Kipandauso

Kipandauso ni tatizo linalotambulika kwa maumivu ya kichwa yanayojirudia tena makali hadi kiasi cha kupindukia na ambayo wakati mwingi huambatana na dalili nyingi za mfumo wa neva.

Migraine
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyNeurology Edit this on Wikidata
ICD-10G43.
ICD-9346
OMIM157300
DiseasesDB8207 (Migraine)
31876 (Basilar)
4693 (FHM)
MedlinePlus000709
eMedicineneuro/218 neuro/517 emerg/230 neuro/529
MeSHD008881

Jina la Kiingereza "Migraine" limetoka katika neno la Kigiriki ἡμικρανία (hemikrania), "uchungu kwa upande mmoja wa kichwa", kutoka ἡμι- (hemi-), "nusu", na κρανίον (kranion), "fuvu la kichwa".

Kwa kawaida, maumivu hayo huathiri sehemu moja ya kichwa, huku kikidunda kwa muda wa saa 2 hadi 72. Dalili zinazohusiana na hali hii ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, fotofobia, fonofobia (ongezeko la usikivu dhidi ya sauti) na uchungu wake kwa kawaida huzidishwa na shughuli za kimwili. Hadi thuluthi moja ya watu wenye ugonjwa wa kipandauso kinachoandamana na maumivu ya kichwa hupata aura: ishara bandia ya matatizo ya macho, hisia, lugha au mwendo inayoashiria kuwa maumivu ya kichwa yatatokea punde.

Kipandauso huaminika kutokea kufuatia mchanganyiko wa masuala ya kimazingira na kijeni.Thuluthi mbili za kesi hizo zinahusika na familia.

Kiwango cha homoni kinachoshuka na kupanda pia kinaweza kuwa kisababishi cha ugonjwa huu: kipandauso huathiri wavulana kwa kiwango cha juu kidogo kuliko wasichana kabla ya kubalehe, ingawa kinawaathiri wanawake mara mbili hadi tatu kuliko wanaume, ila ujauzito unakipunguza.

Utaratibu wa ugonjwa huu haujatambulika. Hata hivyo, hali hii inaaminika kuwa tatizo la mfumo wa neva. Nadharia ya msingi inahusiana na kuongezeka kwa uchangamfu wa koteksi ya serebramu na udhibiti usio wa kawaida wa maumivu ya nyuroni kwa kiiniseli cha trijemia cha mfumo wa ubongo.

Matibabu ya kwanza yanayopendekezwa ni dawa za kuondoa maumivu kama vile ibuprofen na acetaminophen ili kutuliza maumivu ya kichwa na antiemetic ili kutuliza kichefuchefu na kuepuka vichocheo. Dawa maalumu kama vile triptan au ergotamine zinaweza kutumika kwa watu wasiosaidiwa na dawa za kawaida za kuondoa maumivu. Zaidi ya asilimia 10 ya watu wote ulimwenguni huathiriwa na kipandauso wakati fulani maishani mwao.

Ishara na dalili

Kwa kawaida kipandauso hutokea pamoja na maumivu ya kichwa makali, yanayojisetiri na yanayojirudiarudia ambayo huhusishwa na dalili za mfumo unaojiongoza wa neva. Takriban asilimia 15-30 za wenye kipandauso hukabiliwa na aura lakini mara nyingi hupata kipandauso kisicho na dalili za aura. Ukali wa maumivu ya kichwa, muda yanayochukua na marudio yake hubadilika mara kwa mara. Kipandauso kinachodumu zaidi ya saa 72 hujulikana kwa Kilatini kama status migrainosus.

Kuna awamu nne zinazoweza kutokea kwa kipandauso, ingawa si sharti mtu azipitie zote :

  1. Dalili za awali ambazo hutokea saa au siku chache kabla ya maumivu ya kichwa
  2. aura hutangulia maumivu ya kichwa
  3. Awamu ya maumivu ya kichwa.
  4. Dalili za baadaye, athari zinazofuatia kukabiliwa na kipandauso

Awamu ya dalili za awali

Dalili za awali hutokea kwa asilimia ~60 ya watu wanaopata kipandauso zinazoanza kwa saa mbili hadi siku mbili kabla ya kuanza kwa maumivu au aura Dalili hizi zinajumuisha visa mbalimbali pamoja na: mabadiliko kwa halihisi ya moyo, kukereka, mfadhaiko au uforia, uchovu, kushaukia chakula fulani, kukazana misuli (hasa shingoni), uyabisi wa utumbo au kuhara, na kuchukia harufu au kelele. Hali hii inaweza kutokea kwa watu wenye kipandauso chenye aura au kisicho na aura

Awamu ya aura

Kipandauso  Kipandauso 
Kipandauso  Kipandauso 

aura ni hali ya neva za macho inayopita na hutokea kabla au wakati wa maumivu ya kichwa.Dalili hizi hutokea polepole kwa dakika kadhaa na kwa jumla hudumu kwa kipindi kisichopita dakika 60 . Dalili hizi zinaweza kuwa za kuona, kuhisi au za kimwendo, na watu wengi hupata zaidi ya dalili moja. Athari za kuona ndizo zinazotokea mara nyingi zaidi, na hutokea kwa hadi visa asilimia 99 na zaidi, nusu yake vikiwa na hatari hizi pekee. Matatizo ya kuona mara nyingi huhusisha skotoma yenye vimulimuli (eneo la jicho lisiloona kwa sehemu ya kutazamia inayowaka). Tatizo hili kwa kawaida huanzia karibu na kiini cha sehemu ya kuona, kisha kusambaa kuelekea pande zote kwa mistari ya zigizagi inayofananishwa na nguzo au kuta. Kwa kawaida, mistari hii huwa nyeusi na nyeupe lakini watu wengine huona mistari yenye rangi. Baadhi ya watu hupoteza sehemu muhimu ya kuona inayojulikana kama hemianopsia huku wengine wakipata kiwaa.

