Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia ni mmoja wa mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mgawanyo wa madaraka katika dola.
Mihimili mingine ni mahakama na serikali.
Bunge ni chombo kinachotokana na mfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka Uingereza. Kutokana na mfumo huo kuenea, mara nyingi Bunge la Uingereza huitwa "Mama wa Bunge" duniani.
Bunge la kwanza nchini Uingereza liliundwa wakati wa utawala wa Mfalme Henri III katika karne ya 13. Bunge hilo lina sehemu mbili, Bunge la Makabwela na Bunge la Mabwanyeye.
Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu huwa ndio kiongozi mkuu wa serikali bungeni.
Shughuli za bunge husimamiwa na mbunge aliyechaguliwa kama mwenyekiti, rais au spika wa bunge.
Kuna aina mbili za bunge:
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Bunge, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.