Manii

Manii (pia: shahawa; kwa Kiing.

sperm, spermatozoa) ni mbegu za madume wa wanyama zinazozalishwa katika korodani. Kila chembe ya manii (spermatozoo) ni seli inayoweza kusogea nje ya mwili.

Manii
Picha iliyokuzwa sana ya spermatozoo wakati inapojaribu kuingia ndani ya kijiyai cha mwanamke.
Shahawa jinsi inavyoonekana kwa hadubini.

Kazi yake ni kubeba kromosomu zenye taarifa za jenetikia (yaani sifa za mwili inakotoka) na kupitia uterasi ya jike na kuingia ndani ya virijaova (virija vya uzazi vya jike) huko ndani ya yai. Kuingia kwa spermatozoo ndani ya yai kunasababisha ungano la ADN ya yai na spermatozoo na mgawanyo wa yai ambalo ni chanzo cha kiumbehai mpya.

Umbo la spermatozoo linaundwa na "kichwa" kidogo kinachobeba ADN na mkia mrefu ambao mwendo wake unasogeza seli mbele. Umbo hilo linafanana na kiluwiluwi mdogo lakini ni seli 1 tu.

Manii ya binadamu huzalishwa katika korodani za mwanamume. Kila seli ya manii ina kromosomu 23. Seli za mwili huwa na kromosomu 46, kwa hiyo spermatozoo inabeba nusu ya taarifa zinazohitajika kwa kuanzisha kiumbe kipya. Nusu nyingine inapatikana katika yai la mwanamke ambako spermatozoo inaelekea kuingia.

Wakati wa tendo la ndoa manii yanachanganyika kwa viowevu kutoka kibofushahama na tezi za shahawa na mchanganyiko huo unafyatuliwa nje ya mboo. Kama hii inatokea ndani ya kuma ya mwanamke, shahawa inasambaa na kuenea ndani ya kuma. Ilhali idadi ya spermatozoo ni kubwa sana, yaani seli zaidi ya milioni mia nne (400,000,000), uwezekano ni mkubwa kwamba seli kadhaa zitafika hadi virijaova na kukuta yai lililo tayari. Si zaidi ya seli 100 kati ya milioni zilizotoka ambazo zinafika kwenye yai.

Yai lililo tayari linapokea spermatozoo moja tu. Hapo kromosomu 23 ndani ya yai zinaunganishika na kromosomu 23 za spermatozoo na kufanya jumla ya 46 zinazotosha kuanzisha kiumbe kipya.

Marejeo

Viungo vya Nje

Manii 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Manii  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Manii kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

DumeKiing.MbeguMnyamaMwiliSeliShahawa

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Tanganyika African National UnionVivumishi vya pekeeMagonjwa ya kukuKiraiEdward SokoineMafumbo (semi)Kalenda ya KiislamuChakulaVita Kuu ya Pili ya DuniaMzabibuWabondeiMartin LutherChepeMarekaniRisalaKamusiMobutu Sese SekoMapambano kati ya Israeli na PalestinaVielezi vya mahaliKata (maana)Vielezi vya idadiUtamaduniUtataWairaqwNyangumiHekalu la YerusalemuIstilahiUchimbaji wa madini nchini TanzaniaNelson MandelaErling Braut HålandKadi za mialikoMapambano ya uhuru TanganyikaMkoa wa SingidaNusuirabuKidoleViwakilishi vya kuulizaNevaMapafuLingua frankaLenziVivumishi vya jina kwa jinaManchester CityWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiUchumiKitenziMatiniInshaMkanda wa jeshiSemantikiMuda sanifu wa duniaTarbiaMamaLigi ya Mabingwa UlayaSaudiaDaktariMfumo wa upumuajiMiikka MwambaKoloniDhahabuWanyama wa nyumbaniMwanzo (Biblia)Mpira wa miguuWakingaJokofuMkoa wa ShinyangaVita vya KageraNyumba ya MunguNg'ombeMbwaMichael JacksonKihusishiTanganyika (ziwa)SitiariJangwa🡆 More