Aura ya kihisia ni aura ya pili kati ya aura zinazotokea mara nyingi huku ikitokea kwa asilimia 30-40 ya watu wenye aura. Mara nyingi hisia kama ya kudungwa kwa vipini- na-sindano huanzia kwa upande mmoja wa mkono kisha kuenea hadi sehemu ya pua na kinywa kwa upande uo huo. Kufa ganzi mara nyingi hutokea baada ya hisia ya mwasho na kupoteza hisia za ubinafsia. Dalili zingine za awamu ya aura ni pamoja na: tatizo la kuzungumza, hisia za dunia kuzunguka, na mara nadra matatizo ya kimwendo. Kuwepo kwa dalili za kimwendo huashiria kuwa kuna kipandauso cha hemiplejia na udhaifu kudumu kwa zaidi ya saa moja, tofauti na aura zingine. Ni nadra kwa aura kudumu bila kufuatiwa na maumivu ya kichwa, na hujulikana kama kipandauso kimya.

Awamu ya maumivu

Kwa kawaida maumivu ya kichwa huathiri upande mmoja, hudunda, na ukali wake huwa wa kadri hadi mkali mno. Kwa kawaida hali hii huja polepole na huzidishwa kwa kujishugulisha sana.Hata hivyo, kwa visa zaidi ya asilimia 40, maumivu yanaweza kuathiri pande zote mbili huku maumivu ya shingo yakihusishwa na hali hii. Maumivu ya pande zote mbili huwa hasa kwa watu walio na kipandauso bila aura. Maumivu yasiyo ya kawaida yanaweza kutokea hasa kwa sehemu ya nyuma au ya juu ya kichwa. Kwa kawaida, maumivu hudumu kwa saa 4 hadi 72 kwa watu wazima ingawa katia watoto mara nyingi yanadumu kwa kipindi kisichozidi saa 1 . Marudio ya kukabiliwa na hali hii hubadilika mara kwa mara, kutoka visa vichache maishani hadi visa kadhaa kwa wiki, huku wastani ukiwa ni mara moja kwa mwezi .

Mara nyingi maumivu huandamana na kichefuchefu, kutapika, usikivu dhidi ya mwanga, usikivu dhidi ya sauti, usikivu dhidi ya harufu , uchovu na kukereka. Kwa, kipandauso cha basila, kipandauso chenye dalili za kinurolojia zinazohusiana na shina la ubongo au chenye dalili za kinurolojia kwenye pande zote za mwili,athari za kawaida zikiwa ni pamoja na: kuhisi kana kwamba dunia inazunguka, wepesi wa kichwan, na kuwa na utatanishi. Kichefuchefu hutokea kwa takriban watu asilimia 90, huku takriban thuluthi moja wakitapika. Hivyo basi, watu wengi hutafuta chumba kitulivu chenye giza. Dalili zingine ni pamoja na: kiwaa, kufungana pua, kuhara, kukojoa kila mara, kuparara, au kulowa jasho. Uvimbe au uchungu kwenye ngozi ya sehemu ya juu ya kichwa, na shingo kuwa ngumu ni hali zinazoweza kutokea Dalili husika huwa nadra kwa watu wazee.

Dalili za baadaye

Athari za kipandauso zinaweza kudumu kwa siku kadhaa baada ya maumivu makuu kuisha; hii huitwa dalili za baadaye za kipandauso. Watu wengi hukisia kuwa na hisia za mwasho kwa eneo lililoathiriwa na kipandauso na wengine kusema wana ulemavu wa kifikra kwa siku chache baada ya maumivu ya kichwa. Mgonjwa anaweza kuchoka au kupata 'maruerue' na maumivu ya kichwa, matatizo ya kiutambuzi, dalili za tumbo na utumbo, mabadiliko ya kihisia, na udhaifu.Kwa muhtasari mmoja, " Baadhi ya watu hupata hisia ya uchangamfu usio wa kawaida baada ya kukabiliwa na hali hii, huku wengine wakiripoti kupata mfadhaiko na unyonge wa mwili."

Kisababishi

Kisababishi halisi cha kipandauso hakijulikani Hata hivyo, kipandauso hukisiwa kuhusiana na mchanganyiko wa vipengele vya kimazingira na kijeni. Hali hii hurithiwa kifamilia - kwa thuluthi mbili ya visa na hutokea nadra kufuatia hitilafu moja ya kijeni.Baadhi ya hali za kisaikolojia yanayohusishwa ni pamoja na: mfadhaiko, [[wasiwasi na maradhi ya hisia mseto as are many biological events or triggers.

