewa ni pamoja na ongezeko kwa esinofili na kunenepa kwa lamina lililofanana na neti. Msuli wa njia za hewa inaweza kuwa kubwa kwa ukali na kuongezeka kwa idadi ya tezi ya miukosi. Aina zingine za seli zilizohusika ni pamoja na: T lymphocytes, macrophages, na nutrofili. Pia kunaweza kuwa na vijenzi vya mfumo wa kinga pamoja na: cytokines, chemokines, histamine, na leukotrienes miongoni mwa zingine.

Utambuzi

Pumu umetambulika vizuri, ilhali hakuna ufafanuzi hata moja ulioidhinishwa. Inafafanuliwa na Uvumbuzi wa Kidunia wa Pumu kama "ulemavu mkali wa inflamesheni katika njia za hewa ambapo seli mingi na elementi za seli huwa na jukumu. Inflamesheni kali inahusishwa na mwitikio uliozidi wa njia ya hewa zinazosababisha matukio ya kukoroma, kushindwa kupumua, mikazo kifuani na kukohoa hasa usiku au asubuhi na mapema. Matukio haya kwa kawaida yanahusiana na kutapakaa kwa hewa mwilini lakini mtiririko wa hewa uliozuiwa ambao unabadilika kwa pafu ambayo mara kwa mara inaweza kurudi kwa hali ya kawaida bila matibabu au na matibabu".

Kwa sasa hakuna uchunguzi maalum na utambuzi unaofanana hasa uliokatika muundo wa dalili na mwitikio kwa tiba muda unapoendelea. Utambuzi unapaswa kushukiwa ikiwa kuna: ukoromaji unaotokea mara kwa mara, kukohoa au kupumua kwa ugumu na hizi dalili hutokea au kuzidi kwa sababu ya mazoezi, maambukizi ya virusi, alejeni au hewa chafu. Kisha Spirometry hutumika kuthibitisha utambuzi. Utambuzi kwa watoto waliochini ya miaka sita ni vigumu kwa sababu ni wadogo kufanyiwa spirometry.

Spirometry

Spirometry inapendekezwa ili isaidie utambuzi na udhibiti. Hii ndio uchunguzi bora wa pumu. Ikiwa FEV1 kilichopimwa na mbinu hii kitakuwa bora na zaidi ya asilimia 12 kufuatiliwa na utoaji wa kipanua bronkasi kama vile sabutamoli, husaidia kwa utambuzi. Hata hivyo inaweza kuwa sawa kwa walio na historia ya ugonjwa isiyokali, isiyojitokeza. Kiwango cha hewa mtu anaweza kuvuta kwa pumzi moja inaweza kusaidia kutofautisha pumu COPD. Ni muhimu kufuatilia spirometry kila mwaka moja au mbili ili kufuatilia jinsi ugonjwa unavyodhibitiwa.

Njia nyingine

Kipimo cha tatizo la methacholine kinahusisha kuvuta hewa ya kuongeza viwango vya dutu vinavyosababisha njia ya hewa kuwa nyembamba katika eneo linalochangia kupata magonjwa. Ikiwa hakuna dalili inamaanisha hana ugonjwa; ikiwa ana dalili, hata hivyo, si ya ugonjwa hasa.

Ushahidi mwingine unaochangia ni: tofauti ya asilimia ≥20 kwa kiwango cha mwisho cha kupumua angalau siku tatu kwa wiki kwa wiki mbili, uboreshaji kwa asilimia ≥20 ya kiwango cha kupumua ukifuatiliwa na matibabu ya sabutamoli, kotikosteroidi ya kuvuta au prinisoni, au upungufu wa asilimia ≥20 ya kifaa cha kupima hewa kutoka kwa mapafu ikifuatiliwa na hatari ya kisababishi. Kipimo cha kiwango cha juu cha kupumua hubadilika zaidi kuliko ya spirometry, hata hivyo, haijakubaliwa kwa utambuzi wa mara kwa mara. Inaweza kuwa ya manufaa ya kujitathmini kila siku kwa wale walio na ugonjwa uliokali kiasi hadi kwa iliyokali na kutathmini matokeo yanayofaa kwa matibabu mapya. Inaweza pia kuwa ya manufaa ya kuongoza kwa matibabu kwa walio na hali ya kuongezeka kwa ukali wa ugonjwa.

