Ubunifu (kutoka kitenzi chenye asili ya Kiarabu kubuni; pia: ugunduzi, japo si maneno yanayolingana kabisa katika maana zake.
) mara nyingi huchukuliwa kuwa ni matumizi ya njia bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya, changamoto ambazo tayari zipo lakini hazijapatiwa ufumbuzi bado, au changamoto zilizopo kwenye soko au jamii kwa kipindi husika.
Dhana hii hutimilika pale ambapo bidhaa, huduma, teknolojia, mpangilio wa biashara au njia nyingine yoyote inayoweza kutatua changamoto husika katika jamii ni adimu kuipata katika masoko ya kiuchumi, serikali au jamii yenyewe.
Neno ubunifu linaweza kutafsiriwa kuwa ni kitu fulani halisia na chenye mchango wa wazi katika jamii na hivyo ni kitu kipya kinachojitokeza katika soko au jamii kwa hali ya upya.
Ubunifu chanzo chake ni Mungu maana ndiye aliyeanzisha vitu vyote kwa kuachilia mawazo ndani ya watu.
Ili ubunifu uweze kuonekana ni lazima wabunifu waaminiwe, wapewe kipaumbele, ikiwezekana pia wapewe mitaji na kuendeleza elimu za ubunifu wao.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Ubunifu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.