Jenetikia

Utafiti wa mapacha umedhihirisha uwezekano wa asilimia 34 hadi 51 wa vipengele vya kijeni kuathiri uwepo wa maumivu ya kichwa yanayohusiana na kipandauso. Uhusiano huu wa kijeni ni mkuu zaidi kwa watu wenye kipandauso chenye aura kuliko wale wasio.Kuwepo kwa aina maalum za jeni huongeza hatari kutoka kiasi kidogo hadi wastani.

Hitilafu ya jeni moja inayopelekea kipandauso ni ya nadra. Mojawapo ya hali hizi hujulikana kama kipandauso cha familia cha hemiplejia, aina ya kipandauso chenye aura]] ambacho hurithiwa kwa njia ya autosomia kuu Hitilafu hizi zinahusiana na aina za miundo ya jeni za protini zinazohusika kwa usafirishaji wa ioni. Hitilafu nyingine inayosababisha kipandauso ni sindromu ya CADASIL au ateriofati yenye ukuu wa autosomia na yenye inifarakti na lukoensefalopathia chini ya koteksi.

Vichochezi

Kipandauso kinaweza kuanzishwa na vichochezi, huku baadhi ya watu wakiripoti kuwa hali hii huwa hatari tu kwa visa vichache na wengine kwa visa vingine. Vitu vingi vimedaiwa kuwa vichochezi, ingawa uzito na umuhimu wa madai hayo haujadhibitishwa.>Kichochezi kinaweza kutokea na kudumu hadi saa 24 kabla ya dalili kuanza.

Vipengele vya kifiziolojia

Vichochezi vilivyotajwa mara nyingi ni mfadhaiko, njaa na uchovu (vichochezi hivi huchangia kutokea kwa maumivu ya kichwa yanayotokana na mahangaiko).]] Kuna uwezekano mkubwa wa kipandauso kutokea siku zinazokaribiana na hedhi.Athari zingine za kihomoni, kama vile hedhi ya kwanza, na matumizi ya tembe za kuzuia mimba, ujauzito, muda unaokaribia ukomohedhi naukomohedhi pia huhusishwa na kipandauso. Athari hizi za kihomoni huhusika pakubwa kwa kutokea kwa kipandauso kisicho na aura. Kwa kawaida kipandauso hakitokei kwa ya pili na na trimesta ya tatu au kufuatia ukomohedhi.

Vipengele vya kilishe

Utafiti kuhusu vichochezi vinavyohusu lishe umegundua kuwa ushahidi hutegemea utathmini dhahania na hautilii maanani kuthibitisha au kukanusha kichochezi chochote. Kuhusu vipengele maalum, hakuna ushahidi kuhusu jinsi tairamini inavyoathiri kipandauso nayo monosodium glutamate (MSG) imeripotiwa mara nyingi kuwa kichochezi cha kilishe, mara nyingi ushahidi hauafikiani na wazo hili.

Vipengele vya kimazingira

Vichochezi kwa mazingira ya ndani na nje ni thibithisho kuwa ushahidi wa kijumla ilikuwa duni, lakini ulishauri kuwa watu wenye kipandauso wachukue hatua za kuzuia kipandauso zinazohusiana na ubora wa hewa ya ndani na mwangaza. Wazo kuwa vichochezi hivi hupatikana mara nyingi kwa watu werevu zaidi si kweli.

Pathofisiolojia

Kipandauso 
Animation of cortical spreading depression

Kipandauso kinaaminiwa kuwa tatizo la neva na mishipa pamoja na ushahidi unaothibitisha utaratibu wa kipandauso kuanzia ndani ya ubongo kisha kuenea hadi kwenye mishipa ya damu. Baadhi ya watafiti huamini kuwa taratibu za kiniuronihuchangia pakubwa, huku wengine wakiamini kuwa mishipa ya damu huchangia zaidi. Watafiti wengine huhisi kuwa athari zote mbili huhusika pakubwa. Kiwango kikubwa cha niurotransmita serotonini, pia inayojulikana kama 5-hydroxytryptamine, inaaminiwa kuhusika.

Aura

Mfadhaiko unaosambaa kwenye koteksi au mfadhaiko wa kusambaa kwenye Leão ni mchipuko ghafla wa shughuli za kineva unaofuatiwa na kipindi kisicho na shughuli, hali inayopatikana kwa twatu wenye kipandauso chenye aura. Kuna maelezo mengi kuhusu kutokea kwa hali hii, ikiwa ni pamoja na uchochezi wa kipokezi cha NMDA, hali inayopelekea kalisi kuingia kwenye seli. Baada mchipuko huu wa ghafla wa shughuli, mtiririko wa damu kuelekea koteksi ya serebramu kwa sehemu iliyoathirika hupungua kwa muda wa saa mbili hadi sita. Inaaminiwa kuwa uondoaji wa kingamizi unapoelekea kwenye sehemu ya chini ya ubongo, neva za uchungu kichwani na shingoni huchochewa.