Uainishaji

Clinical classification (≥ 12 years old)
Severity Symptom frequency Night time symptoms %FEV1 of predicted FEV1 Variability SABA use
Intermittent ≤2/week ≤2/month ≥80% <20% ≤2 days/week
Mild persistent >2/week 3–4/month ≥80% 20–30% >2 days/week
Moderate persistent Daily >1/week 60–80% >30% daily
Severe persistent Continuously Frequent (7×/week) <60% >30% ≥twice/day

Ugonjwa huu huainishwa kulingana na dalili inavyojitokeza mara kwa mara, kutoka kwa pumzi inayotolewa nje (FEV1), na kiwango cha mwisho cha kupumua. Pumu inaweza kuainishwa kama atopi (iliyo ya nje) au isiyo ya atopi (iliyo ya ndani), kwa kuzingatia iwapo dalili zimechochewa na alejeni (atopi) au la (zisizo za atopi). Pumu unapoainishwa kulingana na ukali, kwa sasa hakuna mbinu halisi ya kuainisha vikundi vidogo mbalimbali vya ugonjwa huu zaidi ya mfumo huu. Kutafuta njia za kutambua vikundi vidogo vinavyoitikia vyema kwa aina tofauti za matibabu ni lengo muhimu la utafiti wa pumu.

Ingawa pumu ni hali kali pingamizi, haichukuliwi kama sehemu ya ugonjwa kali unaopinga mapafu kwa kuwa jina hili linahusu mchanganyiko wa magonjwa zisizoweza kurudi katika hali iliyosawa kama vile bronkektasisi,bronkitisi kali, na emphysema. Tofauti na magonjwa haya, kizuizi cha njia ya hewa huweza kurudi katika hali yake ya kawaida; hata hivyo, isipotibiwa, inflamesheni kali kutokana na pumu huweza kusababisha mapafu kuwa na kizuizi kisichorudi kwa hali yake ya kawaida kwa sababu ya njia ya hewa kupata muundo mwingine. Tofauti na emphysema, ugonjwa huu huathiri bronkia, sio alveoli.

Kuzidi kwa pumu

Severity of an acute exacerbation
Near-fatal High PaCO2 and/or requiring mechanical ventilation
Life threatening
(any one of)
Clinical signs Measurements
Altered level of consciousness Peak flow< 33%
Exhaustion Oxygen saturation< 92%
Arrhythmia PaO2< 8 kPa
Low blood pressure "Normal" PaCO2
Cyanosis
Silent chest
Poor respiratory effort
Acute severe
(any one of)
Peak flow 33–50%
Respiratory rate ≥ 25 breaths per minute
Heart rate ≥ 110 beats per minute
Unable to complete sentences in one breath
Moderate Worsening symptoms
Peak flow 50–80% best or predicted
No features of acute severe asthma

Ugonjwa kali uliozidi huitwa shambulizi la pumu. Dalili zinazotambulika ni upungufu wa hewa, ukorotaji, na kujikaza kwa kifua. Wakati hizi ni dalili za kwanza za ugonjwa, baadhi ya watu huonyesha kwa kukohoa, na katika hali kali, mwendo wa kupumua unaweza kuwa umeharibika sana kiasi kwamba ukoromaji hausikiki.

Dalili zinzazotokea wakati wa shambulizi la ugonjwa ni pamoja na matumizi zinazosaidia misuli za kupumua (sternocleidomastoid na misuli ya scalene za shingo), kunaweza kuwa na mpwito wa moyo wa kifumbo (mpwito uliodhaifu wakati wa kuvuta hewa na ulio na nguvu wakati wa kutoa hewa), na kuvimba kwa kifua. rangi ya bluu ya ngozi na kucha inaweza kutokea kutokana na ukosefu wa oksijeni.

Katika hali ya maumivu usio kali kiwango cha mwisho cha kupumua ni ≥200 ya lita moja kwa dakika au asilimia ≥50 ya utabiri uliobora. Wastani wake unafasiliwa kama kati ya 80 na 200 ya lita moja kwa dakika au asilimia 20 na 50 ya utabiri uliobora bali iliokali inafasiliwa kama ≤ 80 ya lita kwa dakika au asilimia ≤25 ya utabiri uliobora.

