Ini

Ini ni kiungo cha mwili, hasa wa binadamu na wanyama wa hali ya juu.

Ini
Ini

Kazi

Ini linafanya kazi nyingi muhimu katika mwili:

  • Ini linatengeneza nyongo - ni kimiminika king'aavu cha njano chenye ukijani ambacho kinakwenda kwenye utumbo mwembamba ambacho kinasaidia kumeng'enya vyakula tunavyokula.
  • Ini linatunza glukosi tukila kisha linaweka kwenye damu wakati glukosi ya kwenye damu ikiwa ndogo. Hii hutokea wakati mtu anahisi njaa.
  • Ini linatuwezesha kuishi.
  • Ini linachukua protini na mafuta na kugeuza kuwa glukosi, hii ni muhimu wakati mtu hajala kwa muda mrefu.
  • Pia ini linatengeneza mafuta na kolestro
  • Ini humeng'enya vitu vingi kwenye damu.
  • Ini linatengeneza protini.

Magonjwa ya ini

Magonjwa ya ini yanaweza kumfanya mtu aumwe sana sababu ya kazi muhimu za kiungo hicho. Yapo magonjwa mengi ya ini. Watu ambao wana magonjwa mabaya ya ini huwa wanakufa; ili kuokoa maisha yao wenyewe itawabidi kupandikiziwa ini jingine. Hii ni kwamba, ini la mtu mwingine ambaye amekufa huamishwa kwa mtu mwingine kwa upasuaji. Upasuaji huo huwa na changamoto za kitaalamu lakini inaweza kuokoa uhai.

Dalili za magonjwa ya ini

Dalili za magonjwa ya ini hutokea kwa sababu ini halifanyi kazi inavyotakiwa:

Ini likishindwa kuyeyusha sumu na uchafu, hivi vitu vichafu vitakaa kwenye damu kwa muda mrefu. Kitu kimoja ambacho kinajijenga ni bilirubini (dutu ya njano inayoipa nyongo rangi ya njano), seli nyekundu za damu zinapokufa, hemoglobini iliyopo kwenye hizo seli zikivuja kwenye damu hemoglobini huwa bilirubini. Ini huchukua bilirubini hiyo nje ya damu na kuweka kwenye nyongo, nyongo huenda kwenye utumbo, kisha hutolewa nje pamoja na uchafu kutoka mwilini. Kama ini likipata matatizo, halitatoa bilirubini, kwa hiyo bilirubini itakaa mwilini: hii hufanya mtu aonekane wanjano na inajulikana kama homa ya manjano. Kwa hiyo macho na ngozi kuwa ya njano ni dalili za magonjwa ya ini.

Dalili nyinginezo ni:

  • Kutokwa damu kwa sababu ini halitengenezi protini ya ugandishaji ya kutosha
  • Kuvimba mwili
  • Kuchoka sana kwa sababu amonia ya ziada haiyeyushwi na ini
  • Kutokwa damu kwenye vena kubwa zilizovimba

Aina za magonjwa ya ini

Homa ya ini (kwa Kiingereza hepatitis): hii hutokea kama seli za ini zikiugua. Hii inaweza kutokana na maambukizi ya virusi. Pia inaweza kusababishwa na sumu. Sumu kuu ambayo mara kwa mara husababisha hii ni kileo (pombe). Inaweza ikawa kijenitikia, au sababu za mfumo wa kingamwili wenyewe.

Kusinyaa kwa ini (kwa Kiingereza cirrhosis): hii husababishwa na kufa kwa seli za ini ambao hutokea tena na tena. Kama seli za ini zikifa, tishu za makovu hujiunda. Hizi tishu huharibu muundo wa ini, hii hufanya ini lisifanye kazi vema. Lakini pia hufanya shinikizo kwenye vena ambayo huenda kwenye ini kubwa sana.

Unaweza pia kupata saratani ya ini. Hii inaweza ikawa saratani ya kuathiri sehemu nyinginezo ambayo inaweza kutokea kwenye sehemu nyingine kwenye mwili wako.

Tiba kwa magonjwa ya ini

Magonjwa mengine ya ini hutibika kirahisi kwa dawa.

Virusi vingine vya ini vinaweza kuzuiwa kabla havijaanza kwa chanjo.

Magonjwa mengine ya ini yanaweza tu kutibika kwa kupandikiza ini jingine.

Ini  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ini kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Ini KaziIni Magonjwa ya iniIniBinadamuKiungoMnyamaMwili

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Magonjwa ya machoKadi za mialikoKatibaUhifadhi wa fasihi simuliziMalariaNuktambiliMichezo ya watotoRiwayaBurundiDar es SalaamJacob StephenIntanetiNominoManchester United F.C.LatitudoPunyetoUkristo nchi kwa nchiKabilaUEFAUtataBendera ya ZanzibarUfeministiMuundo wa inshaKitaluMaudhuiMtaguso wa kwanza wa NiseaVivumishi vya urejeshiMzunguOrodha ya Watakatifu wa AfrikaMadawa ya kulevyaUfupishoMange KimambiJeshiRose MhandoSiasaMkoa wa ManyaraViwakilishi vya idadiMachweoIdhaa ya Kiswahili ya Radio TehranMadhehebuBiblia ya KikristoMtume PetroJamhuri ya Watu wa ZanzibarMahakamaTanganyika (ziwa)Orodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaNetiboliPonografiaWimboMfumo wa nevaWahayaWazaramoAgano la KaleJumuiya ya MadolaOrodha ya visiwa vya TanzaniaUtumbo mwembambaUyahudiAina za udongoVieleziNgono zembeTwigaUchumiIrene UwoyaUbuntuFananiWawanjiMazingiraChuiKisimaBabeliKibena (Tanzania)KidoleNdiziVita Kuu ya Kwanza ya DuniaVitendawiliMkoa wa RuvumaSarufi🡆 More