Orodha Ya Magavana Wa Tanganyika

Magavana wa Tanganyika walikuwa wawakilishi wakuu wa Uingereza katika Tanganyika wakati wa ukoloni kuanzia 1920 hadi uhuru.

Walikuwa na mamlaka yote ya serikali kwa niaba ya serikali ya Uingereza.

Orodha Ya Magavana Wa Tanganyika
Bendera ya Tanganyika (1919-1961)

Baada ya uhuru wa Tanganyika kwenye tarehe 9 Desemba 1961 gavana Mwingereza Richard Turnbull aliitwa "gavana mkuu" (general governor) alikuwa mwakilishi wa malkia aliyekuwa mkuu wa dola hadi kuanzishwa kwa jamhuri ya Tanganyika mnamo tar. 9 Desemba 1962.

Magavana wa enzi ya Kijerumani

Hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia maeneo ya Tanganyika yalikuwa sehemu ya koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliyoanzishwa kuanzia mwaka 1885 kwa njia ya vituo vya kampuni ya kibinafsi Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki lililoongozwa na Carl Peters. Shirika hilo halikufaulu kuanzisha utawala halisi nje ya vituo vichache. Baada ya kuporomoka kwa shirika kutokana na upinzani wa watu wa pwani chini ya Abushiri mnamo 1888 serikali ya Ujerumani iliingia kati kwa kutuma kikosi cha kijeshi chini ya kamishna Wissmann.

  • 1888–1891: Hermann von Wissmann (kamishna wa kijeshi)
  • 1891–1893: gavana Julius von Soden
  • 1893–1895: gavana Friedrich von Schele
  • 1895–1896: gavana Hermann von Wissmann
  • 1896–1901: gavana Eduard von Liebert
  • 1901–1906: gavana Gustav Adolf Graf von Götzen
  • 1906–1912: gavana Georg Albrecht von Rechenberg
  • 1912–1918: gavana Heinrich Albert Schnee

Orodha ya Magavana wa Tanganyika

Tangu mwaka 1917/18 maeneo yote ya Tanganyika yalitawaliwa na jeshi la Uingereza. Mwaka 1922 utawala ulipelekwa chini ya utawala wa kiraia wa Kiingereza uliotekelezwa na gavana. Mwaka 1922 Shirikisho la Mataifa liliamua kukabidhi Tanganyika mkononi mwa Ufalme wa Maungano (Uingereza) .

Jina Miaka ya maisha Muda wa Utawala
Sir Horace Archer Byatt (* 1875, † 1933) 22 Julai 1920 - 5 Machi 1925
Donald Charles Cameron (* 1872, † 1948) 5 Machi 1925 - Januari 1931
Sir George Stewart Symes (* 1882, † 1962) Januari 1931 - Februari 1934
Sir Harold MacMichael (* 1982, † 1969) 19 Februari 1934 - 8 Julai 1938
Sir Mark Aitchison Young (* 1886, † 1974) 8 Julai 1938 - 19 Julai 1941
Sir Wilfrid Edward Francis Jackson (* 1883, † 1971) 19 Juni 1941 - 28 Aprili 1945
Sir William Denis Battershill (* 1896, † 1959) 28 Aprili 1945 - 18 Juni 1949
Sir Edward Twining, Baron Twining (* 1899, † 1967) 18 Juni 1949 - Juni 1958
Sir Richard Gordon Turnbull (* 1909, † 1998) 15 Julai 1958 - 9 Desemba 1961

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Quincy Wright: Mandates under the League of nations, Chicago, Ill. : The University of Chicago press, [1930], online hapa kwenye tovuti ya hathitrust.org

Tags:

Orodha Ya Magavana Wa Tanganyika Magavana wa enzi ya KijerumaniOrodha Ya Magavana Wa Tanganyika Orodha ya Magavana wa TanganyikaOrodha Ya Magavana Wa Tanganyika Tazama piaOrodha Ya Magavana Wa Tanganyika TanbihiOrodha Ya Magavana Wa Tanganyika MarejeoOrodha Ya Magavana Wa Tanganyika

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Kiazi kikuuFasihi andishiUkoloniIjumaa KuuMikoa ya TanzaniaNyaniHektariZana za kilimoVita Kuu ya Kwanza ya DuniaNominoMtandao wa kompyutaChaiVitenzi vishiriki vipungufuKiswahiliHistoria ya Kanisa KatolikiUhakiki wa fasihi simuliziMimba za utotoniKidole cha kati cha kandoSoko la watumwaUbatizoNomino za dhahaniaMkoa wa PwaniTiba asilia ya homoniNamba za simu TanzaniaZama za MaweJinsiaMsituKarafuuMarekaniWilaya ya HandeniHistoria ya TanzaniaWaluguruTaasisi ya Taaluma za KiswahiliBendera ya KenyaMariooKima (mnyama)Hekalu la YerusalemuMashuke (kundinyota)NevaJuxHaitiOrodha ya Marais wa TanzaniaNabii IsayaWakingaSayariTausiSkeliMwigizajiAir TanzaniaKukuMongoliaUkabailaMji mkuuNembo ya TanzaniaJumapili ya matawiUgonjwa wa kupoozaAustraliaMfumo wa JuaOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaKupatwa kwa MweziMapambano kati ya Israeli na PalestinaOrodha ya Marais wa UgandaMshororoKengeAla ya muzikiBungeWhatsApp🡆 More