Pumu iliyo kali mno, ulioitwa hali ya kuwa na pumu kali mbeleni, na inayoendelea kwa muda mrefu, ni ugonjwa kali uliozidi ambao hautibii na matibabu ya kawaida ya kipanua koromeo na kotikosteroidi. Nusu ya hali hizi zimesababishwa na maambukizi kutoka kwa mengine yaliyosababishwa na alejeni, hewa chafu, ukosefu wa dawa au kuzitumia kwa njia isiyofaa.

Pumu ya brittle ni aina ya ugonjwa unaotambuliwa na mashambulizi makali yanayorudi. Aina ya kwanza ya ugonjwa wa brittle ni ugonjwa ulio tofauti na mtiririko wa upeo mpana, licha ya makali ya dawa. Aina ya pili ya ugonjwa wa brittle ni ugonjwa ulio na usuli uliothibitiwa kwa njia inayofaa na ukali wa ghafla.

Yanayosababisha na mazoezi

Zoezi linaweza kusababisha kuminya bronkasi kwa wote walio na wasio kuwa na ugonjwa. Hutokea kwa watu wengi walio na pumu na hadi asilimia 20 ya watu wasio kuwa na ugonjwa. Hutokea mara nyingi kwa wanariadha wa tabaka la juu, kwa viwango vinavyobadilika kutoka asilimia 3 kwa wanaoshiriki katika mashindano ya bobsled hadi asilimia 50 kwa wanariadha wa baiskeli na asilimia 60 kwa cross-country skiing. Ingawa inaweza kutokea katika hali yoyote ya hewa ni ya kawaida zaidi wakati hewa ni kavu na baridi. Beta2-agonists ya kuvuta inaonekana kuwa haileti mabadiliko katika matokeo ya wanariadha wasiokuwa na pumu hata hivyo dozi za kumeza zinaweza kuboresha uvumilivu na nguvu.

Kazini

Pumu unaotokea (au kuzidishwa na) mazingira ya kazini, hurejelewa kama magonjwa ya kazini. Hata hivyo hali nyingi haziripotiwi au kutambuliwa. Inakadiriwa kuwa asilimia 5-25 ya ugonjwa huu kwa watu wazima huhusiana na mahali pa kazi. Maajenti karibu mia moja wamehusishwa na ya kawaida ikiwa: isocyanates, nafaka na uchafu wa mbao, colophony, soldering flux, ulimbo wa mpira, wanyama, na aldehydes. Uajiri uliohusishwa na hatari kubwa ya matatizo inajumuisha: wale ambao wanajipaka rangi, waokaji na watengenezao chakula, wauguzi, wafanyikazi wa kemikali, wanaofanyakazi na wanyama, wati weko, watengenezaji nywele na wafanyikazi wa mabao.

Utambuzi tofauti

Hali zingine zinaweza kusababisha dalili zinazofanana na za pumu. Kwa watoto, magonjwa mengine ya njia ya hewa kama vile mzio wa pua na sinositisi zinapaswa kuangiliwa pia kama visababishi vinavyofunga njia ya hewa ikijumuisha: kitu kigeni mwilini, tracheal stenosis au laryngotracheomalacia, vizingo vya utomvu, hurefushwa Tezi au uzito wa shingo. Kwa watu wazima, COPD, kutofanya kazi kwa moyo, uzito wa hewa kupita, vile vile dawa za kukomesha athiri ya ACE zinapaswa kuangaliwa. Kwa watu wote kutofanya kazi kwa mshipi wa sauti inaweza kutokea pia.

Pumu zibifu wa kudumu inaweza kuwa na ugonjwa huu na inaweza kutokea kama tatizo la kudumu. Katika umri wa miaka 65 watu wengi walio na ugonjwa wa njia ya hewa iliyofunganga watakuwa na pumu na COPD. Kati hali hii, COPD inaweza kutofautishwa kwa nutrofili nyingi katika njia ya hewa, inayoongezwa na ukubwa wa ukuta, na kuongezeka kwa msuli mdogo bronkia. Hata hivyo, kiwango hiki cha kuchunguza haiwezi kutekelezwa kwa sababu COPD na pumu huwa na kanuni sawa za usimamizi: kotikosteroidi, kuwepo kwa beta agonists, na hatua za kuacha kuvuta sigara. Hukaribiana na pumu kwa dalili, huhusiana na uvutaji wa sigara, umri mkubwa, kutobadilika kwa dalili baada ya kuweka kipanua bronkasi, na upungufu wa kuwepo kwa atopi katika familia.

