Mafua Ya Kawaida

Mafua ya kawaida (pia mafua ya kuku au mafua tu; kwa Kiingereza: common cold, nasopharyngitis, rhinopharyngitis), ni ugonjwa wa kuambukizwa unaoathiri sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji, hasa pua na shingo.

Mafua ya kawaida
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyFamily medicine, infectious diseases, otolaryngology Edit this on Wikidata
ICD-10J00.{{{3}}}
ICD-9460
DiseasesDB31088
MedlinePlus000678
eMedicinemed/2339
MeSHD003139

Dalili ni pamoja na kikohozi, utoaji kamasi puani (rhinorrhea), na homa. Dalili kwa kawaida hupotea baada ya siku saba hadi kumi, ingawa baadhi ya dalili zake zinaweza zikakaa hadi wiki tatu.

Mafua ya kawaida husababishwa na virusi mbalimbali; zaidi ya mia mbili zinajulikana kusababisha mafua ya kawaida. Virusi vya jamii ya rinovirusi (rhinovirus) ndivyo visababishi vikuu.

Maambukizo makali ya pua, mianzi ya pua, koo au zoloto (maambukizi ya sehemu ya juu ya njia ya hewa: URI au URTI) yanabainishwa na eneo la mwili ambalo limeathirika zaidi. Mafua ya kawaida yanaathiri pua, yanavimbisha kolomeo, koo, na yanavimbisha mianzi ya pua. Dalili zinatokana na mfumo wa kinga unaopambana na maambukizi, si kwa sababu ya uharibifu wa seli mwilini unaoletwa na virusi. Kuosha mikono ni njia ya msingi ya kuzuia maambukizi. Kuna ushahidi unaounga mkono uvaaji kitambaa usoni ni bora zaidi.

Hakuna tiba ya mafua ya kawaida, lakini dalili zinaweza kutibiwa. Ni ugonjwa unaoambukiza sana binadamu. Kwa kawaida watu wazima wanaambukizwa mara mbili au tatu kwa mwaka. Kwa kawaida watoto huwa wanapata mafua mara sita au mara kumi na mbili kwa mwaka. Ugonjwa huo umekuwa ukiambukiza binadamu tangu zamani.

Dalili na ishara

Dalili za kawaida za mafua ni pamoja na kikohozi, mafua, kuziba kwa pua, na koo linalouma. Dalili nyinginezo ni pamoja na kuumwa misuli (myalgia), kuwa mchovu, kuumwa na kichwa, na kupoteza hamu ya kula. Kuumwa koo huwa hali inayowapata karibia asilimia 40 ya watu. Kikohozi ni hali inayowapata asilimia 50 ya watu Kuumwa misuli hutokea kwa nusu ya watu. Homa si dalili ya kawaida inayowapata watu wazima, lakini ni kawaida kwa watoto wachanga, na watoto wadogo Kikohozi kinachosababishwa na mafua ya kawaida si kali sana ukilinganisha na kikohozi kinachosababishwa na homa ya mafua (influenza). Kikohozi na homa vinaonyesha dalili kubwa ya homa ya mafua kwa watu wazima Idadi kubwa ya virusi vinavyosababisha mafua ya kawaida, vinaweza visiwe na dalili yoyote Kamasi wakati wa kukohoa hupita katika njia ya hewa na kamasi na inaweza kutofautiana kwa rangi nyeupe hadi kuwa ya njano au kijani. Rangi ya kamasi haionyeshi kama ugonjwa huo umesababishwa na bakteria au na virusi.

Maendeleo ya ugonjwa

Mafua kwa kawaida huanza na uchovu, hali ya kusikia baridi, kupiga chafya, na maumivu ya kichwa. Dalili nyinginezo ni kama vile pua inayotoa kamasi na kikohozi huanza baada ya siku mbili au zaidi. Dalili huwa zinakuwa mbaya siku mbili au tatu baada ya kuambukizwa. Dalili hizo kwa kawaida huendelea kwa siku saba hadi siku kumi, lakini huweza kuendelea hadi wiki tatu

Visababishi

Virusi

Mafua Ya Kawaida 
Coronavirus ni kundi la virusi linalojulikana kusababisha mafua ya kawaida. Kimaumbile vina nuru, au taji kama inavyoonekana kwa darubini elektroniki.

