Zama Za Mawe

Zama za Mawe (pia: Mhula wa mawe) zilikuwa kipindi kirefu cha historia ya awali ya binadamu.

Jina hilo linatokana na kwamba wakati huo watu walitumia vifaa vya mawe kwa shughuli zao za kila siku.

Zama Za Mawe
Mawe yaliyochongwa kuwa na kona kali kwa matumizi kama kisu.
Zama Za Mawe
Mtu wa zama za mawe akikata mti.

Utamaduni wa watu mwanzoni mwa zama za mawe

Mwanzoni watu walikuwa wawindaji-wakusanyaji, yaani walidumisha maisha yao kwa kukusanya matunda, mizizi na kuwinda wanyama.

Kwa umbile na akili yake binadamu ana uwezo wa kuwinda wanyama wakubwa kama chakula na kutumia ngozi yao kama mavazi ya kujikinga dhidi ya baridi.

Lakini meno na makucha yake hayafai kupasua ngozi ya mnyama mkubwa au kukata nyama yake vipande-vipande akitaka kubeba windo hadi mahali penye familia yake. Vilevile makucha hayafai sana kuchimba mizizi kwa chakula.

Hapo binadamu aliweza kutumia vitu vinavyopatikana kiasili katika mazingira: jiwe lenye kona kali, tawi la mti lenye ncha kali pamoja na vipande vya mifupa. Hivyo vyote vilisaidia shughuli za kuchimba, kupasua na kukata.

Kuna mabaki mengi ya mawe yaliyochongwa kwa matumizi kama vifaa na mabaki hayo yamekuwa msingi wa jina "zama za mawe". Vifaa hivyo na mabadiliko yake vinaonyesha maendeleo katika maisha ya binadamu na kuongezeka kwa uwezo wake wa kupambana na mazingira yake.

Kwa hiyo ni kipindi cha matumizi ya mawe yaliyochongwa kuwa vifaa baada ya kipindi ambako watu walitumia fimbo tu au mawe katika hali asilia na kabla ya kipindi ambapo watu walielewa namna ya kutumia metali.

Zama Za Mawe 
Kifaa cha mawe sahili - zama za mawe ya kale
Zama Za Mawe 
Shoka la mkononi - bapa pande mbili (mwishoni mwa Zama za mawe ya kale) - inaonyeshwa kutoka mitazamo mbalimbali

Vipindi vya zama za mawe

Wataalamu wa akiolojia wametambua ya kwamba vifaa vya mawe vinaonyesha tabia tofautitofauti.

  • Kuna vifaa sahili sana kama jiwe lililogongwa mara moja ili kipande kivunjike na ncha kali ipatikane.
  • Kuna pia vifaa vya mawe vinavyoonyesha maendeleo zaidi; vilifanyiwa kazi kwa siku kadhaa kiangalifu ili kunyoshwa, kung'arishwa na kutobolewa kwa kuweka pini.

Kutokana na tofauti kubwa katika hali ya vifaa vya mawe wataalamu wanaona ya kwamba wanaonyesha historia ndefu ya maendeleo ya teknolojia ya kushughulikia jiwe ambako watu walianza kwa vifaa sahili na kuendelea kujifunza zaidi na kuboresha matokeo ya juhudi zao.

Kwa hiyo wataalamu wengi wanatofautisha:

  • Zama za mawe za kale (pia: Zama za mwanzo za mawe)
  • Zama za mawe za kati (pia: Zama za kati za mawe)
  • Zama za mawe za mwisho (pia: Zama za mwisho za mawe)

Si tofauti katika ubora wa vifaa pekee, lakini kuna pia dalili nyingine zinazoonyesha ya kwamba watu walibadilisha maisha yao, namna ya kujipatia chakula na makazi.

Kila mtu aliweza kugonga jiwe dhidi ya jiwe hadi ncha kali ilipatikana. Lakini mashoka ya mawe yaliyohitaji siku za kazi makinifu yanaonyesha kuwepo kwa jamii iliyokuwa na mafundi wa pekee walioweza kunyosha ufundi wao wakilishwa na wengine ni pia dalili ya biashara iliyofanywa hasa tukikuta vifaa vya jiwe fulani katika maeneo ambako jiwe hili halipatikani kiasili.

Pamoja na matokeo mengine ya utafiti wa akolojia, kama vile mabaki ya makaburi, vyombo vya ufinyanzi, nyumba na vifaa vingine, wataalamu waliweza kupata picha ya undani zaidi kuhusu maisha na jamii ya watu wa zamani zile.

Zama Za Mawe 
Teknolojia ya kupunguza jiwe hadi kupata kisu chembamba - zama za mawe ya kati (Levallois)
Zama Za Mawe 
Matumizi ya ncha ya jiwe kwenye mkuki

Vifaa vya mawe

Zama za mawe ya kale

Vifaa vya kwanza vilikuwa mawe yaliyokatwa upande mmoja ili kuwa na kona kali moja. Hatuwezi kujua kwa uhakika tukiona jiwe la aina hii kama kama ilikuwa tokeo la mgongano wa mawe katika mkondo wa maji mtoni au kutokana na kuanguka kwa jiwe kutoka mlimani au kama jiwe limepigwa kwa kusudi kwa jiwe lingine kwa shabaha ya kupata kona kali. Lakini mawe haya yalifaa kutumiwa kwa kukata pia si vigumu kuvitengeneza.

Mifano ya kale kabisa ya mawe yaliyogongwa kwa mawe mengine kwa kusudi la kupata kona kali zimepatikana katika eneo la ziwa Turkana (leo nchini Kenya) yalitegenezwa miaka milioni 3.3 iliyopita.

