Mgawanyo Wa Madaraka

Mgawanyo wa madaraka ni fundisho la kisiasa linalotaka katika dola lolote itofautishwe mikono au mihimili 3 ya mamlaka.

Hiyo mihimili mitatu ni:

Falsafa ya mgawanyo wa madaraka

Hoja ya msingi ni kugawanya madaraka kati ya mikono mbalimbali inayotakiwa kutazamiana, kurekebishana na kusaidiana.

Wafuasi wa fundisho hili huona kwamba haki za watu huwa salama katika mfumo huu kuliko penye ile ambamo mamlaka yote imo katika mkono mmoja jinsi ilivyo katika hali ya udikteta.

Serikali inatawala kwa kutumia sheria lakini haiwezi kutunga sheria peke yake zitakazoongeza mno mamlaka yake.

Bunge linatunga sheria lakini haliwezi kufaidika na utekelezaji yake moja kwa moja.

Mahakama inaangalia sheria na kuamua juu ya matumizi yake. Inatakiwa kuzuia serikali inapokwenda nje ya sheria.

Historia

Mgawanyo Wa Madaraka 
Montesquieu

Mgawanyo wa madaraka si jambo jipya katika historia. Ulijitokeza tayari katika Ugiriki ya Kale.

Jamii kadhaa za Afrika zilipakana mamlaka ya chifu kwa kumpa sharti la kuelewana na washauri au baraza la wazee kwa mipango muhimu.

Fundisho la kisasa lilitungwa na Mfaransa Charles-Louis Montesquieu katika kitabu chake "De l'ésprit des lois" (Kuhusu roho ya sheria) alichokitoa mwaka 1748.

Marekani na Ufaransa zilikuwa nchi za kwanza zilizoingiza mfumo huo katika katiba zao.

Siku hizi ni nchi nyingi duniani zinazofuata mfumo huo.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Tags:

Mgawanyo Wa Madaraka Falsafa ya mgawanyo wa madarakaMgawanyo Wa Madaraka HistoriaMgawanyo Wa Madaraka TanbihiMgawanyo Wa Madaraka MarejeoMgawanyo Wa Madaraka Viungo vya njeMgawanyo Wa MadarakaDolaMamlakaSiasa

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

UtumwaBahashaTiktokMiundombinuKitenzi kikuuShambaBungeMuundo wa inshaAzimio la ArushaUaKata za Mkoa wa Dar es SalaamIdara ya Usalama wa Taifa (Tanzania)Hifadhi ya mazingiraOrodha ya viongoziNuktambiliMalengo ya Kiswahili kuwa lugha ya taifaRiwayaSentensiOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaMajeshi ya Ulinzi ya KenyaMohamed HusseinMishipa ya damuAina za manenoYesuAdolf HitlerShahawaNguruwe-kayaSayansiMbeya (mji)Maana ya maishaWimboJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaMbagalaWaheheMeta PlatformsAlama ya uakifishajiKiongoziWanyakyusaImaniHafidh AmeirMikoa ya TanzaniaJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoOrodha ya Marais wa UgandaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiManchester CityWilaya ya UbungoMkutano wa Berlin wa 1885KonyagiMasafa ya mawimbiSilabiKamusiMohammed Gulam DewjiHaki za binadamuMilango ya fahamuHuduma ya kwanzaDubaiUkabailaWhatsAppMkoa wa TangaMzeituniMoses KulolaVivumishi vya kumilikiSemiMbuga za Taifa la TanzaniaFutiUyahudiMazungumzoMisimu (lugha)TafsiriAmina ChifupaVivumishi vya kuonesha🡆 More