Mafua ya kawaida yanaambukiza kirahisi kwa kupitia njia ya hewa. Virusi aina ya rhinovirus ndio vinavyosababisha asilimia 30 hadi 80 ya mafua ya kawaida. Virusi aina ya rhinovirus vina RNA ya familia ya Picornaviridae. Kuna aina 99 inayojulikana ya virusi katika familia hii ya virusi Virusi nyingine pia husababisha mafua ya kawaida. Coronavirus husababisha asilimi 10% hadi 15% ya mafua. Mafua (homa) husababisha 5% hadi 15% ya mafua Mafua mengine yanaweza kusababishwa na virusi vya binadamu vya parainfluenza, virusi vya binadamu vya njia ya hewa viitwavyo syncytial virusi aina ya adenoviruses, enterovirus, na metapneumovirus. Mara nyingi, huwa kuna zaidi ya aina moja ya virusi vinavyosababisha maambukizi Kawaida huwa kuna zaidi ya aina mia mbili ya virusi tofauti vinavyohusiana na homa.

Uenezi

Virusi vya mafua ya kawaida vinaenezwa kwa njia moja kati ya njia kuu mbili. Kujaza hewa mapafu au kumeza vitone vya hewa vyenye virusi. Au kugusa kamasi ya pua iliyoambukizwa au kugusa vitu vilivyoambukizwa Which method of transmitting the cold is most common has not been determined Virusi vinaweza kuishi muda mrefu katika mazingira hayo. Virusi vinaweza kusambaa kutoka mikononi hadi kwenye macho au pua ambapo maambukizi hutokea. Watu waliopo karibu wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa. Maambukizi kawaida hutokea mchana na shuleni kwa sababu watoto hucheza pamoja, hawana kinga ya kutosha na kuna upungufu wa usafi Maambukizi haya yanaletwa nyumbani kwa ndugu wengine wa familia Hakuna ushahidi wa kutosha kwamba mzunguko wa hewa ndani ya ndege za abiria ni njia ya maambukizi . Homa inayosababishwa na virusi aina ya rhinovirus huwa maambukizi yake ni makali katika siku tatu za mwanzo wa dalili. Baada ya muda huo hawaambukizi sana

Hali ya hewa

Tangu zamani mafua yanakisiwa kwamba yanaenezwa kwa mtu aliyepatwa na baridi kwa muda mrefu wakati wa mvua au wakati wa msimu wa baridi, na ndiyo maana yanaitwa mafua ya baridi Kuna mabishano kwamba wajibu wa mwili kuwa katika hali ya baridi unaleta hatari ya kupata mafua Baadhi ya virusi vinavyosababisha homa ya kawaida hujitokeza mara kwa mara wakati wa msimu wa baridi au mvua. Ingawa hii inaaminika kuwa ni kwa sababu watu wanakaa pamoja ndani ya nyumba kwa muda mrefu;. haswa watoto wanaorudi shuleni Hata hivyo, inaweza pia kuwa ni kwa sababu ya mabadiliko ya hewa ambayo yanarahisisha maambukizi Upungufu wa unyevu unaweza kuongeza viwango vya maambukizi kutokana na hewa kavu kuruhusu vitone vidogo kuenea kiurahisi kusambaza mbali zaidi na kukaa angani kwa muda mrefu

Maambukizo mengine

Kinga ya kikundi, ni kinga ambayo hutokea wakati kikundi kizima cha watu kina kinga ya mwili na maambukizi haswa baada ya kupata maambukizo awali.Hivyo watoto wana uwezo mkubwa wa kuambukizwa na maradhi yanayohusiana upumuaji na watu wazima wana uwezo mdogo wa kuambukizwa na maradhi yanayohusiana upumuaji Upungufu wa kinga pia unaongeza hatari ya kuambukizwa ugonjwa Ukosefu wa usingizi na lishe duni pia zinaleta hatari kubwa ya kuendeleza maambukizi yanayoletwa na rhinovirus. Hii inatokana na athari inayoletwa na virusi ya kupunguza kinga ya mwili

Pathofisiolojia

Mafua Ya Kawaida 
Mafua ya kawaida ni ugonjwa unaoathiri sehemu ya juu ya kupitisha hewa

Dalili za mafua ya kawaida zinaaminika kuwa zinajitokeza wakati kinga mwili ikipambana na virusi. Jinsi kinga mwili inavyopambana na virusi inategemea na aina ya virusi.Kwa mfano, ni kawaida rhinovirus kuenezwa kwa kugusana. Inajifunga katika vipokezi vya binadamu I viitwavyo CAM-1 receptor kwa njia isiojulikana na kusababisha kutolewa kwa vichochezi. Vichochezi hivyo ndivyo vinaleta dalili. Kwa kawaida haileti madhara puani Kwa upande mwingine, virusi vya njia ya hewa (RSV) vinaenezwa kwa kugusana na kwa vitone vinavyopeperuka hewani. Ni kisha vinazaana katika pua na koo kabla ya kuenea sehemu ya chini ya kupitisha hewa RSV inasababisha uharibifu wa ukuta wa pua. Virusi vya binadamu vya parainfluenza vinasababisha uvimbi wa pua, koo, na njia za hewa. Vikiathiri bomba la pumzi la watoto wadogo vinaweza kusababisha kifaduro, kikohozi cha sauti na shida ya kupumua. Hii ni kwa sababu njia ya hewa ya watoto inazidi kuwa ndogo.

