Mzizi

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Mizizi

Mzizi katika isimu ni sehemu muhimu sana ya neno ambayo haibadiliki hata kama neno litafanyiwa uambishaji, ukanushi, unyambulishaji na kadhalika. Sehemu hii ikibadilika, hata dhana ya neno hilo hubadilika

Mzizi wa neno ni sehemu ya neno inayobaki baada ya kuondoa viambishi tamati na viambishi awali au, kwa maneno mengine, mzizi wa neno ni sehemu yake inayobaki baada ya kuondoa viambishi vyote.

Kwa mfano: mzizi wa neno "Analima" ni "lim". Hii hutokana na kuchukua neno na kisha kulitafutia shina lake (kitenzi) na kisha kuondoa kiambishi tamati "a".

Jinsi ya kupata mzizi wa neno

  1. Chukua neno lenyewe.Mfano; "Analima"
  2. Tafuta shina la neno hilo (neno hilo katika kitenzi chake).Mfano; shina la neno (Analima) ni "lima".
  3. Kisha ondoa kiambishi tamati "a".Mfano;Lima - a =Lim (kwa hiyo neno hilo ni mzizi wa neno analima).

Kwa hiyo, MZIZI WA NENO = SHINA-A.

Kwa mfano: neno "anakimbia" mzizi wa neno ni "kimbi". Kutokana na mzizi huo, unaweza kuzalisha maneno kama sitakimbia, hakimbii, tunakimbia n.k.

Aina za mizizi ya maneno

Kuna aina mbili za mizizi ya maneno:

  1. Mzizi asilia
  2. Mzizi mnyumbuliko

Mzizi asilia

Hii ni aina ya mzizi ambao hupatikana baada ya neno kutafutiwa shina lake na kuondolewa irabu "a" ambayo ni kiambishi tamati. Mfano wa mzizi asilia ni wakati unapochukua neno "Analima" na kulitafutia shina lake ambalo ni "Lima" na kisha kuondoa kiambishi tamati "a".

Hivyo mzizi wa asili ni mzizi ambao hutokana na kitenzi halisi. Yaani, ni mzizi ambao umejengwa kwa shina la neno lililoondolewa irabu "a". Kikanuni tunaweza kusema MZIZI = SHINA - A. Mfano katika neno "anakimbia" shina ni "kimbia". Ili kupata mzizi ni lazima utoe irabu "a", hivyo mzizi utakuwa "kimbi" ambao huo tunaweza kuuita mzizi wa asili.

Mzizi mnyumbuliko

Huu ni aina ya mzizi ambao hupatikana baada ya kutafuta shina la neno na kisha kulifanyia uambishaji na kisha kulifungulia au kuondoa kiambishi tamati "a".

Mfano: "Wapigana" shina lake ni "piga" lakini baada ya kufanyiwa uambisani limekuwa "pigana" ambapo ili kupata mzizi mnyumbuliko tunaondoa herufi "a" katika neno "pigana" ambapo neno hilo mzizi wake mnyambuliko utakuwa "pigan".

Pia neno kama "wanaimbiana" baada ya kufanyiwa uambishi katika shina lake huwa "imbiana" ambalo baada ya kutolewa kiambishi tamati "a" huwa "imbian" Kwa upande wa mzizi wa mnyumbuliko, ni mzizi ambao umejengwa kwa mzizi wa asili na viambishi tamati vilivyoondolewa irabu "a".

Mfano wa maneno ya mnyumbuliko ni kama vile: chezesha, chezeshwa, chezeka n.k. Mfano kitenzi "Chezesha" mzizi wake wa mnyumbuliko ni "Chezesh", hapo mzizi wa asili ni "Chez" na viambishi tamati ni "esh".

Mzizi  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzizi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Mzizi Jinsi ya kupata mzizi wa nenoMzizi Aina za mizizi ya manenoMzizi asiliaMzizi mnyumbulikoMziziMizizi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Paul MakondaMajira ya mvuaAla ya muzikiMkoa wa RukwaTreniFonimuMkoa wa TangaSayansiSarangaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaViwakilishi vya pekeeOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaYesuPopoMsokoto wa watoto wachangaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaMaadiliAbrahamuMahakama ya TanzaniaRamaniJakaya KikweteMkoa wa Unguja Mjini MagharibiRose MhandoNyangumiBaruaMkoa wa Dar es SalaamUgonjwa wa uti wa mgongoMadhara ya kuvuta sigaraKitenzi kikuu kisaidiziTarbiaWaluguruSomo la UchumiJohn Samwel MalecelaMkataba wa Helgoland-ZanzibarMange KimambiUajemi ya KaleKipimajotoMatumizi ya lugha ya KiswahiliNimoniaUNICEFGhanaKupakua (tarakilishi)SakramentiTungo kishaziKiunzi cha mifupaMuda sanifu wa duniaMafarisayoMaghaniZuchuRushwaUtumwaWilaya ya ArumeruWimboBendera ya TanzaniaVivumishiLigi ya Mabingwa AfrikaMaradhi ya zinaaMtakatifu MarkoTafsidaVirusi vya CoronaAfande SeleMkoa wa KataviKisimaViwanja vya Afrika (Kwa Ukubwa)LahajaInsha za hojaKen WaliboraNdoaMkopo (fedha)Kinembe (anatomia)Athari za muda mrefu za pombe🡆 More