Meta Platforms, Inc. ni kampuni ya intaneti inayojulikana kwa kifupi chake Meta. Kabla ya mwaka 2021 ilifahamika kama Facebook, kampuni lililomilikiwa na Mark Zuckerberg pamoja na waanzilishi wengine na wafanyakazi wake. Makao makuu yako California, Marekani.
Tangu Februari 2012 kampuni ilianza kutoa hisa hadharani.
Pamoja na mtandao wa kijamii Facebook, Meta inamiliki huduma za Instagram, WhatsApp, Messenger na Meta Quest. Kwenye mwaka 2021 kampuni ya Meta ilipata asilimia 97.5 ya mapato yake kutokana na kuuza nafasi za matangazo yanayowekwa na kampuni nyingine kwenye kurasa za huduma zake.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Meta Platforms, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.