Uzuiaji

Ushahidi wa kufanya kazi kwa mikakati ya kuzuia kutokea kwa ugonjwa ni finyu. Baadhi huonyesha matumaini ikijumuisha: kuepekuna na sehemu zilizo na moshi katika uterasi na baada ya kuzaa, unyonyeshaji, na ongezeko la utunzaji au familia kubwa lakini hakuna hata moja inayopendekezwa kwa dalili hii. Kufichuliwa kwa mnyama mapema inaweza kusaidia. Matokeo ya ufichuzi kwa wanyma wakati mwingine inashida na inapendekezwa tu wanyma watolewe nyumbani ikiwa binadamu ana dalili za aleji ya mnyama huyo. Upangaji mlo wakati wa ujauzito au unyonyeshaji haibainishi kama njia nzuri na hivyo haipendekezwi. Utoaji au upunguzaji wa vitu vilivyo hatari kwa watu kazini inaweza kuwa salama.

Udhibiti

Ilhali hakuna matibabu ya pumu, dalili zinaweza kuboreshwa. Mpango maalum, ulioboreshwa kwa kufuatilia na kudhibiti dalili inapaswa kutengenezwa. Mpango huu unapaswa kujumuisha upunguzaji wa alejeni, kwa uchunguzi wa kutathmini ukali, na matumizi ya dawa. Mpango wa matibabu unapaswa kuandikwa chini na kuwashauri kuhusu marekebisho ya matibabu kulingana na mabadiliko ya dalili.

Njia mwafaka ya kutibu ni kutambua visababishi, kama vile uvutaji wa sigara, wanyama, au aspirin, na kuepukana nao. Ikiwa haiwezekani, matumizi ya dawa utahitajika. Dawa ya matibabu yanachaguliwa kwa kuzingatia, vitu vingi, ukali wa ugonjwa na marudio ya dalili. Matibabu maalum ya pumu huanishwa kwa jumla katika kategoria zinazojitokeza na zinazochukua muda.

Vipanua bronkasi vinapendekezwa kwa dalili za muda mfupi. Matibabu mengine hayahitajiki, kwa wanaokuwa na maumivu kila mara. Ikiwa ugonjwa itaendelea kudumu (kuwa mgonjwa zaidi ya mara mbili kwa wiki moja), dozi ndogo ya kuvuta ya kotikosteroidi au nyingine, ya kunywa leukotriene antagonist au mast cell stabilizer inapendekezwa. Kwa walio na maumivu kila siku, dozi kubwa ya kotikosteroidi ya kuvuta inatumiwa. Wakati wa maumivu, kotikosteroidi ya kumeza zinaongezwa kwa matibau haya.

Ubadilishaji wa mtindo wa maisha

Uepaji wa visababishi ni sehemu kuu ya kuboresha udhibiti na kuzuia kupatwa na ugonjwa. Visababishi vya kawaida sana ni pamoja na alejeni, moshi (tobako na vingine), uchafuzi wa hewa, vizuizi beta visivyo chaguzi, na chakula kilicho na salfeti. Uvutaji sigara na uvutaji moshi kutoka kwa anayevuta sigara(moshi wa mtu mwingine) unaweza kupunguza utendakazi wa dawa kama vile kotikosteroidi. Juhudi za kudhibiti wadudu wa vumbi, pamoja na kuchunja hewa, kemikali za kuua wadudu, kutumia kivuta vumbi, vitu vya kufunika godoro na njia zingine hazikuwa na mabadiliko kwa dalili za ugonjwa.

Dawa

Dawa zinazotumika kutibu pumu zimegawanywa mara mbili: zinazotuliza maumivu haraka kwa kutibu dalili kali; na za kudhibiti maumivu kwa muda mrefu ambazo huzuia ongezeko la ugonjwa.