Ngazi iliyofuata ni mawe yaliyofanyiwa kazi zaidi hadi kuwa "shoka la mkononi". Hapo jiwe la kufaa lilipigwa na kupunguzwa pande zote mbili hadi kuwa na bapa pande mbili. Sehemu ya juu ilibaki bila ukali kwa kuishikilia mkononi. Kuna mahali ambako mabaki mengi ya mashoka haya ya mkononi yamepatikana katika hali mbalimbali: mawe yaliyopigwa kiasi, mawe yaliyovunjika vibaya na kutupwa, vipande vidogo vilivyopasuliwa wakati wa kuipa shoka umbo lake na kadhalika. Mahali pale panatazamwa kama karakana au viwanda vya kutengeneza vifaa vya mawe. Mahali mashuhuri katika Afrika ya Mashariki ni bonde la Isimila (karibu na Iringa, Tanzania ya leo).

Zama za mawe ya kati

Kipindi hiki kinatazamwa kilianza miaka 300,000 iliyopita na kudumu hadi miaka 25,000 - 50,000 iliyopita.

Zama Za Mawe 
Mabamba makali ya mawe yamefungwa katika ubao wa mundu ya kukatia majani au mazao

Kipindi hiki kinaonyesha maendeleo ya teknolojia. Watu walianza kutumia pia vipande vidogo vikali vilivyopatikana wakati wa kupunguza jiwe. Vibanzi vikali vya mawe vilifungwa sasa kwenye pini ya ubao kwa gundi la miti. Kwa njia hii vifaa kama kisu, chusa au mundu vilipatikana.

Matatizo ya lugha ya "zama za mawe"

Zama za mawe zilikuwa vipindi virefu sana vya miaka elfu nyingi. Wataalamu wamegawanya zama hizo katika vipindi mbalimbali kama Zama za mawe za kale na Zama za mawe za kati. Tofauti hizo zinaonekana kuwa na msingi, lakini wataalamu wa siku hizi wanaona ya kwamba mgawanyo huu ulitazama zaidi historia ya Ulaya isiyolingana na historia ya sehemu nyingine za dunia.

Tatizo kuu ni kwamba ni kipindi cha teknolojia bila kuangalia pande nyingine za maendeleo ya kibinadamu.

Kwa mfano chuma hakikutumiwa huko Amerika hadi karne ya 16 na huko Pasifiki hadi karne ya 17. Hata hivyo jamii za Amerika kama Azteki au Wainka walikuwa na teknolojia nyingine mbalimbali na waliweza kudumisha miji mikubwa kushinda miji ya Ulaya ya wakati ule.

Basi, lugha ya "zama za mawe" imekuwa kawaida duniani na wataalamu wanaendelea kuitumia wakijua kasoro zake kwa sababu hadi sasa hakuna mawazo ya kufaa zaidi.

Picha

Marejeo

Kujisomea

Viungo vya nje

Zama Za Mawe 
Wiki Commons ina media kuhusu:
  • Giusepi, Robert A. (2000). "The Stone Age". History World International. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-02-22. Iliwekwa mnamo 22 February 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  • Kowalski, D.R. "Stone Age Hand-axes". AerobiologicalEngineering.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-03-17. Iliwekwa mnamo 22 February 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  • Kowalski, D.R. "Stone Age Habitats". AerobiologicalEngineering.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-03-17. Iliwekwa mnamo 22 February 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  • "PanAfrican Archaeological Association". Iliwekwa mnamo 28 February 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  • "Society of Africanist Archaeologists". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-17. Iliwekwa mnamo 3 March 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)
  • "The ASA". Association of Social Anthropologists of the UK and Commonwealth. 
Zama Za Mawe  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zama za Mawe kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Zama Za Mawe Utamaduni wa watu mwanzoni mwa zama za maweZama Za Mawe Vipindi vya zama za maweZama Za Mawe Vifaa vya maweZama Za Mawe Matatizo ya lugha ya zama za maweZama Za Mawe PichaZama Za Mawe MarejeoZama Za Mawe KujisomeaZama Za Mawe Viungo vya njeZama Za MaweBinadamuHistoria ya awaliJinaJiweKifaaShughuliSiku

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MandhariNahauMagonjwa ya machoVitenzi vishiriki vipungufuUislamuMkoa wa MtwaraMtandao wa kijamiiUtumwaRaiaMtiBarua pepeSemiMweziMkoa wa KageraBawasiriMatumizi ya LughaTabianchiKorea KusiniDaudi (Biblia)BahatiAli KibaSaratani ya mlango wa kizaziBinadamuMaarifaJumuiya ya MadolaMobutu Sese SekoSimbaVivumishi vya idadiTungo kiraiWahayaKalenda ya KiislamuVitenzi vishirikishi vikamilifuKupatwa kwa JuaJipuUfugajiMaadiliKukuNabii EliyaMkutano wa Berlin wa 1885Orodha ya wanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoFilomena wa RomaKilimoMpango wa BiasharaAfrikaTarcisius NgalalekumtwaMkojoJeshiWazaramoOrodha ya mito nchini TanzaniaNyumbaStadi za maishaMkoa wa ShinyangaIniDaktariUshairiLeopold II wa UbelgijiKoloniVidonge vya majiraNyati wa AfrikaWanyamweziVivumishi vya jina kwa jinaNyangumiKanuni ya Imani ya Nisea-KonstantinopoliJacob StephenTarakilishiTarafaMtawaVivumishi vya kuoneshaMichezo ya watotoMwigizajiDar es SalaamKiswahiliUti wa mgongo🡆 More