Ngumi ni hali ya mkono ukifumbatwa, yaani kwa kukunja vidole pamoja na kiganja.
Kusudi la kukunja ngumi ni mara nyingi kupiga kwa nguvu, au kujiandaa kwa kupiga. Kutokana na maana hii ngumi inakunjwa pia kama alama ya hasira au ya upinzani, kwa mfano katika salamu ya Black Power.
Michezo ya mapigano mbalimbali hutegemea matumizi ya ngumi, hasahasa mchezo wa ngumi lakini pia karate au taekwondo.
Watafiti wamegundua ya kwamba kukunja ngumi inaweza kusaidia kuondoa hofu au wasiwasi kwa kuelekeza fikra kwa musuli na kuondoa fikra za wasiwasi.
Kwa wtu wengine inaweza kusaidia pia kuelekeza fikra kwa jambo au kukumbuka habari.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Ngumi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.