Teknolojia (kutoka Kiingereza: Technology ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi, ujenzi, vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii.
Asili ya neno ni Kigiriki "τέχνη" (tamka: tékhne): „uwezo, usanii, ufundi".
Teknolojia inaweza kumaanisha:
Teknolojia nyepesi kabisa ni ujuzi wa kutumia vyombo ili kurahisisha kazi. Kwa mfano, katika somo la historia, mwanadamu alivumbua teknolojia ya kuwasha na kudhibiti moto amabo ulimwezesha kupika. Vile vile, aliweza kutumia mawe kwa kulima na kuwinda. Kadri wakati ulivyoenda ndivyo teknolojia yake ilivyoboreka kwa mfano kwa uvumbuzi wa gurudumu lililorahisisha ukulima na kusafiri kwake.
Maendeleo ya teknolojia ya kale yalihusisha uvumbuzi wa chombo cha kupiga chapa, simu na mtandao ambazo zimefanya mawasiliano yawe rahisi.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Teknolojia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.