Popo

Nusuoda 2:

Popo
Popo-masikio wa Townsend (Corynorhinus townsendii)
Popo-masikio wa Townsend
(Corynorhinus townsendii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Ngeli ya chini: Eutheria
Oda: Chiroptera (Wanyama kama popo)
Ngazi za chini

Popo ni mamalia kama panya wenye mabawa.

Spishi zake nyingi sana hula wadudu: hizi zimo katika nusuoda Yangochiroptera.

Spishi kubwa za nusuoda hii hula ndege, mijusi, vyura na hata samaki.

Spishi chache za popo wanyonya-damu huko Amerika ya Kusini hula damu ya mamalia au ndege.

Familia Pteropodidae ya nusuoda Yinpterochiroptera ina spishi kubwa hadi ukubwa wa paka na uzito wa kilogramu moja; urefu wa mabawa pamoja unaweza kufikia sentimita 150. Spishi hizi hula matunda.

Uainishaji

Hapo awali, popo waligawanywa katika nusuoda Microchiroptera na Megachiroptera. Walakini, tafiti za ADN zilifunua kuwa baadhi ya familia za Microchiroptera zilikuwa karibu na Megachiroptera. Kwa hivyo, nusuoda mbili mpya zilipendekezwa, Yangochiroptera na Yinpterochiroptera. Nusuoda ya mwisho imegawanywa katika familia za juu Pteropodoidea (popo-matunda) na Rhinolophoidea (popo-wadudu; spishi mbalimbali hula vertebrata wadogo).

Utambuaji kwa mwangwi

Popo wengi hutumia sauti kwa kutambua mazingira yao, yaani wanatumia mwangwi wa mlio wao kukadiria umbali hadi kizuizi au hata windo pamoja na ukubwa na maumbile ya vitu vilivyopo njiani. Kwa hiyo masikio yao ni mlango wa fahamu muhimu zaidi. Kinyume chake popo wengi hawana macho mazima ingawa hakuna aliye kipofu kabisa. Lakini kuna pia aina nyingine wanaoona vizuri sana.

Picha

Popo  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Popo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MlongeNdege (mnyama)Lahaja za KiswahiliMsituBiblia ya KikristoKihusishiNgono zembeMnyoo-matumbo MkubwaFamiliaKipindupinduMkoa wa MaraTendo la ndoaNgoma (muziki)MadhehebuMkoa wa LindiMajiUislamuUvuviMatumizi ya lugha ya KiswahiliRisalaFasihi simuliziUbepariIdi AminMkataba wa Helgoland-ZanzibarChawaTetemeko la ardhiTupac ShakurZama za ChumaSkeliUpendoAfrika ya Mashariki ya KijerumaniPemba (kisiwa)Ukwapi na utaoHuzuniKongoshoJumuiya ya MadolaElimuWapareTungo sentensiMkoa wa DodomaUtafitiMbuVitendawiliShangaziKajala MasanjaSalaKilatiniShabuAlama ya uakifishajiWangoniMkoa wa SimiyuJoyce Lazaro Ndalichako22 ApriliTungoSayansiWayahudiWahangazaInsha za hojaMkoa wa TangaMuungano wa Madola ya AfrikaAlama ya barabaraniMimba za utotoniBendera ya KenyaUshairiMaambukizi ya njia za mkojoMimba kuharibikaUlumbiAfrika ya MasharikiMbadili jinsiaMandhariMjasiriamaliKitenzi kikuu kisaidiziPaka (maana)Kamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniMfumo wa neva🡆 More