Uaguzi

Tofauti ya maambukizi ya sehemu ya juu ya kupitisha hewa (URTIs) inatokana na eneo lenye dalili. Mafua ya kawaida yanaathiri pua, uvimbe wa koromeo, koo, na mkamba inayoathiri mapafu. Mafua ya kawaida husababisha uvimbe wa pua na aina tofauti ya uvimbe wa koo. Ni jambo la kawaida kujifanyia mwenyewe utambuzi. Kutengwa kwa virusi kunafanyika mara chache Kwa kawaida si rahisi kutambua aina ya virusi kwa kutizama dalili.

Uzuiaji

Njia bora ilyopo ya kuzuia mafua ya kawaida ni kupunguza uenezi wa virusi mwilini Hii ni pamoja na kunawa mikono na kuvaa vitambaa usoni. Katika mazingira ya huduma ya afya, magauni na glavu za kinga pia huvaliwa Kuwatenga watu walioathirika, si rahisi kwa sababu ugonjwa huo unaenea sana na dalili haisababishwi na kundi moja la virusi. Chanjo zimeonekana kuwa hazina uwezo mkubwa kwa sababu kuna aina nyingi ya virusi na virusi hubadilika kwa haraka Utengenezaji wa chanjo wenye uwezo mkubwa si rahisi

Kunawa mikono mara kwa mara kunapunguza maambukizi ya virusi ya mafua. Njia hii ni bora zaidi kwa watoto Haijulikani kama kutumia dawa za kuzuia virusi au bakteria wakati wa kuosha mikono ni njia bora zaidi. Kuvaa vitamba usoni ukiwa karibu ya watu walioathirika inaweza kuwa ni njia nzuri. Kuna ushahidi usiotosha unaokiri kwamba kuwa mbali zaidi kimwili au mbali na jamii kunapunguza maambukizi. Nyongeza ya zinki inaweza kusababisha upungufu wa idadi ya homa mtu anayopata Utaratibu wa kujiongezea vitamini C haupunguzi hatari au makali ya mafua. Inaelekea vitamini C hupunguza muda wa mafua.

Usimamizi

Mafua Ya Kawaida 
Hmizo la kumkimblia daktari dhidi ya mafua.

Kwa sasa hakuna dawa au tiba za mitishamba ambazo zimthibitiwa kwa kufupisha muda wa maambukizi. Tiba ni pamoja na kutoa tulizo ya ishara. Hii ni pamoja na kupata mapumziko ya kutosha, kunywa maji ili kudumisha maji, na kugogomoa na maji ya joto ya chumvi. Mengi ya faida kutoka kwa matibabu hata hivyo inahusishwa na athari ya kipozauongo.

Ya dalili

Matibabu ambayo husaidia kupunguza dalili ni pamoja na kitulizo rahisi cha maumivu (analgesics) na tiba ya kupunguza homa (antipyretics) kama vile ibuprofen na acetaminophen/paracetamol. Ushahidi haionyeshi kwamba dawa za kukohoa si fanisi zaidi kuliko dawa rahisi za kupunguza maumivu (analgesics). Madawa ya kukohoa pia haifai kwa matumizi kwa watoto kutokana na ukosefu wa ushahidi fanisi unaothibitisha na hatari kwa madhara. Katika mwaka 2009, Kanada ilizuia matumizi ya tiba ya kukohoa ya dukani na mafua kwa watoto wenye umri wa miaka sita na ndogo kutokana na shauku kuhusu hatari na faida ambazo hazijathibitishwa. Matumizi mabaya ya dextromethorphan (dawa ya kuuzwa dukani) imesababisha kupigwa marufuku katika nchi kadhaa.

