Musuli

Misuli ni sehemu ya mwili wa wanyama na binadamu inayowezesha mwendo wa viungo vyake.

misuli inaundwa na tishu ya pekee yenye uwezo wa kujinywea na kulegea. Wakati wa kujinywea huwa mifupi zaidi. Kwa njia hii misuli inayounganishwa na mifupa ya mkono au mguu huleta mwendo wa viungo hivi.

Musuli
Kazi ya musuli mkononi.
Musuli
Aina za musuli:
misulia milia, misuli myororo, misuli ya moyo

Aina za musuli

Misuli hutofautishwa kwa namna mbalimbali:

  • kama ni misuli ridhia inayoendeshwa kwa hiari maana tunaamua kuzinywea au kuzilegeza (kama misuli ya kusogeza mkono) au misuli sihuria inayoendeshwa bila hiari (kama misuli inayoendesha mwendo wa utumbo)
  • kufuatana na umbo na muundo wa misuli kama ni misuli milia (striped muscle) au misuli myororo (smooth muscle)

Mara nyingi hutofautishwa namna tatu za misuli:

  • misuli kiunzi iinayounganishwa na mifupa kwa ukano. Hii misuli inasababisha mwendo wa mifupa ya viungo na kuendeshwa kwa ridhia ya mtu kwa hiyo inaitwa pia misuli ridhia. Katika mwili wa mwanaume wastani hii misuli kiunzi ni takriban asilimia 42 ya masi ya mwili wake; kwa mwili wa mwanamke wa wastani hii misuli ni 36 % ya masi ya mwili. Hiyo ndiyo sababu ya kwamba kwa wastani wanaume wana nguvu kuliko wanawake.
  • misuli msisima ambayo haiunganishwi na mifupa na kuendesha mwendo wa viungo vya ndani vya mwili kama utumbo, mapafu, mizizi ya nywele au mishipa ya damu. Misuli hii hiongozwi kwa ridhia huitwa misuli sihuria.
  • misuli ya moyo ni misuli sihuria lakini kwa umbo hufanana zaidi na misuli kiunzi. Wakati misuli hii inajikaza inasukuma damu kwenda mishipa ya damu upande moja na ikilegea upande mwingine kupokea damu kutoka mishipa.

Misuli milia

Misuli ya kiunzi na moyo huitwa pia "misuli milia" kutokana na milia inayoonekana usoni mwao. Milia hii inatokana na muundo wa misuli hii inayofanywa na vinyuzi virefu vya rangi mbili vinavyopangwa taratibu katika misuli na kuonyesha milia meupe na mekundu kwa kubadilishana. Vinyuzi vyekundu ni protini za kiaktini na vinyuzi vyeupe ni protini kimiosi.

Muundo wa misuli

Misuli inaundwa na seli za pekee zenye uwezo wa unyweo. inatekeleza unyweo baada ya kupokea kiamshi kupitia neva. Kiamshi ni mshtuko wa umeme unaopitishwa kutoka seli kwenda seli nyingine. Seli za misuli huwa na protini za kiaktini na kimiosini.

Unyweo wa misuli

Wakati misuli inapokea kiamshi kutoka neva nafasi katika utando wake inapitisha kalsi na kalsi inasababisha aina mbili za protini kuingiliana hivyo kufupisha urefu wa misuli.

Jinsi ya kuunda misuli

  • Anza polepole. Kuunda misuli huchukua muda mrefu na haifai ujiweke presha kupata misuli kwa muda mfupi.
  • Kuwa na mpango na mikakati unayofuata ili kuweza kuifikia kama vile mipango ya wakati wa kufanya mazoezi, kuinua chuma au kula.
  • Chakula kina maana sana katika misuli haswa protini ambayo wafaa uile kwa wingi. Maji pia ni muhimu kwa umetaboli.
  • Fuata mikakati uliyopanga na usife moyo hata usipoona matokeo kwa haraka.

Marejeo

Viungo vya nje

Musuli  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Musuli kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Musuli Aina za musuliMusuli Misuli miliaMusuli Muundo wa misuliMusuli Unyweo wa misuliMusuli Jinsi ya kuunda misuliMusuli MarejeoMusuli Viungo vya njeMusuliBinadamuMwiliWanyama

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WahadzabeHafidh AmeirFasihi andishiIfakaraMajira ya mvuaVita ya Maji MajiSah'lomonLugha za KibantuMuhammadOrodha ya Marais wa ZanzibarKimeng'enyaPijiniNguzo tano za UislamuKiolwa cha angani25 ApriliMobutu Sese SekoFonolojiaMlima wa MezaSaidi Salim BakhresaSayansi ya jamiiSkeliUhakiki wa fasihi simuliziCleopa David MsuyaRufiji (mto)NandyViwakilishiMeliNyangumiSanaa za maoneshoKunguruUbaleheAfrika KusiniVivumishi vya kumilikiRuge MutahabaMfumo wa upumuajiMaudhuiKinembe (anatomia)Bendera ya TanzaniaUkimwiMbeya (mji)TiktokLiverpool F.C.Bikira MariaWakingaMkoa wa TangaHaki za watotoOrodha ya nchi kufuatana na wakaziMtandao wa kijamiiFutiUkristo barani AfrikaUzalendoZiwa ViktoriaViwakilishi vya pekeeAsili ya KiswahiliMatumizi ya lugha ya KiswahiliHistoria ya WasanguYoung Africans S.C.HedhiHaki za wanyamaBunge la TanzaniaKitenzi kishirikishiWilaya ya KinondoniMoses KulolaKiambishi tamatiSexUpepoOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoOrodha ya Marais wa KenyaUaUhuru wa Tanganyika🡆 More