Mvua ni matone ya maji yanayoanguka chini kutoka mawingu angani.
Mvua ni aina ya usimbishaji. Kama matone yafikia kipenyo cha zaidi ya milimita 0.5 huitwa mvua. Kama matone ni madogo zaidi kunaitwa manyonyota. Mgongoni mwa ardhi mvua imetapaka kisawasawa.
Asili ya mvua ni mvuke wa maji katika angahewa. Kiasi cha mvuke hewani kutajwa kama gramu za maji kwa kilogramu ya hewa. Kiasi cha unyevu (yaani maji) katika angahewa huitwa unyevuanga. Uwezo wa hewa kushika unyevuanga hutegemea halijoto ya hewa. Hewa baridi ina uwezo mdogo kutunza unyevu ndani yake, kiasi kinaongezeka kadiri halijoto iko juu zaidi. Pale ambapo hewa inafikia hali ya kushiba unyewu unaanza kutonesha yaani matone kutokea. Wakati matone yanafikia kiwango fulani cha uzito yanaanza kuanguka chini yaani mvua inaanza kunyesha.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mvua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mvua, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.