Maumivu

Utaratibu halisi wa maumivu ya kichwa ambayo hutokea wakati wa kipandauso haujulikani.. Ushahidi unaafiki jukumu la kimsingi wa sehemu za mfumo mkuu wa neva (kama vile shina la ubongo na diensefaloni) huku utafiti mwingine ukiafiki jukumu la uchochezi kwenye sehemu za pembeni( kama vile kupitia kwaneva za hisia zinayozingira mishipa ya damuya kichwa na shingo). Mishipa inayoweza kuathirika ni pamoja na: ateri za dura, ateri ya pia na ateri zilizo nje ya fuvu kama zile za ngozi ya kichwa. Jukumu la kupanuka kwa ateri, hususan zilizoko nje ya fuvu inaaminiwa kuwa muhimu

Utambuzi

Utambuzi wa kipandauso hutegemea ishara na dalili. upigaji pichahufanywa mara nyingi ili kubainisha visababishi vingine vya maumivu ya kichwa. Inaaminika kwamba idadi kubwa ya watu wenye hali hii hawajatambuliwa.

Utambuzi wa kipandauso bila aura unaweza kufanyika kwa kufuata kanuni ya "5, 4, 3, 2, 1; kulingana na International Headache Society,,:

  • Kukabiliwa na kipandauso chenye aura mara tano au zaidi—, makabiliano mawili yanatosha kufanya utambuzi.
  • Kipandauso kudumu kwa saa nne hadi siku tatu
  • Mawili au zaidi ya yafuatayo:
    • Maumivu ya upande mmoja (yanayoathiri nusu ya kichwa);
    • Kudundadunda;
    • "Maumivu ya kadri hadi makali";
    • "Inayoongezeka kuwa chungu au inayotatiza shughuli za kila siku za mwili ."
  • Moja au zaidi ya haya:
    • Kichefuchefu na/au kutapika;
    • Usikivu dhidi ya mwanga (fotophobia) na usikivu dhidi ya sauti (fonofobia)

Ikiwa mtu ataweza kukumbwa na hali mbili kati ya hizi: fotophobia, kichefuchefu, au kutoweza kufanya kazi/kusoma kwa siku moja, kuna uwezekano wa kuwa na kipandauso . Kwa watu wenye hali nne kati ya hali tano zifuatazo: maumivu ya kichwa ya kudundadunda, maumivu kudumu kwa saa 4–72, maumivu kwa upande mmoja wa kichwa, kichefuchefu au dalili zinazotatiza maisha ya mtu, uwezekano wa kipandauso ni asilimia 92 Kwa watu wenye dalili hizi chini ya tatu uwezekano ni asilimia 17

Uainishaji

Mwaka 1988 ndio wakati wa kwanza kwa kipandauso kuainishwa kwa kina. Shirika laInternational Headache Society hivi karibuni walibadilisha uainishaji wao mwaka wa 2004.Kulingana na uainishaji huu, kipandauso ni maumivu ya kimsingi ya kichwa yanayoandamana na aina ya maumivu ya kichwa]] yenye [[wasi wasi na maumivu ya kichwa mbalimbali na mengineyo.

Kipandauso kimeainishwa kwa vitengo saba (baadhi ya vitengo hivi vimegawanywa zaidi kwa vijitengo vingi):

  • Kipandauso bila aura au "kipandauso cha kawaida", kinahusisha maumivu ya kichwa yasiyoandamana na aura
  • Kipandauso chenye aura au "kipandauso maalum", kinahusisha maumivu ya kichwa yanayoandamana na aura. Kwa mara nadra, aura inaweza kutokea bila maumivu ya kichwa au kuandamana na maumivu ya kichwa yasiyohusika na kipandauso. Vijitengo vingine viwili ni kipandauso cha familia na kipandauso mtawanyiko, ambapo mtu anapata kipandauso chenye aura na kinachoandamana na udhaifu wa kimwendo. Ikiwa jamaa kwa familia amewahi kupata hali hii, basi itaitwa "kipandauso cha kifamilia"; la sivyo kipandauso "mtawanyiko". Aina nyingine ni kipanduso cha aina ya basila , ambapo maumivu ya kichwa na aura huandamana na ugumu wa kuongea, hisia ya kuwa dunia inazunguka, kelele kama king'ora maskioni au dalili zingine nyingi zinazohusiana na shina la ubongo, lakini sio udhaifu wa kimwendo. Awali, aina hii iliaminiwa kufuatia spazimu ya ateri ya basila, ateri inayosafirisha damu kwenye shina la ubongo.
  • Sindromu ya utotoni ambayo kwa kawaida ni kitangulizi cha kipandauso ni pamoja na msururu wa kutapika (vipindi vichache vya kutapika sana), kipanduso cha fumbatio (maumivu ya fumbatio, mara nyingi huandamana na kichefuchefu), na kisulisuli hafifu cha utotoni kinachotokea ghafla (kukabiliwa na kisulisuli mara chache).
  • Kipandauso cha retinali kinajumuisha maumivu ya kichwa yanayoandamana na kutoona vizuri au hata upofu wa jicho moja kwa siku chache.
  • Matatizo ya kipandauso ni maumivu ya kichwa na/au aura ambayo hudumu kwa muda mrefu au kutokea mara nyingi kuliko inavyokuwa kawaida au kuandamana na kifafa au kidonda kwenye ubongo.
  • Uwezekano wa kipandauso huashiriwa na hali zilizo na baadhi ya sifa za kipandauso, lakini hakuna ushahidi tosha wa kutambua kwa hakika kama ni kipanduso (wakati kuna matumizi ya dawa kupita kiasi kwa mfululizo).
  • Kipandauso sugu ni tatizo kufuatia vipandauso, na ni maumivu ya kichwa yanayothibitisha mbinu ya kiutambuzi wa maumivu ya kichwa yanayohusiana na kipandauso na hujirudia baada ya muda mrefu. Hususan, siku 15 au zaidi kwa mwezi kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu.

