Mahakama ni mfumo wa wataalamu na kamati maalumu ambao unatafsiri na kutumia sheria katika jina la wananchi, la jamhuri au la mfalme.
Mahakama pia inatoa mfumo wa kutatua migogoro. Chini ya mfumo wa mgawanyo wa madaraka mahakama kwa ujumla haitungi wala haiundi sheria (ambayo ni kazi ya bunge) wala kutekeleza sheria (ambayo ni wajibu wa serikali), bali inatafsiri sheria na kutumia na kutekeleza katika ukweli wa kila kesi.
Mahakama ina kazi ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa watu wote.
Kwa kawaida kuna mahakama za ngazi mbalimbali; mahakama za juu zinapokea rufaa dhidi ya kesi za ngazi za chini hadi mahakama ya rufaa ya mwisho inayoitwa mahakama kuu au mahakama ya katiba. Tawi hili la mahakama lina uwezo wa kubatilisha sheria zisizolingana na katiba ya nchi.
Neno "mahakama" pia hutumika kumaanisha kwa pamoja maafisa ndani yake kama vile majaji, mahakimu na makarani wengine.
Kimsingi mahakama ina kazi ya kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya matumizi yao. Hali halisi sheria haziwezi kutaja kila kitu kinachoweza kutokea hivyo ni mahakama zinazoamua kwa njia ya kulinganisha kesi, sheria na maazimio ya mahakama yaliyotangulia.
Kwa hiyo mahakama zinashiriki kiasi katika kazi ya kutunga haki hasa pale ambako sheria za bunge zinaacha pengo.
Kidesturi muundo wa haki na sheria katika Uingereza na Marekani unaziachia mahakama nafasi kubwa zaidi kuendeleza taratibu za kisheria.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mahakama, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.