Mbegu

Mbegu ni sehemu ya tunda la mmea inayoweza kuendelea kuwa mmea mpya.

Mbegu ni njia ya kuzaliana kwa mimea mingi zinazoitwa kwa njia ya kibiolojia spermatophytina. Mbegu inaanzishwa ndani ya ua la mmea inaendelea kukua. Kuna mbegu ndogo sana ambazo ni vigumu kuona kwa jicho na mbegu kubwa kama nazi.

Mbegu
Mbegu za alizeti zimekauka lakini zinahitaji tu maji, halijoto ya kufaa na mwanga ili kuanzisha mmea mpya
Mbegu
Muundo wa ndani ya mbegu: a)ganda la mbegu b) lishe (endosperm) c) cotyledon au chanzo cha jani d) hypocotyledon au chanzo cha mzizi

Sehemu za mbegu

Huwa ndani yake na sehemu tatu

  • ganda la nje au testa
  • kitoto cha mmea yaani sehemu yenye chanzo cha majani na mizizi.
  • lishe ya kitoto cha mmea au "endosperm" ambayo ni hasa akiba ya wanga na sukari, mara nyingi pia protini na mafuta. Akiba hii inalisha mmea changa hadi imekuza mizizi na majani mabichi madogo inayoweza kuanza kazi ya usanisinuru.

Kulala kwa mbegu

Uwezo wa pekee wa mbegu za mimea tofauti na mimba ya wanyama ni ya kwamba kitoto kinaandaliwa ndani ya una lakini kinaacha kukua na kukauka. Katika hali kavu inaweza kukaa kwa muda, na mbegu kadhaa zimejulikana zilikaa miaka hata karne zikaweza kuchipuka hata baada ya muda mrefu.

Uwingi wa mbegu

Mimea inatofautiana sana kuhusu idadi za mbegu zinazoweza kutolewa. Lakini hata mimea yenye uwezo wa kutoa mbegu nyingi hazitoi kila mwaka; hii inategemea pia na hali ya hewa (ukame na baridi), magonjwa ya mimea na wadudu. Kwa mfano wataalamu walitazama sehemu ya msitu wa misonobari kwa kipindi cha miaka 20 wakaona ya kwamba mavuno ya mbegu yalikuwa kati ya 0 na milioni 5 za mbegu kwa hektari moja. Katika miaka sita mebgu zilitokea kwa wingi sana, katika miaka mitano chache sana, na miaka kumi miti ilikuwa na kiasi kizuri cha mbegu.

Mbegu na chakula

Mbegu huwa kati ya vyakula muhimu sana kwa wanadamu. Nafaka zote ni mbegu za aina za manyasi na kuwa chanzo kikii cha wanga kwa binadamu. Mbegu kama alizeti na jozi nyingi ni chanzo cha mafuta na protini.


Mbegu 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

Mbegu Sehemu za mbeguMbegu Kulala kwa mbeguMbegu Uwingi wa mbeguMbegu na chakulaMbeguMmeaNaziTundaUa

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

FamiliaMisemoSayansiMaishaLava Lava (mwimbaji)Dubai (mji)Maambukizi ya njia za mkojoShuleKitenzi kishirikishiDayolojiaTungo kishaziDoto Mashaka BitekoSaratani ya mlango wa kizaziUhakiki wa fasihi simuliziMusaMadiniMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaKito (madini)WachaggaOrodha ya maziwa ya TanzaniaUharibifu wa mazingiraMkoa wa TangaKisononoMfumo wa nevaMuziki wa hip hopMillard AyoInsha ya kisanaaIsraeli ya KaleHistoria ya BurundiMahakamaSerie AMashariki ya KatiAgano JipyaMnururishoDawatiMaana ya maishaMkoa wa KageraLingua frankaOrodha ya Magavana wa TanganyikaMatamshiMbooUyakinifuMaktabaWahayaUlumbiRejistaAmri KumiManispaaWaheheKipazasautiSimba S.C.Vivumishi vya idadiKumamoto, KumamotoMkoa wa DodomaShinikizo la juu la damuMbuyuUsultani wa ZanzibarLigi ya Mabingwa AfrikaUpinde wa mvuaMuunganoAngahewaTabataJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMgawanyo wa AfrikaKinyongaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaUandishi wa ripotiMkoa wa NjombeMatumizi ya LughaVielezi vya idadiViganoUbunifuMkoa wa ShinyangaMunguTenzi🡆 More