Kipandauso cha fumbatio

Utambuzi wa kipandauso cha fumbatio umekumbwa na utata. Baadhi ya utafiti umeonyesha kuwa visa vya kujirudia ya maumivu ya fumbatio yanaweza kuwa ni aina ya kipandauso Au angalau ni kitangulizi cha kipandauso Visa hivi yanaweza au kutoweza kufuatiwa na dalili zinazoashiria kipandauso na kwa kawaida hudumu kwa dakika chache hadi saa kadhaa Mara nyingi, visa hivi hutokea kwa watu wenye historia ya kipandauso maalumu kwa mtu binafsi au kwa familia.Sindromu zingine zinazoaminika kuwa viashiria ni pamoja na:sindromu ya msururu wa kutapika na kutokea kwa ghafla kwa kisulisuli hafifu cha utotoni .

Dalili za kifisiolojia

Hali zingine zinazoweza kuleta dalili sawa na maumivu ya kichwa ya kipandauso ni pamoja na: maambukizi ya ateri ya panja, maumivu ya kichwa upande mmoja, klaukoma kali, meningitisi na kuvuja damu kwenye sehemu ya chini ya araknoidi ya ubongo. Kwa kawaida maambukizi ya ateri ya panja hutokea kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 50 na huandamana na uchungu kwa panja, maumivu ya kichwa ya upande mmoja hutambulika kwa kufungana kwa pua moja, machozi na maumivu makali kwa obiti obiti, klaukoma kali huhusika na matatizo ya kuona, meningitisi na homana kuvuja damu kwenye sehemu ya chini ya araknoidi ya ubongo. Maumivu ya kichwa kutokana na wasiwasi kwa kawaida hutokea kwa pande zote mbili, hayadhoofishi wala kulemaza sana.

Kinga

Matibabu ya kuzuia kipandauso ni pamoja na: dawa, lishe mbadala, kubadilisha mienendo ya maisha, na upasuaji. Kinga hupendekezwa kwa watu wenye maumivu ya kichwa kwa zaidi ya siku mbili kwa wiki, wasioweza kutibika kwa dawa za kupunguza makali au wenye maumivu makali yasiyoweza kudhibitiwa.

Malengo ya hatua hizi ni kupunguza marudio, maumivu na/au muda wa kudumu wa kipandauso, na kuongeza ubora wa matibabu ya awali. Sababu nyingine ya kinga ni kuepuka maumivu ya kichwa yanayohusiana na matumizi ya dawa kupita kiasi. Jambo hili ni tatizo linalotolea mara nyingi na linaweza kusababisha maumivu makali ya kichwa kila siku.

Tiba

Matibabu ya kuzuia kipandauso yanakisiwa kuwa bora ikiwa yatapunguza visa au ukali wa kipandauso kwa asilimia 50 Miongozo huwa na yamkini viwango thabiti kwa kutathmini topiramate, divalproex/sodium valproate, propranolol nametoprolol kama dawa zilizo na kiwano cha juu zaidi cha ushahidi kuhusu matumizi ya matibabu ya kwanza| yanayopendekezwakwanza . Mapendekezo kuhusu ubora ulitofautiana kuhusu gabapentin. Timolol pia ni bora kwa kuzuia kipandauso na kupunguza makali na marudio yake huku frovatriptan ikizuia kipandauso kinachohusiana na hedhi Amitriptyline na venlafaxine vile vile ni bora. Botox imegunduliwa kuwa bora kwa watu wenye kipandauso cha kudumu wala sio wenye kipandauso cha muda tu.

Tiba mbadala

Kipandauso 
Petasites hybridus inayotolewa kwenye mizizi ya mti wa (butterbur) imedhibitishwa kuwa bora kwa kuzuia kipandauso.

Akupancha ni matibabu bora ya kipandauso. Matumizi ya akupancha "halisi" siyo bora kuliko matumizi ya akupancha "bandia". Hata hivyo, aina zote zimegunduliwa kuwa bora kuliko utunzanji kidesturi, kwani zinaandamana na mathara machache zaidi kuliko matumizi ya dawa ya profilaktiki. Tibamwili, tibamaungo, kupapasa na kupumzika huwa bora sawa na matumizi ya dawa ya propranolol au topiramate kwa kuzuia maumivu ya kichwa yanayohusiana na kipandauso; hata hivyo mbinu iliyotumika kwa utafiti huu ina walakini. Kuna ushahidi ulio na tashwishi wa ubora wa: magnisiamu, enzaimu pacha Q10, riboflavin, vitamini B(12), and Fever-few, ingawa majaribio mwafaka yanafaa kufanywa ili kuthibitisha matokeo haya ya mwanzo.Matumizi ya butterbur yamethibitiwa kuwa bora kati ya matibabu mbadala.

