Hussein Ali Mwinyi: Rais wa Zanzibar

Hussein Ali Mwinyi (amezaliwa 23 Desemba 1966) ni tabibu na mwanasiasa nchini Tanzania aliyechaguliwa kuwa rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Hussein Ali Mwinyi: Rais wa Zanzibar
Picha ya Mwinyi.

Baada ya kipindi cha kazi ya tiba aliingia katika siasa kwa kuchaguliwa mbunge wa Mkuranga (Mkoa wa Pwani) mwaka 2000 akaendelea kugombea na kuchaguliwa bungeni katika jimbo la Kwahani (Zanzibar) tangu mwaka 2005. Anatokea katika chama cha CCM. Mwaka 2000 akateuliwa kuwa waziri katika serikali ya Tanzania alipokuwa naibu waziri ya afya mwaka 2000-2005, halafu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais kwa mambo ya Muungano 2006 - 2008, Waziri wa Ulinzi mwaka 2008- 2012 na tena 2014 hadi 2020. Mwaka 2012 hadi 2014 alikuwa Waziri wa Afya.

Hussein Ali Mwinyi ni mwana wa rais wa zamani Ali Hassan Mwinyi. Baada ya kusoma shule za sekondari za Azania na Tambaza, mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Tiba cha Marmara huko Istanbul, Uturuki alipohitimu masomo ya tiba mwaka 1991. Aliongeza masomo kwenye chuo cha kifalme cha tiba katika hospitali ya Hammersmith huko London, Uingereza alipopata shahada za uzamili na uzamivu (PhD) mnamo 1997.

Miaka 1993-1995 alifanya kazi ya tabibu kwenye Hospitali ya Muhimbili akaendelea kuwa tabibu na mwalimu kwenye Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kwenye miaka 1998 - 2000.

Mwaka 2020 Mwinyi aliteuliwa na CCM kuwa mgombea wake kwa urais wa Zanzibar akatangazwa mshindi na kuapishwa.

Tazama pia

Marejeo

Tags:

196623 DesembaMwanasiasaRais wa ZanzibarTabibuTanzaniaUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Ndoa katika UislamuKalenda ya KiislamuUgonjwa wa moyoBata MzingaChuo Kikuu cha Dar es SalaamPasaka ya KiyahudiBiashara ya watumwaUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiNguvaPasakaNenoMapambano kati ya Israeli na PalestinaVielezi vya mahaliJamhuri ya Watu wa ZanzibarMwenge wa UhuruMashariki ya KatiMajina ya Yesu katika Agano JipyaIsaWayback MachineHistoria ya TanzaniaMsalabaMkoa wa PwaniLuis MiquissoneMauaji ya kimbari ya RwandaKadi za mialikoMajira ya mvuaArsenal FCItikadiSheriaSenegalLil WayneLugha ya programuOrodha ya vitabu vya BibliaBaruaMadinaSiafuUkooJay MelodyHaitiLatitudoDaudi (Biblia)BawasiriMfumo wa JuaSiasaMuda sanifu wa duniaUgaidiSaratani ya mapafuInshaBungeNileJumuiya ya Afrika MasharikiWasukumaJumamosi kuuHistoria ya AfrikaChombo cha usafiriNomino za pekeeMbooZana za kilimoDumaUsawa (hisabati)LongitudoBotswanaRiwayaChelsea F.C.SikioOrodha ya majimbo ya MarekaniOrodha ya maziwa ya TanzaniaUkoloniBunge la TanzaniaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaUnju bin UnuqMajiMaisha🡆 More