Kwa watu wazima, dalili za mafua inaweza kupunguzwa na antihistamines za kizazi cha kwanza. Hata hivyo, antihistamines za kizazi cha kwanza inahusishwa na athari mbaya kama vile utepetevu. Decongestants zingine kama vile pseudoephedrine pia ni bora kwa watu wazima. Kinyunyizio cha Ipratropium cha pua pia inaweza kupunguza dalili za mafua, lakini kuna athari kidogo kwenye fukuto. Antihistamines za kizazi cha pili haionekani kuwa bora.

Kutokana na ukosefu wa masomo, haijulikani kama kuongezeka kwa ulaji wa maji inaboresha dalili au kupunguza ugonjwa kupumua. Ukosaji wa data kama hiyo ipo kwa matumizi ya hewa ya joto. Utafiti mmoja uligundua mvuke wa kusugua kifua ni fanisi katika kutoa baadhi ya tulizo la dalili ya kukohoa usiku, foleni, na ugumu wa usingizi.

Viua vijasumu na Kinza virusi

Viua vijasumu haina athari dhidi ya maambukizi ya virusi na hivyo haina athari dhidi ya homa. Viua vijasumu kwa kawaida huagizwa ingawa madhara ya viua vijasumu husababisha madhara kwa ujumla. Viua vijasumu kwa kawaida huagizwa kwa sababu watu wanatarajia watabibu kuziagiza na watabibu wanataka kusaidia watu. Maagizo ya viua vijasumu pia hutokea kwa sababu ni vigumu kutenga sababu ya maambukizi ambayo yanaweza kusimamiwa na viua vijasumu. Hakuna madawa fanisi za kuzuia virusi za homa ingawa baadhi ya utafiti wa awali imeonyesha faida.

Matibabu mbadala

Wakati kuna matibabu mengi mbadala inayotumika kwa homa, kuna upungufu wa ushahidi wa kisayansi wa kuunga mkono matumizi ya matibabu zaidi. Kufikia mwaka 2010, hakuna ushahidi wa kutosha wa kupendekeza kwa au dhidi ya aidha asali au umwagiliaji kwa pua. Virutubisho vya zinki vinaweza kupunguza ukali na muda wa dalili wakati itamezwa ndani ya masaa 24  ya mwanzo wao. Athari za vitamini C kwa homa, wakati inafanyiwa utafiti sana, inakatisha tamaa. Ushahidi kuhusu manufaa ya echinacea haiendani. Aina tofauti ya virutubisho vya echinacea inaweza kutofautiana katika utendaji wao.

Matokeo

Homa kwa kawaida ni kidogo na hupotea pekee yake na dalili nyingi kuwa bora katika wiki moja. Matatizo makubwa, kama yatatokea, kwa kawaida huwa katika watu wazee sana, vijana, au wale ambao wanashida ya kinga (wana mfumo dhaifu wa kinga). Maambukizi sekondari ya bakteria yanaweza kutokea na kusababisha sinusitis, pharyngitis, au maambukizi ya masikio. Inakadiriwa kuwa sinusitis hutokea katika matukio ya asilimia 8. Maambukizi ya sikio hutokea katika matukio ya asilimia 30.

Uwezekano

Homan ni zaidi ya ugonjwa wa kawaida wa binadamu na watu wanaathirika kimataifa. Watu wazima kwa kawaida huwa na maambukizi mbili hadi tano kwa mwaka. Watoto wanaweza kuwa na homa sita hadi kumi kwa mwaka (na homa hadi kumi na mbili kwa mwaka kwa watoto wa shule). Viwango vya maambukizi ya dalili huongezeka katika wazee kutokana na kudhoofika kwa mfumo wa kinga.

Historia

Wakati chanzo cha homa imetambuliwa tu tangu miaka ya 1950, ugonjwa umekuwa na ubinadamu tangu nyakati za kale. Dalili zake na matibabu zinaelezwa katika Ebers papyrus ya Misri, maandishi kongwe yaliyopo ya matibabu, iliyoandikwa kabla ya karne ya 16 KK. Jina "homa" ilikuja katika matumizi ya karne ya 16, kutokana na kufanana kati ya dalili zake na zile zitokanazo na hali ya hewa baridi.

Katika Uingereza, Kitengo cha Homa (CCU) kilianzishwa na Baraza la Utafiti wa Afya katika mwaka 1946 na ilikuwa hapa kwamba rhinovirus iligunduliwa katika mwaka 1956. Katika miaka ya 1970, CCU imeonesha kwamba matibabu na interferon wakati wa awamu ya kupevuka kwa maambukizi ya rhinovirus inatoa baadhi ya kinga dhidi ya ugonjwa. Hakuna tiba ya vitendo iliweza kukuzwa. Kitengo kilifungwa katika mwaka 1989, miaka miwili baada ya kukamilisha utafiti wa zinc gluconate lozenges katika kuzuia matibabu ya homa ya rhinovirus. Zinki ilikuwa tu ni matibabu fanisi iliyoundwa katika historia ya CCU.