Vifaa na upasuaji

Vifaa vya kimatibabu kama vile bayomwitiko na vichochea neva vina manufaa fulani kwa kuzuia kipandauso, hasa wakati dawa ya kuzuia kipandauso zimetumika bila kuzingatia maagizo kama vile kutumia dawa kupita kiasi. Bayomwitiko husaidia watu kufahamu baadhi ya parameta za kifiziolojia ili waweze kuzidhibiti na kujaribu kutulia, hivyo inaweza kuwa bora kwa kutibu kipandauso. Uchochezi neva hutumia vichocheaneva vya kubandika vilivyo sawa na viongozamwendo vya kutibu kipandauso sugu huku matokeo bora yakiwepo hasa kwa visa vya kipandauso kikali Upasuaji wa kipandauso , unaohusu kugandamua neva fulani kwa sehemu ya kichwa na shingo, inaweza kuwa chaguo kwa watu ambao afya yao haijaimarika kufuatia matibabu mengine.

Udhibiti

Kuna njia tatu kuu za matibabu: kuepuka vichochezi, kudhibiti dalili kali za ghafla na kuzuia kwa kutumia dawa. Dawa ni bora ikiwa itatumika punde tu mtu anapokabiliwa na hali hii. Marudio ya kutumia dawa mara nyingi husababisha maumivu ya kichwa yanayohusiana na matumizi ya dawa kupita kiasi na maumivu ya kichwa huzidi kuwa makali na kutokea mara nyingi zaidi. Hii inaweza kutokea kwa triptani, ergotaminesna vitoa maumivu hasa vya aina ya narkotia.

Viondoa maumivu

Matibabu ya kwanza yanayopendekezwa kwa watu wenye dalili zisizo kali hadi za wastani ni vitoa maumivu vya kawaida dawa ya inflamesheni isiyo na steroidi au mchanganyiko wa acetaminophen, asidi ya asitilsalikiliki na kafeni. Dawa kadhaa za kutibu inflamesheni zisizo na steroidi zimetambulika kuwa bora. Ibuprofen imegunduliwa kupunguza maumivu kikamilifu kwa takriban nusu ya watu wanaoitumia Diclofenacimethibitiwa kuwa bora pia

Aspirin inaweza kupunguza maumivu wastani ya kipandauso hadi yaliyo makali huku ikiwa na ubora sawa na sumatriptan. Ketorolac inapatikana kwa muundo wa kudungia mishipani Paracetamol (pia inayojulikana kama acetaminophen), aidha ikiwa pekee au ikiwa imechanganywa na metoclopramide ni tiba nyingine yenye madhara machache. Kwa ujauzito, acetaminophen na metoclopramide huaminika kuwa dawa salama na bora zaidi hadi trimesta ya tatu ya ujauzito.

Triptani

Triptani, kama vile sumatriptan, ni dawa bora ya kutibu maumivu na kichefuchefu hadi asilimia 75 ya watu. Dawa hizi hupendekezwa kutumika mwanzoni kwa watu wenye maumivu ya wastani hadi makali au kwa watu wenye dalili hafifu zisizotibika kwa vitoa maumivu vya kawaida. Njia za kutumia dawa hizi ni pamoja na kumeza, kudungia, kunyunyisia puani, na kumumunya. Kwa jumla, triptani zote zinaonekana kuwa bora huku zikiwa na madhara sawa. Hata hivyo, watu binafsi wanaweza kuafikiana na dawa maalum. Madhara mengi huwa si makal, kama vile wekundu usoni; ingawa, visa vichache vya iskemia ya miokadiumu vimeripotiwa. Hivyo basi dawa hizi hazipendekezwi kwa watu wenye magonjwa ya mfumo wa moyo na mishipa. Kwa historia, dawa hizi hazipendekezwi kwa watu wenye kipandauso cha basila, ingawa hakuna ushahidi maalum wa hatari unaothibitisha tahadhari hii. Dawa hizi hazipelekei uraibu wowote lakini zinaweza kusababisha maumivu ya kichwa yanayohusiana na matumizi ya dawa kupita kiasi hasa zikitumiwa kwa zaidi ya siku 10 kwa mwezi.

Ergotamini

Ergotaminina dihidroergotamini ni aina ya dawa za kitambo ambazo zingali zinapendekezwa kutumika kutibu kipandauso, za hivi punde zikiwa na muundo wa kunyunyisia pua na kudungia. Dawa hizi zimethibitishwa kuwa bora sawa na triptani, ni zaa bei nafuu zaidi, na huwa na madhara makali ambayo kawaida ni hafifu. Dawa hizi ni chaguo bora zaidi kwa watu wenye visa vikali ya kipandauso.

