Uhifadhi wa fasihi simulizi ni juhudi zinazofanywa kwa makusudi ya kuhakikisha kazi za fasihi simulizi zisisahaulike na hatimaye kupotea kabisa.
Kazi hizo zimeanza tangu binadamu walipoanza kupambana na mazingira yao ya kuishi pamoja. Kazi hizo zilisimuliwa na kuakisi shughuli zilizokuwa zikifanywa na watu katika mazingira ya wakati huo. Kadiri mazingira yalivyobadilika hali kadhalika mambo yaliyokuwa yakisimuliwa ndivyo yalivyokuwa yakibadilika. Hivyo, kulikuwepo na haja ya kuhifadhi kazi hizo kwa faida ya vizazi vipya.
Katika kuhifadhi kazi hizo, kuna njia mbalimbali zilizotumika tangu kale na nyingine zinazotumika leo kwa kufaidika na maendeleo ya teknolojia. Njia hizo ni:
(a) Kichwani / Akilini
(b) Kwa maandishi
(c) Kwa vinasa sauti
(d) Kwa kanda za video, runinga na tarakilishi
Kazi ya fasihi simulizi huwa katika hali ya masimulizi, hivyo mara nyingi huhifadhiwa katika akili ya mtu. Fasihi simulizi ikihifadhiwa kichwani huendelea kuwa hai kwani hadhira na fanani huweza kuwasiliana ana kwa ana. Hadhira huweza kumpongeza au kumhoji fanani papo kwa papo.
Fasihi simulizi huweza kuhifadhiwa katika maandishi. Mfano kwenye vitabu, vijarida na kadhalika. Fasihi simulizi ikihifadhiwa k2a njia hii haiwezi kupotea wala kubadilika. Njia hii inaweza kutunza kumbukumbu ya kudumu.
Hizi ni zana zinazotumika katika kurekodi sauti. Mfano wa zana hizo ni tepurekoda au santuri. Katika njia hii, ukweli wa sanaa ya kazi haitabadilika, sauti halisi ya wahusika itaendelea kusikika kama ilivotolewa. Hivyo, fasihi simulizi haipotei wala kubadilikabadilika.
Njia hii huweza kutumika katika kurekodi picha pamoja na sauti kisha kuzionyesha katika runinga au tarakilishi.
Fasihi simulizi ikihifadhiwa kuna faida mbalimbali zinazojitokeza. Miongoni mwa faida hizo ni:
i) Kutopotea kwa kazi hizo: Fasihi simulizi ikihifadhiwa uwezekano wa kupotea huwa haupo. Kitendo hiki husababisha kazi hiyo iendelee kutumika katika jamii husika.
ii) Kutunza amali ya jamii: Mambo yanayojadiliwa katika fasihi simulizi ni mambo mbalimbali ambayo ni desturi ya jamii husika. Kitendo cha kuhifadhi kazi za fasihi simulizi husaidia kutunza amali za jamii ili ziweze kutumika kwa vizazi vijavyo.
Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uhifadhi wa fasihi simulizi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Uhifadhi wa fasihi simulizi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.