Mkoa Wa Mbeya

Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, ukipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa, mbali na mkoa mpya wa Songwe uliomegwa kutoka ule wa Mbeya upande wa magharibi mwaka 2016.

Mkoa wa Mbeya
Mahali paMkoa wa Mbeya
Mahali paMkoa wa Mbeya
Mahali pa Mkoa wa Mbeya katika Tanzania
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.750°S 32.750°E / -2.750; 32.750
Nchi Tanzania
Wilaya 7
Mji mkuu Mbeya
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Juma Zuberi Homera
Eneo
 - Jumla 35,954 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 2,343,754
Tovuti:  http://www.mbeya.go.tz/

Una Postikodi namba 53000.

Kabla ya kugawiwa kulikuwa na wilaya 9 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe, Kyela, Ileje, Mbozi, Chunya, Momba na Mbarali.

Tangu 2016 mkoa umekuwa na wilaya 7 za: Busokelo, Chunya, Kyela, Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Rungwe.

Kadiri ya sensa ya mwaka 2022 idadi ya wakazi ni 2,343,754 .

Jiografia

Kijiolojia mkoa wa Mbeya ni eneo la kukutana kwa mikono miwili ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki inayoendelea hapa katika ziwa Nyasa. Mkoa wa Mbeya inapakana pia na Ziwa Rukwa. Hasa milima yenye asili ya volkeno ya wilaya ya Rungwe imejaa maziwa ya kasoko.

Mito mikubwa ni Songwe na Kiwira. Chanzo cha mto Ruvuma kiko pia Mbeya katika tambarare ya Usangu.

Wilaya ya Rungwe ni eneo lenye mvua nyingi katika Tanzania, ila maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu..

Mkoa kwa ujumla ni mmojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.

Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu. Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu na waishio huko zaidi ni Wanyiha.

Vivutio vya kitalii

Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za ziwa Nyasa, Mlima ya Mbeya, Mlima ya Rungwe, Uwanda wa juu wa Uporoto, Uwanda wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii. Mkoa wa Mbeya una idadi ya vivutio vya kitalii ambavyo ni pamoja na:

  1. Ziwa Ngosi
  2. Ziwa Kisiba
  3. Hifadhi ya Taifa Kitulo
  4. Pori la Akiba Mpanga Kipengere
  5. Maporomoko ya maji (Kapologwe, Malamba, Kimani, Isabula)
  6. Vilele vya Mlima Mbeya, Mlima Loleza, Mlima Rungwe
  7. Safu za Milima ya Kipengere (Livingstone)

Majimbo ya bunge

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

  • Busokelo:mbunge ni Atupele Mwakibete(CCM)
  • Ileje:mbunge ni Janeth Mwamben(CCM)
  • Kyela:mbunge ni Ally Jumbe Mlaghila(CCM)
  • Lupa:mbunge ni Masache Njelu Kasaka(CCM)
  • Mbarali:mbunge ni Haroon Mullah Pirmohamed(CCM)
  • Mbeya Mjini:mbunge ni Tulia Ackson Mwansasu(CCM)
  • Mbeya Vijijini:mbunge ni Oran M. Njeza(CCM)
  • Mbozi:mbunge ni George Mwenisongole(CCM)
  • Momba:mbunge ni Condester Michael Sichalwe(CCM)
  • Rungwe:mbunge ni Sauli Henry Amon(CCM)
  • Songwe:mbunge ni Philipo Mulugo(CCM)
  • Tunduma:mbunge ni Mwakajoka Frank(Chadema)
  • Vwawa:mbunge ni Hasunga Ngailanga(CCM)

Waandishi toka mkoa wa Mbeya

Tazama pia

Viungo vya nje

Marejeo


Mkoa Wa Mbeya  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Mbeya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.

Tags:

Mkoa Wa Mbeya JiografiaMkoa Wa Mbeya Vivutio vya kitaliiMkoa Wa Mbeya Majimbo ya bungeMkoa Wa Mbeya Waandishi toka mkoa wa MbeyaMkoa Wa Mbeya Tazama piaMkoa Wa Mbeya Viungo vya njeMkoa Wa Mbeya MarejeoMkoa Wa Mbeya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Tamathali za semiKassim MajaliwaLuhaga Joelson MpinaTamthiliaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaJohn Raphael BoccoAli KibaUtafitiHekalu la YerusalemuNamba za simu TanzaniaMburahatiBahashaSakramentiMaktabaAina za udongoMkoa wa KataviMshororoIniKisimaMvuaViwakilishi vya kuoneshaImaniHistoria ya AfrikaUnyevuangaLigi Kuu Tanzania BaraKitenzi kishirikishiSheriaMsituBikiraMgawanyo wa AfrikaMichael JacksonMkoa wa SongweJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaUhifadhi wa fasihi simuliziVivumishi vya urejeshiUtumwaMkoa wa ArushaAlfabetiJakaya KikweteNg'ombeMickey MouseShetaniArusha (mji)Maji kujaa na kupwaMikoa ya TanzaniaMunguMashariki ya KatiBarabaraHussein Ali MwinyiKitunda (Ilala)Biashara ya watumwaMimba kuharibikaWabena (Tanzania)Tanganyika African National UnionIyumbu (Dodoma mjini)DamuHistoriaPhilip Isdor MpangoMkoa wa Unguja Mjini MagharibiSaidi Salim BakhresaMnyoo-matumbo MkubwaMeta PlatformsOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaDhamiraFB24 ApriliChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)UkongaLady Jay DeeIlluminati🡆 More