    Zinazofanya kazi haraka
Pumu 
Sabutamoli kivutia dawa cha dozi kinachotumika kwa matibabu.
  • beta2-adrenajiki agonistibeta2-adrenosepta agonistsi (SABA), kama vile sabutamoli (albuterol USAN) ni matibabu ya kwanza ya dalili za ugonjwa.
  • Dawa za Anticholinergic kama vile bromidi ya ipratropiamu, hupeana faida zinapotumika pamoja na SABA kwa walio na dalili. Vipanuzi vya bronkasi visivyo na anticholinergic inaweza pia hutumika iwapo mtu hawezi kustahimili SABA.
  • Kipokezi cha adrenaji cha zamani, kisichochaguliwa sana adrenajiki agonistsi, kama vile epinephrine ya kuvuta huwa na matokeo sawa na yale ya SABA. Hazipendekezwi kwa sababu ya tatizo la kuchangamsha moyo.
    Udhibiti wa muda mrefu
Pumu 
Fluticasone propionate kivutia dawa kwa kawaida kinachotumika kwa udhibiti wa muda mrefu.
  • Kotikosteroidi huchukuliwa kama matibabu yanayofaa kwa udhibiti wa muda mrefu. Aina zinazovutwa hutumika isipokuwa kwa ugonjwa kali unaoendelea, ambapo kotikosteroidi za kumeza zitahitajika. Hupendekezwa kuwa aina za kuvutwa zitumike mara moja au mbili kwa siku, kulingana na ukali wa dalili.
  • Adrenosepta agonisti beta zinazofanya kazi kwa muda mrefu (LABA) kama vile salmeterol na formoterol zinaweza kuboresha udhibiti wa ugonjwa, angalau kwa watu wazima, zinapopeanwa pamoja na kotikosteroidi za kuvuta. Kwa watoto faida hii si hakika. Zinapotumika bila steroidi huongeza hatari ya athari na hata zikitumiwa na kotikosteroidi zinaweza kuongeza hatari kidogo.
  • Leukotriene antagonist (kama vile montelukast na zafirlukast) zinaweza kutumika kando na kotikosteroidi za kuvuta, pia pamoja na LABA. Dhibitisho hairuhusu matumizi katika ongezeko la ugonjwa. Kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano, therapi ya kuongeza baada ya kuvuta kotikosteroidi inapendekezwa.
  • Mast cell stabilizer (kama vile sodiamu kromolini) haitumiki badala ya kotokosteroidi.
    Njia za kupeana

Dawa hupeanwa kama kifaa cha kuvutia dawa (KKD) pamoja na kifaa cha kupeana dawa ya pumu au kama kivutia dawa cha poda. Kifaa kinachopeana dawa ni silinda ya plastiki ambayo huchanganya dawa na hewa, na kurahisisha kupata dozi kamili ya dawa. Nebulaiza inaweza kutumiwa. Nebulaiza na kifaa cha kutoa nafasi hufaa kwa walio na dalili, hata hivyo hakuna thibitisho kuamua iwapo kuna au hakuna tofauti kwa dalili kali.

    Athari

Matumizi ya muda mrefu ya kotikosteroidi ya kuvuta huwa na hatari ndogo ya athari. Hatari ni pamoja na kutokea kwa cataract na kurudi nyuma kidogo kwa akili.

Dawa nyingine

Pumu isipobadilika na dawa za kawaida, kuna aina zingine za chaguo zinazopatikana kwa udhibiti wa dharura na uzuizi wa milipuko. Kwa udhibiti wa dharura aina zingine za chaguo ni:

  • Oksijeni ili kutuliza haipoksia ikiwa viwango vya juu iko chini ya asilimia 92.
  • Salfeti ya magnesia matibabu ya mishipa ya ndani yameonyeshwa kusababisha athari ya kupanua bronkasi inapotumika pamoja na matibabu mengine katika mashambulizi makali ya ugonjwa.
  • Helioksi, mchanganyiko wa heli na oksijeni, unaweza kutumiwa kwa visa vikali visivyoonyesha mabadiliko kwa kutumia dawa.
  • Sabutamoli ya mishipa ya ndani haitetewi na dhibitisho linalopatikana na hivyo hutumika tu kwa visa vikali zaidi.
  • Methylxanthines (kama vile theophylline) wakati mmoja ilitumika kwa wingi, lakini haiongezi athari za beta-agonistsi. Matumizi yake kwa maumivu makali huwa na pingamizi.
  • Kitiaganzi kinachojitenga ketamini inaweza kutumiwa kinadharia iwapo intubesheni na uingizaji wa hewa utahitajika kwa watu wanaokaribia kuwa na tatizo la upumuo; hata hivyo, hakuna dibitisho kutoka kwa majaribio ya kliniki ili kudhibitisha hili.