Dawa nyingine

Metoclopramide ya kudungia mishipani au lidocaineya kuingizia puani ni chaguo zingine zilizoko. Metoclopramide inapendekezwa kwa watu wanaoletwa hospitalini ili kupata usaidizi wa dharura. Kipimo kimoja cha dexamethasoneya kudungia mishipani kikiongezwa kwenye tiba iliyoafikiwa ya kipandauso huhusika kwa kupunguza kurejea kwa maumivu ya kichwa kwa asilimia 26 kwa saa 72 zinazofuata. Njia ya kutibu mfululizo wa maumivu ya kichwa yanayohusiana na kipandauso kwa kutumia kunyoosha uti wa mgongo haina ushahidi wowote. Inapendekezwa kuwa dawa ya opioid na barbiturate isitumike

Prognosisi

Prognosisi ya muda mrefu kwa watu wenye kipandauso hubadilika mara kwa mara. Watu wengi wenye kipandauso hupoteza wakati mwingi wa kufanya kazi kufuatia ugonjwa huu. Hata hivyo, kwa kawaida hali hii si hatari sana na haihusishwi na kuongezeka kwa hatari ya kifo. Ugonjwa huu una mikondo minne mikuu: dalili kutoweka kabisa, dalili kuendelea huku zikipunguka wakati unapopita, dalili kuendelea kwa kiwango sawa na ukali uo huo au makabiliano kuzidi kuwa mabaya na kujirudia mara nyingi zaidi.

Kipandauso chenye aura huonekana kuwa hatari yakiharusi ya iskemia doubling the risk.Kuwa kijana, mtu wa jinsia ya kike, kutumiavizuia mimba vyenye homoni na kuvuta sigara huongeza hatari ya kupata ugonjwa huu.. Pia hatari hii huonekana kuwa na uhusiano na kupasuka kwa ateri ya seviksi. Kipandauso bila aura hakionekani kuwa kipengele.. Uhusiano wa hali hii na matatizo ya moyo sio wazi, huku utafiti mmoja ukiafiki uhusiano huo. Kwa ujumla, kipandauso hakionekani kuongeza hatari ya kufa kufuatia kiharusi au ugonjwa wa moyo. Matibabu ya kipandauso kwa wenye kipandauso chenye aura yanaweza kuzuia kiharusi husika.

Epidemolojia

Kipandauso 
Disability-adjusted life year for migraines per 100,000 inhabitants in 2004
     no data      <45      45–65      65–85      85–105      105–125      125–145
     145–165      165–185      185–205      205–225      225–245      >245

Kote ulimwenguni, kipandauso huathiri zaidi ya asilimia 10 ya watu Kule Marekani, takriban asilimia 6 ya wanaume na asilimia 18 ya wanawake hupata kipandauso kila mwaka huku wakiwa na hatari ya daima ya asilimia 18 na 43 mtawalia. Barani Uropa, kipandauso huathiri asilimia 12–28 ya watu maishani mwao huku takriban asilimia 6–15 ya wanaume wazima na asilimia 14–35 ya wanawake wazima wakipata angalau tukio moja kila mwaka. Kima cha kipanduso ni chini kiasi barani Asia na Afrika ikilinganishwa na nchi za Magharibi. Kipandauso sugu hutokea kwa takriban asilimia 1.4 ya watu hadi 2.2.

Kipandauso 
Visa vya ugonjwa wa kipandauso kwa umri na jinsia

Takwimu hizi hutofautiana sana kwa umri: mara nyingi zaidi, kipandauso huanza kati ya umri wa miaka 15 na 24 na hutokea mara nyingi kwa watu wenye umri wa miaka 35 hadi 45. Kwa watoto, takriban asilimia 1.7 ya watoto wenye umri wa miaka 7 na asilimia 3.9 kwa wale wa kati ya miaka 7 na 15  wana kipandauso, huku hali hii ikitokea mara nyingi kwa wavulana kabla ya kubalehe. Wakati wa kubaleghe, kipandauso hutokea mara nyingi kwa wanawake na hali hii huendelea maishani, ikitokea mara mbili zaidi kwa wanawake wazee kuliko wanaume. Kipandauso bila aura hutokea mara nyingi zaidi kwa wanawake kuliko kipandauso chenye aura, ingawa aina hizi mbili hutokea kwa kiwango sawa kwa wanaume.

Kwa kipindi kilichokaribia ukomohedhi mara nyingi dalili huzidi kabla ya kupunguka ukali. Huku dalili zikitokomea kwa takriban thuluthi mbili ya wazee, dalili hizi hudumu kwa kati ya asilimia 3 na 10.

Historia

Kipandauso 
The Head Ache, George Cruikshank (1819)

Maelezo ya mwanzo ya yaliyozingatia kipandauso yamo kwa mafunjo ya Eber, yaliyoandikwa takriban mwaka wa 1200 BCE kwa kale za Misri Kwa mwaka wa 200 BC, maandishi kutoka kwa Shule ya madaktari ya Hippocrates yalieleza aura inayohusiana na kuona inayotokea kabla ya maumivu ya kichwa na kupata nafuu kidogo kufuatia kutapika.

Kipandauso 
A trepanated skull, from the Iron age. Mzunguko wa shimo kwa fuvu la kichwa unazingirwa na ukuaji wa tishu gumu kama mifupa kuashiria kuwa mtu huyo alipona baada ya upasuaji.