Athari za kiuchumi

Mafua Ya Kawaida 
British poster from World War II describing the cost of the common cold

Athari za kiuchumi ya homa hazifahamiki vizuri katika mengi ya dunia. Nchini Marekani, homa inaongoza kwa ziara watabibu milioni 75 hadi milioni 100 kila mwaka katika makisio ya gharama ya $ 7.7 kwa mwaka. Wamarekani wanatumia dola bilioni 2.9 kwa madawa ya dukani (OTC). Wamarekani hutumia dola za ziada milioni 400 kwa maagizo ya madawa kwa tukizo la dalili. Zaidi ya theluthi moja ya watu ambao walimwona daktari walipokea maagizo ya viua vijasumu. Matumizi ya maagizo ya viua vijasumu ina madhara kwa upinzani wa antibiotiki. Makadirio ya siku za shule milioni 22 hadi 189 hazihudhuriwi kila mwaka kutokana na homa. Kama matokeo, wazazi walikosa siku za kazi milioni 126 kukaa nyumbani ili kuwatunza watoto wao. Wakati ikiongezwa kwa siku za kazi milioni 150 ambazo hazikuhudhuriwa na wafanyakazi wanaosumbuliwa na homa, jumla ya athari za kiuchumi za hasara ya kazi inayohusiana na homa inazidi dola bilioni 20 kawa mwaka. Hii inachangia asilimia 40 ya muda uliopotezwa kutoka kazini nchini Marekani.

Utafiti

Idadi ya kinzavirusi zimejaribiwa kwa ufanisi katika homa. Kufikia mwaka 2009, hakuna zote zimepatikana kuwa fanisi na kutolewa idhini ya matumizi. Kuna majaribio yanayoendelea ya sawa za kinza viruzi ya pleconaril. Inaonyesha ahadi dhidi ya picornaviruses. Pia kuna majaribio yanayoendelea ya BTA-798. Aina ya pleconaril ya kumeza ilikuwa na masuala ya usalama na aina ya erosoli inachunguzwaa.

Watafiti kutoka kwa Chuo kikuu cha Maryland, College Park na UChuo kikuu cha Wisconsin–Madison imetambua genome kwa Matatizo yote inayojulikana ya virusi vinavyosababisha homa.

Marejeo

    References

Tags:

Mafua Ya Kawaida Dalili na isharaMafua Ya Kawaida VisababishiMafua Ya Kawaida UeneziMafua Ya Kawaida Maambukizo mengineMafua Ya Kawaida PathofisiolojiaMafua Ya Kawaida UaguziMafua Ya Kawaida UzuiajiMafua Ya Kawaida UsimamiziMafua Ya Kawaida MatokeoMafua Ya Kawaida UwezekanoMafua Ya Kawaida HistoriaMafua Ya Kawaida Athari za kiuchumiMafua Ya Kawaida UtafitiMafua Ya Kawaida MarejeoMafua Ya KawaidaKiingerezaMfumo wa upumuajiPuaShingoUgonjwa wa kuambukizwaw:common cold

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mkoa wa KigomaHistoria ya UislamuMichezo ya watotoWamasaiMachweoTanzaniaPundaIdi AminMkoa wa KataviKamusi za KiswahiliMvuaTabianchiOrodha ya maziwa ya TanzaniaNyaniWiki FoundationFisiKichochoUbunifuAgano JipyaMsituWaluoMamba (mnyama)UfupishoTungo sentensiBloguJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaUturukiMadhehebuMashuke (kundinyota)Biblia ya KikristoNomino za jumlaWahaPalestinaNguvaNabii IsayaMimba kuharibikaWaheheOrodha ya Marais wa MarekaniCleopa David MsuyaMaambukizi ya njia za mkojoUmoja wa KisovyetiUandishi wa barua ya simuUrusiFasihi andishiUhuru wa TanganyikaUmoja wa AfrikaOrodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaBomu la nyukliaAmina ChifupaLimauHeshimaDubai (mji)KunguniGeorge WashingtonShangaziMatiniBarua rasmiKiambishi awaliNigeriaMjusi-kafiriMpira wa miguuMkoa wa SongweIsimujamiiSahara ya MagharibiTiktokOrodha ya kampuni za TanzaniaSarufiBiashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiWhatsAppAnwaniNgeliAlama ya barabaraniUa🡆 More