Kwa walio na ugonjwa kali unaoendelea usiodhibitiwa na kotikosteroidi za kuvuta na LABAS themoplasti ya bronkasi inaweza kutumiwa. Huhusisha hupeanaji wa nishati joto kwa njia za hewa wakati wa mifululizo ya bronkoskopi. Ingawa inaweza kuongeza idadi ya maumivu katika miezi michache ya kwanza huonekana kupunguza idadi ambayo hufuata.Athari za kupita mwaka mmoja hazijulikani.

Dawa mbadala

Watu wengi, kama wale walio na matatizo ya muda mrefu, hutumia matibabu mbadala; uchunguzi unaonyesha kuwa takribani asilimia 50 hutumia baadhi ya therapi isiyo ya kawaida. Kuna data chache ya kudhibitisha utendakazi wa therapi hizi. Ushahidi hautoshi kudhibitisha matumizi ya vitamini C. Acupuncture haipendekezwi kwa matibabu maana hakuna ushahidi wa kudhibitisha matumizi yake. Kutia aioni kwa hewa haionyeshi ushahidi wa mabadiliko ya dalili au kusaidia utendakazi wa mapafu; hii ikitumika sawa kwa jenereta hasi na zisizo hasi.

"Therapi za mikono", ikiwa ni pamoja na osteopathi, kiropraktiki, fiziotherapi na therapi ya pumzi washawishi, wasio na ushahidi wa kudhibitisha matumizi kwa kutibu pumu. Mbinu ya Butyko ya kupumua ya kudhibiti upitishaji wa hewa nyingi inaweza kusababisha upungufu wa matumizi ya dawa hata hivyo haina athari yoyote kwa pafu. Hivyo kamati ya wastadi ilihisi kuwa ushahidi haukutosha kudhibitisha matumizi yake.

Prognosisi

Pumu 
Ulemavu-uliobadilisha miaka ya maisha kwa pumu kwa watu 100,000 mwaka wa 2004.
     no data      <100      100–150      150–200      200–250      250–300      300–350
     350–400      400–450      450–500      500–550      550–600      >600

Prognosi ya pumu ni nzuri, hasa kwa watoto walio na ugonjwa usio mkali. Vifo vimepungua katika miongo michache iliyopita kwa sababu ya utambuzi na uboreshaji wa utunzaji.

Ulimwenguni umesababisha ulemavu wa watu milioni 19.4  kufikia mwaka wa 2004 (milioni 16 wakiwa katika hali ya chini na ya kawaida katika nchi zinazoendelea). Kwa pumu uliotambuliwa wakati wa utotoni, nusu ya hali hizi hazitafanyiwa utambuzi baada ya mwongo mmoja. Upitishaji wa hewa hutengenezwa upya, lakini haijulikani ikiwa italeta faida au madhara. Matibabu ya mapema kwa kutumia kotikosteroidi inaonekana kuzuia au kusaidia kupunguza matumizi kwa pafu.

Epidemiolojia

Pumu 
Viwango vya pumu katika nchi tofauti ulimwenguni kufikia mwaka wa 2004.
     no data      <1%      1-2%      2-3%      3-4%      4-5%      5-6%
     6-7%      7-8%      8-10%      10-12.5%      12.5–15%      >15%

Kufikia mwaka wa 2011, watu milioni 235–300 ulimwenguni walikuwa wameathiriwa na ugonjwa huu, na karibu watu 250,000 hufa kila mwaka. Viwango vyao hutofautiana kati ya nchi zilizo na maambukizi kati ya asilimia 1 hadi 18. Zinapatikana sana katika zilizoendelea kuliko nchi zinazokuwa. Kuna viwango vya chini barani Asia, Ulaya Mashariki na Afrika. Katika nchi zilizoendelea ni kawaida kwa wale walio na shida ya kifedha unapolinganisha na nchi zinazokuwa inapatikana sana kwa walio na fedha. Sababu ya tofauti hizi haijulikani. Nchi zilizo na pato la chini wanajumulisha asilimia 80 ya vifo.

Ilhali ugonjwa huu unapatikana kwa wavulana mara mbili zaidi ya wasichana, ukali wa ugonjwa hutokea kwa viwango sawa. Katika utofautishaji, wanawake wana viwango vikubwa vya pumu kuliko wanaume na hupatikana sana kwa wachanga kuliko wakubwa.