Maelezo ya karneya pili ya Aretaeus of Cappadocia yaliainisha maumivu ya kichwa kwa aina tatu: sefalejia, sefalea na heterokrania. Galen wa Pergamon alitumia neno hemikrania (nusu ya kichwa), ambapo neno kipandauso hatimaye lilikopwa. Galen pia alipendekeza kuwa maumivu huanzia kwenye meninjesi na mishipa ya damu kichwani.Hapo awali, kipanduso kilikuwa kimeainishwa kwa aina mbili zinazotumika hata sasa - kipandauso chenye aura(migraine ophthalmique) na kipanduso bila aura (migraine vulgaire) kwa mwaka wa 1887 na Louis Hyacinthe Thomas Mkutubi Mfaransa.

Utoboaji, yaani kutoboa tundu kwa hiari kwenye fuvu la kichwa, ulifanyika hata mwaka wa 7,000 BCE. Huku baadhi ya watu wakipona, wengi wao huenda walikufa kufuatia maambukizi. Tendo hili liliaminika kufanya kazi kwa kupitia "kufungulia mapepo watoroke". Kwa karne ya 17, William Harvey alipendekeza utoboaji tundu kama matibabu ya kipandauso.

Huku majaribio mengi ya matibabu ya kipandauso yakifanyika, ni mpaka mwaka 1868 ambapo matumizi ya dutu ambazo hatimaye ziliweza kuwa bora yalianza. Dutu hizi nierogoti ya kuvu ambapo dawa ya ergotamine ilitolewa kwa mwaka wa 1918. Methysergideilitolewa mwaka wa 1959, na triptani ya kwanza, sumatriptan, kutolewa mwaka wa 1988. Kufuatia utafiti mwafaka, dawa bora za kukinga kipandauso zilipatikana na kuthibitishwa kwa karne ya 20.

Jamii na Utamaduni

Kipandauso ni chanzo kikuu cha gharama ya kimatibabu na kukosa matokeo mema kazini. Imekadiriwa kwamba kipandauso ni ugonjwa wenye gharama kali mno kati ya magonjwa mengine yanayohusika na mfumo wa neva kwa Jumuiya ya Ulaya, ukigharimu zaidi ya bilioni €27 kwa mwaka Huko Marekani gharama ya moja kwa moja imekadiriwa kuwa dola bilioni 17.. Takriban asilimia 10 ya gharama hii ni ya triptani. Gharama isiyo ya moja kwa moja ni takriban dola bilioni 15 za Marekani, ambapo kukosa kazi ni kipengele kikuu. Ubora wa wanaoweza kuendelea na kazi licha ya kuwa na kipandauso hupunguka kwa takriban theluthi moja. Mathara mabaya mara nyingi pia hutokea kwa familia ya mtu.

Utafiti

Peptidi inayohusiana na jeni ya kidhibiti kalisi imethibitiwa kuhusika kwa pathojenesisi ya maumivu yanayohusiana na kipandauso. Vipokezi pinzani vya peptidi inayohusiana na jeni ya kidhibiti kalisi, kama vile olcegepant na telcagepant, vimechunguzwa kwa utafiti wa vitro] na kwa utafiti wa kiafya ya matibabu ya kipandauso. Mwaka wa 2011, kampuni ya Merck ilisitisha awamu ya III ya majaribio ya kimatibabu ya uchunguzi wao wa dawa ya telcagepant.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

Kipandauso Ishara na daliliKipandauso KisababishiKipandauso PathofisiolojiaKipandauso UtambuziKipandauso KingaKipandauso UdhibitiKipandauso PrognosisiKipandauso EpidemolojiaKipandauso HistoriaKipandauso Jamii na UtamaduniKipandauso UtafitiKipandauso TanbihiKipandauso MarejeoKipandauso Viungo vya njeKipandausoDaliliMaumivu ya kichwaMfumo wa neva

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Millard AyoFonimuMkoa wa SingidaAla ya muzikiJangwaMaumivu ya kiunoHistoria ya WasanguMohamed HusseinUwanja wa Taifa (Tanzania)Ngw'anamalundiKata za Mkoa wa MorogoroKiambishiMgawanyo wa AfrikaMkoa wa RuvumaHalmashauriWachaggaOrodha ya miji ya TanzaniaTendo la ndoaWakaguruMbossoMbooMagonjwa ya machoMisimu (lugha)PombooMkanda wa jeshiMapambano ya uhuru TanganyikaMaigizoMlongeKipimajotoLugha ya taifaMpira wa kikapuUfisadiMatumizi ya lugha ya KiswahiliMkopo (fedha)Vita ya uhuru wa MarekaniAfyaDemokrasiaWilaya ya IlalaNileDodoma MakuluMwanza (mji)Simba S.C.Asili ya KiswahiliUfilipinoOrodha ya kampuni za TanzaniaJava (lugha ya programu)Bagamoyo (mji)Mashuke (kundinyota)MadhehebuUtumwaBarua pepePhilip Isdor MpangoKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiMfumo wa JuaJumuiya ya MadolaSayansiSarufiSteven KanumbaIsimuTanganyika (ziwa)MatendeKina (fasihi)Orodha ya milima ya TanzaniaKibodiZama za MaweOksijeniAbedi Amani KarumeKitunda (Ilala)Manchester United F.C.FananiWema Sepetu🡆 More