Viwango vya ugonjwa huu ulimwenguni viliongezeka kwa kasi kati ya miaka ya 1960 na 2008 ikipitishwa kama shida kubwa katika afya ya umma kwanzia miaka ya 1970. Viwango vya ugonjwa havijabadilika tangu katikati ya miaka ya 1990 kukiwa na ongezeko katika nchi zinazoendelea. Pumu huathiri takriban asilimia 7 ya watu nchini Marekani na asilimia 5 nchini Uingereza. Kanada, Australia and Nyuzelandi vina viwango vya kati ya asilimia 14-15.

Historia

Pumu uligunduliwa kitambo nchini Misri na ulitibiwa kwa kunywa ubani mchanganyiko unaoitwa kyphi. Ulitajwa rasmi kama tatizo la upumuaji na Hippocrates mwaka 450 KK hivi, kutoka kwa neno la Kigriki kumaanisha "kuhema" ikiunda asili ya neno la kisasa. Mnamo 200 KK uliaminika kuhusiana kidogo na hisia.

Mwaka wa 1873, mmoja kati ya karatasi za kwanza za dawa za kisasa kuhusu taarifa zilijaribu kuelezea ugonjwa wa pathofisiolojia ilhali nyingine mwaka wa 1872 ilihitimisha kuwa ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa kupanguza kifua na chloroform liniment. Matibabu ya afya mwaka wa 1880, ilijumuisha matumizi ya sindano ya vena inayoitwa pilocarpin. Mnamo mwaka wa 1886, F.H. Bosworth alieleza uhusiano kati ya pumu na mafua ya mzio. epinefrini ulirejelewa mara ya kwanza mwaka wa 1905 katika matibabu ya pumu. Kotikosteroidi za kunywa zilianza kutumiwa miaka ya 1950 ilhali kotikosteroidi za kuvuta na beta agonist za kuchagua zilianza kutumika miaka ya 1960.

Kati ya miaka ya 19301950, ugonjwa huu ulijulikana kama "takatifu saba" maradhi ya saikosomatiki. Kisababishi chake kilichukuliwa kama saikolojia, na matibabu kuangaliwa kwa uchunguzi nafsia na matibabu mengine ya kuzungumza. Walivyofafanua wachanganuzi ukoromaji wa pumu jinsi mtoto alivyolilia mama yake, walibaini kuwa matibabu ya masumbuko ni muhimu kwa walio na pumu.

Tanbihi

Viungo vya nje

Tags:

Pumu Ishara na daliliPumu VisababishiPumu PathofisiolojiaPumu UtambuziPumu UzuiajiPumu UdhibitiPumu PrognosisiPumu EpidemiolojiaPumu HistoriaPumu TanbihiPumu Viungo vya njePumuDaliliHewaKiingerezaUgonjwaw:Asthma

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

SintaksiKata za Mkoa wa Dar es SalaamOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaMfupaMtandao wa kijamiiUtoaji mimbaKunguniMatumizi ya LughaJangwaKiimboKichochoMmeng'enyoTanganyika (ziwa)SarangaAbedi Amani KarumeAbrahamuJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaLongitudoMabiboMaajabu ya duniaUgonjwa wa kuharaMnyoo-matumbo MkubwaMuhammadOrodha ya Magavana wa TanganyikaFutiMkoa wa SongweMvuaMlo kamiliIsimujamiiShetaniTasifidaPopoKihusishiJohn MagufuliMaarifaMeta PlatformsHektariOrodha ya mito nchini TanzaniaUandishi wa barua ya simuSteven KanumbaWabena (Tanzania)UbunifuIsraeli ya KaleUhifadhi wa fasihi simuliziViwakilishi vya sifaUturukiKinyongaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaWazaramoSaida KaroliUzalendoUtamaduni wa KitanzaniaUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Hekalu la YerusalemuRwandaOmmy DimpozKipimajotoMbeziStadi za lughaKiwakilishi nafsiNgome ya YesuNomino za jumlaUaminifuVivumishi vya -a unganifuNdege (mnyama)MazingiraAfrikaBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiHifadhi ya mazingiraTwigaWakaguruVita vya KageraMkoa wa MaraMafua ya kawaidaNyangumi🡆 More